Kamati ya Bunge kumhoji Trump

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,568
Washington. Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump ameitwa mbele ya Kamati ya Bunge (Capitol Hill) kuhojiwa kuhusiana na vurugu za wafuasi wake waliovamia Bunge wakipinga ushindi wa Joe Biden kuwa Rais wa 46 wa Marekani.

Kamati hiyo ilikuwa ikichunguza vurugu zilizotokea Januari 6, 2021 baada ya wafuasi wa Trump kuvamia Bunge wakijaribu kuzuia wabunge wasitambue ushindi wa mgombea wa Democratic, Joe Biden.

Vurugu hizo zilisababisha vifo vya watu wanne, akiwamo mwanamke aliyepigwa risasi na polisi. Wafuasi hao waliingia ndani ya ukumbi wa Bunge na kuleta vurugu, huku wengine wakiingia ofisi ya Spika na kukaa kwenye kiti chake.

Trump, aliyekuwa akitetea muhula wake wa pili kwa chama cha Republican alishindwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, lakini aligomea matokeo ya uchaguzi akidai kaibiwa kura na hakwenda kwenye uapisho wa Biden.

Kamati ya Bunge iliyokuwa ikichunguza tukio hilo imetoa wito kwa Trump kuhojiwa kwenye kamati hiyo.
Wito huo umesomeka: “Wewe ulikuwa chanzo cha harakati za kuvuruga matokeo ya uchaguzi. Ulijua harakati hizo ni kinyume cha sheria na katiba.”

Kamati hiyo imesema kama Trump atadharau wito huo anaweza kufunguliwa mashitaka ya jinai.
Trump amepewa hadi Novemba 4, 2022 awe amejibu na kutakiwa kufika mbele ya kamati hiyo Novemba 14.
“Kama hatafika, kamati ina uwezo wa kulipeleka suala hilo kwenye idara ya mashitaka kwa ajili ya kuendelea na mashitaka ya jinai,” ilisomeka taarifa hiyo.

Wito huo umetolewa ikiwa zimepita siku chache baada ya mmoja wa wasaidizi wa Trump, Steve Bannon kupigwa faini ya dola 6,500 na kifungo cha miezi minne jela kwa kuingilia Bunge.

Alipewa adhabu hiyo baada ya kukataa kuipa kamati ya Bunge nyaraka walizokuwa wamezitaka kutoka kwake.
Msaidizi mwingine wa Trump, Peter Navarro naye ameitwa mbele ya kamati hiyo mwezi ujao baada ya kukataa kutoa ushirikiano kwa kamati hiyo.

Vurugu zilivyokuwa
Wafuasi wa Trump waliokuwa na hasira waliandamana huku wakiimba: “Tunamtaka Trump”, huku mmojawao akipigwa picha akiwa ameketi kwenye kiti cha Spika wa Bunge.

Wakati wa vurugu hizo, Trump alilazimika kurekodi ujumbe kwenye video na kuutuma katika mtandao wa Twitter akitoa wito kwa wafuasi wake kuondoka katika majengo ya Bunge, lakini naye akawa anaendeleza madai kuwa Democrats waliiba kura.

“Najua machungu yenu, najua mmevunjika moyo,” Trump alisema. “Lakini, lazima sasa mrejee nyumbani, lazima tuwe na amani...hatutaki yeyote ajeruhiwe.”

Wafuasi wa Trump wenye hasira walivuka mipaka ya usalama iliyowekwa na kusimama kandokando ya Bunge wakati wabunge walipokuwa wakikutana kumuidhinisha Rais mteule Joe Biden kama mshindi wa uchaguzi uliofanyika Novemba 2020.

Waandamanaji walizunguka jengo la Bunge huku wabunge nao wakisindikizwa kutoka bungeni humo na polisi.
Biden kwa upande wake alisema huo ni “uasi”, huku Trump akitoa ujumbe kwa njia ya video akiwataka wafuasi wake kutoka bungeni na kurejea nyumbani.

Uvamizi huo ulisababisha Bunge la kuidhinisha ushindi wa Biden kuahirishwa.
Waandamanaji walifika katika majengo ya Bunge kutokana na mkutano uliopewa jina la “Save America Rally”, ambapo Trump aliwataka wafuasi wake kuunga mkono wabunge wanaopinga kuidhinishwa kwa Biden kama mshindi.

Trump alikataa kukubali kuwa ameshindwa katika uchaguzi wa Novemba 3, 2020 na kudai mara kadhaa kwamba uchaguzi huo ulikumbwa na wizi wa kura bila kutoa ushahidi wowote.

Mashitaka ya Trump
Wabunge walimshutumu Trump kwa kuchochea vurugu kufuatia uvamizi wa majengo ya Bunge na kutaka ashitakiwe na kuondolewa madarakani kabla ya Rais mpya kuapishwa.

Wabunge waliounga mkono mashitaka dhidi ya Trump walisema alihusika kuwachochea wafuasi wake kuvamia majengo ya Bunge Capitol Hill mjini Washington.

Wabunge 10 wa chama cha Republic waliungana na wa Democrat wakisema Rais Trump anapaswa kuwajibishwa, huku wakionya kuhusu kitisho cha dhahiri ikiwa Bunge litamuacha bila kumwajibisha kabla ya Joe Biden kuchukua madaraka.

Zikiwa zimebaki siku saba tu kabla ya muda wa Trump madarakani kumalizika, wabunge wa Democrat waliharakisha mchakato wa kutaka kumvua madaraka, lakini Makamu wa Rais, Mike Pence alikataa kuitikia wito wa kutumia ibara ya 25 ya katiba ya nchi hiyo kumuondoa ofisini.

Hakuna aliye juu ya sheria
Baada ya kura ya kutaka Trump ashitakiwe kupingwa na wabunge, Spika Nancy Pelosi alisema hatua hiyo ya wabunge inathibitisha kuwa hakuna yeyote aliye juu ya sheria.

“Kwa pande zote mbili, Bunge limedhihirisha kwamba hakuna aliye juu ya sheria, hata Rais wa Marekani. Na kwamba ni wazi kuwa Trump ni kitisho cha sasa kwa taifa letu na kwa mara nyingine tumetekeleza wajibu wetu kwa kulinda katiba ya Marekani.

“Na sasa kwa masikitiko haya yanamaanisha kwa nchi yetu kuhusu Rais atakayechochea uasi atastahili kukamatwa kwa kufunguliwa mashtaka,” alisema Pelosi.

Trump ni kati ya marais watatu wa chama cha Republic ambao wabunge walipitisha mashtaka dhidi yao, lakini huenda akawa wa kwanza kushtakiwa katika Bunge baada ya kuondoka ofisini.

Mara ya kwanza mashtaka ya kutaka Trump avuliwe madaraka yalipitishwa na Bunge Desemba 2019, kuhusiana na shinikizo lake kwa Ukraine. Hata hivyo, Bunge lilipiga kura kumuondolea lawama.

Chanzo: Mwananchi
 
Hiyo kauli ya huyo Bi pelosi ndio kauli inayo ashiria Muhimili unao jitegemea sio huku kwenye shimo la #@()1.
 
Back
Top Bottom