usser
JF-Expert Member
- Sep 25, 2015
- 13,978
- 14,092
Kama kuna nnao wa heshimu jf kwa michango yao hekima,ushaur mzur bhas ww n no 2 maana no 1 ipo kwa mzizi mkavu anyway heshima kwakoHongera sana mpendwa, na mzidi kumtanguliza Mungu kwenye ndoa yenu. Msiache kumshukuru Mungu hata kama ndoa yenu ina siku moja, kuna watu walifunga ndoa, kufika kwenye honey moon tu zikavunjika, nyie kufikisha hiyo miaka kwenye ndoa ni kwa neema tu. Watu tumeshazoea na tunapenda kweli kusikia habari mbaya kuhusu ndoa, sijui kwa sababu ndoa zetu zishajifia ndo maana tunatamani na za wenzetu zijifie pia? Mtu akimsifia mkewe, utawasikia tu watabiri wa ndoa za watu "ndoa yenu bado mpya ooh huwajui wanawake wewe lazima tu atakuumiza", sasa usimsifie mkeo kwa sababu tu unahisi mbeleni atasumbua, jamaniiii. Mpende muheshimu, mjali na mthamini mkeo as if there is no tomorrow. Enjoy ndoa yako kiasi kwamba hata ukitwaliwa leo, utasema tu Mungu ahsante kwa ajili ya ndoa yangu. Hakuna maisha yasiyo na changamoto, hamuwezi tu kucheka siku zote 365, so tatizo likitokea, shirikianeni kwenye kulitatua, then uchekeni wakati ujao
Wengine hapa kuwaonyesha wake zao wanavyowajali au kuwapenda watakwambia si sawa. Ila subiria sasa wanavyoicare michepuko yao mtcheew. Unampenda mkeo, just muoneshe eeh, otherwise una Mtu mwingine wa kumuoneshea. Kwa nini uishi na Mtu kwa machale/kutokumiani as if kuna kitu kibaya amekufanyia? Kwa nini uishi maisha yako kwa kutumia mifano ya walioharibu maisha yao? Ndoa ni yako, itengeneze iwe vile unavyoitaka wewe. Nawatakia maisha ya amani na furaha, zibeni masikio kwa sisi tunaoendekeza mifano ya walioshindwa. Nyie mkishindwa ndo furaha yetu, maana mtaongeza list yetu ya walioshindwa eishh
Nkifkia kuoa please usisite kupokea cad ya mwaliko