Obama aanza kumlaumu Trump kwa kushindwa kulikabili janga la Corona. Asema Trump anaishughulikia Corona kama janga la machafuko

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
8de3edc32b321271078b1b5bbd94daef

Donald Trump, Rais wa Marekani
BARACK Obama, Rais Mstaafu wa Marekani, amemtuhumu rais wa sasa Donald Trump kwamba ameshindwa kuukabili ugonjwa wa mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19). Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).
Kupitia kituo cha Televisheni cha CNN, Obama ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na waiokuwa wafanyakazi wake wa Ikulu, sambamba na timu ya kampeni ya uchaguzi ya Joe Biden.
Amesema, mbinu anazotumia Trump kukabiliana na janga la corona katika taifa hilo, hazijasaidia chochote na kwamba, yeye (Trump) ni mwingoni mwa watu wanaopaswa kulaumiwa kwa vifo vingi vilivyotokea.

Mpaka tarehe 9 Mei 2020, Marekani kumetokea vifo vya watu zaidi ya 77,000 vilivyotokana na corona. Maambukizi yamefikia watu zaidi ya milioni 1.2.

Obama amesema, takwimu hizo zimeweka rekodi ya juu kabisa katika uso wa dunia kutokana na Trump kushindwa kujua namna ya kuwaokoa Wamarekani kutokana na janga hilo.

Trump aliahidi kwamba, mpaka mwezi Februari mwaka huu, ugonjwa huo ungekuwa umemalizwa kabisha ndani ya mipaka ya taifa hilo.

Hata hivyo, ilivpofika katikati ya Machi, Trump alieleza kwamba ugonjwa huo umekuwa ukisambaa kwa kiwango cha juu ndani ya taifa hilo.

Ilipofika Aprili, Trump alidai dawa za kuua bakteria zinaweza kuzuia virusi, hata hivyo wanasayansi ndani ya taifa hilo walilikana kwamba si kweli.

Kutokana na kuchanganyikiwa na kasi ya maambukizi, wiki iliyopita Trump aliahidi atavunja kikosi kazi kinachopambana na kusambaa kwa virusi vya corona, baadaye akatangaza kuachana na mpango huo.

Ikulu ya Marekani imemtetea Trump kwamba amekuwa akifanya kazi kubwa kuhakikisha anakabiliana na corona na kwamba, ameliokoa taifa hilo kutumbukia katika janga kubwa
 
Rais mstaafu anamkosoa Rais aliyepo madarakani....nzuri sana hii.

Huku kwetu (Tz) ngumu kutokea hili kwa sababu....
 
Taifa kubwa kama US kuongozwa na likichaa kama TRUMP ni Janga Baya Sana Aseee

Turmp Akili zake Hazina Akili.....

Sent using My COVID-19
 
8de3edc32b321271078b1b5bbd94daef

Donald Trump, Rais wa Marekani
BARACK Obama, Rais Mstaafu wa Marekani, amemtuhumu rais wa sasa Donald Trump kwamba ameshindwa kuukabili ugonjwa wa mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19). Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Amesema, mbinu anazotumia Trump kukabiliana na janga la corona katika taifa hilo, hazijasaidia chochote na kwamba, yeye (Trump) ni mwingoni mwa watu wanaopaswa kulaumiwa kwa vifo vingi vilivyotokea.

Mpaka tarehe 9 Mei 2020, Marekani kumetokea vifo vya watu zaidi ya 77,000 vilivyotokana na corona. Maambukizi yamefikia watu zaidi ya milioni 1.2.

Obama amesema, takwimu hizo zimeweka rekodi ya juu kabisa katika uso wa dunia kutokana na Trump kushindwa kujua namna ya kuwaokoa Wamarekani kutokana na janga hilo.

Trump aliahidi kwamba, mpaka mwezi Februari mwaka huu, ugonjwa huo ungekuwa umemalizwa kabisha ndani ya mipaka ya taifa hilo.

Hata hivyo, ilivpofika katikati ya Machi, Trump alieleza kwamba ugonjwa huo umekuwa ukisambaa kwa kiwango cha juu ndani ya taifa hilo.

Ilipofika Aprili, Trump alidai dawa za kuua bakteria zinaweza kuzuia virusi, hata hivyo wanasayansi ndani ya taifa hilo walilikana kwamba si kweli.

Kutokana na kuchanganyikiwa na kasi ya maambukizi, wiki iliyopita Trump aliahidi atavunja kikosi kazi kinachopambana na kusambaa kwa virusi vya corona, baadaye akatangaza kuachana na mpango huo.

Ikulu ya Marekani imemtetea Trump kwamba amekuwa akifanya kazi kubwa kuhakikisha anakabiliana na corona na kwamba, ameliokoa taifa hilo kutumbukia katika janga kubwa
Wanasiasa hasa anapokuwa mpinzani wako siku zote anakuwa mtu wa kulaumu,hawajui huu muda si wa kulaumiana kama una njia za kutatua tatizo wape wenzio,US wana hali mbaya wamezidiwa ila ndio vile wanajikaza.

Sasa unamlaumu Trump utazani yy ndiye anatoa roho za watu ,hamna kiongozi anayependa watu wake wafe.
 
Hivi JK angetoa maoni km hayo kwa magufuli angekutana na zahama gani?
 
Hahah kumbuka mkewe na mtoto wake ni wabunge.

Hapo tungeweza kutumia kale ka-sheria kadogo tu ka ukivuliwa uanachama wa chama chako unakua umepoteza tayari ubunge.
 
Coronavirus COVID-19 ni janga, nashauri Trump atumie mbinu Kama za Rais wangu mpendwa.
Afunge siku tatu, maombi, kujifukiza na kufuata dawa Madagascar kutaiokoa Marekani 🇺🇸🇺🇸🇺🇸 walijaribu
 
Ukiupima huu ukosoaji wa Trump utagundua kuna jambo wengi hawajalishtukia,hapa ni wakati wa kutazama picha kwa makini zaidi.
 
Back
Top Bottom