Oa ujue thamani ya mwanamke

cosa nostra

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
1,773
1,805
Najua hii itaonekana tofauti..

Lakini hii imenitokea live, since nimeoa nazidi kumpenda mke wangu zaidi ya kipindi tulipokua wapenzi tu kabla ya ndoa. Kipindi hicho nilikua naweza kumchukulia poa hata simu zake nilikua naweza potezea tu na nikatoka club alone.

Lakini saizi ikitokea sijamuona siku chache tu napata shida sana na weza kuita wivu wa mapenzi lakini with very good feeling.

Kipindi amejifungua akaenda kwao kupumzika kidogo nyumbani palikua ovyo sana tofauti na zamani, ningefurahia uhuru na kufanya yangu lakini nimejikuta nakua mpweke sana na nikamrudisha haraka sana.

Saizi tumepata mtoto na namuona shujaa sana kwa hali aliyopitia kipindi chote kwa ujauzito. Nimejikuta namheshimu sana bila kulazimishwa.

Sijui this feeling ni kawaida au nitofauti na kawaida?
 
“A man who doesn't spend time with his family can never be a real man.”

Mario Puzo, The Godfather

Najua hii itaonekana tofauti

lakini hii imenitokea live, Since nimeoa nazidi kumpenda mke wangu zaidi ya kipindi tulipokua wapenzi tu kabla ya ndoa.Kipindi hicho nilikua naweza kumchukulia poa hata simu zake nilikua naweza potezea tu na nikatoka club alone

Lakini saizi ikitokea sijamuona siku chache tu napata shida sana,Na weza kuita wivu wa mapenzi lakini with very good feeling,

Kipindi amejifungua akaenda kwao kupumzika kidogo ic nyumbani palikua ovyo sana tofauti na zamiani ningefurahia uhuru na kufanya yangu.lakini nimejikuta nakua mpweke sana na nikamrudisha haraka sana,

Saizi tumepata mtoto na namuona shujaa sana kwa hali aliyopitia kipindi chote kwa ujauzito.Nimejikuta namheshimu sana bila kulazimishwa,

Sijui this feeling ni kawaida au nitofauti na kawaida?
 
Aah useme ukweli tu ile mahari uliyomtolea ndio inakuuma. Sio hizo sababu ulizotoa.
Ila kuwa makini kwa huo upendo uliopitiliza maana binadamu yoyote akijua anapendwa lazima maringo yaje.
Mpende lakini usizidishe mpaka akakuona boya ukaja tena hapa kuomba ushauri.
 
jitahidi usimuoneshee hizo feeling machoni pake, ziishie huko huko moyoni mwako... akijua tu unamthamini na kumuheshimu kiasi hicho UTAKOMA... ni jambo zuri sana kwa kweli unalofanya, ila lazima uijue saikolojia ya mwanamke ili uendane nae pasipo kuathiri saikolojia yako.
 
Hongera sana kwa kuwa na ushajaa huo. Hongera sana mkuu.

Lakini kiuhalisia NDOA ni kijiwe cha usaliti, unafiki, uongo na unyanyasaji, wenyewe wazungu wanasema 'hypocritical institution'

Bill Clinton na ushawishi wote aliokuwa nao, heshima, elimu, pesa na zaidi yote kupata mke smart 'Hillary' lakini alizini na binti mbichi Monica Lewinsky, hakuishia hapo akamgonga Gennifer Glowers tena akiwa ikulu. Hakuishia hapo akambanjua Paula Jones na Juannita Broad.

Watu wanatembea usoni wanaonekana wana furaha na amani, lakini kiuhalisia chumbani hakuna mapatano, vita, chuki, ugomvi na lawama kibao. Hata Barack na Michelle kuna kipindi hawakuongeleshana ikulu kwa siku 4, na ni hawa hawa wanalala kitanda kimoja.

Mara nyingi wanawake ndio victims.

Siku hizi hapa mjini nahisi hata na huko vijijini ndoa imekua ni fashion. Masela wanaoa wapate uhakika wa kupakua muda wowote na mabinti wanatafuta ndoa wasionekane magume gume.
 
point taken

hii nikawaida wewe na mama yako tu mlishawahi kubadilikiana itakua mwanamke mlie juana ukubwani,whats needed is kuwa marafiki wawazi na kupendana,mimi ni dume huwa natamani mademu lakini nikikumbuka wife home na change mind fasta kwa heshima yake.una sacrifice for good family life uta enjoy sana
 
Hongera sana kwa kuwa na ushajaa huo. Hongera sana mkuu.

Lakini kiuhalisia NDOA ni kijiwe cha usaliti, unafiki, uongo na unyanyasaji, wenyewe wazungu wanasema 'hypocritical institution'

Bill Clinton na ushawishi wote aliokuwa nao, heshima, elimu, pesa na zaidi yote kupata mke smart 'Hillary' lakini alizini na binti mbichi Monica Lewinsky, hakuishia hapo akamgonga Gennifer Glowers tena akiwa ikulu. Hakuishia hapo akambanjua Paula Jones na Juannita Broad.

Watu wanatembea usoni wanaonekana wana furaha na amani, lakini kiuhalisia chumbani hakuna mapatano, vita, chuki, ugomvi na lawama kibao. Hata Barack na Michelle kuna kipindi hawakuongeleshana ikulu kwa siku 4, na ni hawa hawa wanalala kitanda kimoja.

Mara nyingi wanawake ndio victims.

Siku hizi hapa mjini nahisi hata na huko vijijini ndoa imekua ni fashion. Masela wanaoa wapate uhakika wa kupakua muda wowote na mabinti wanatafuta ndoa wasionekane magume gume.
hizo issue za kawaida sana, ili kufanikiwa na ndoa nzuri usisome mifano kwa watu negative wala msijifananishe na ndoa yoyote ndio mwanzo wa kuharibu,Be real na mwanandoa wako soma maandiko yanasema nini kumbuka Agano la ndoa Basi,Mengine mwachie Mungu
 
Aah useme ukweli tu ile mahari uliyomtolea ndio inakuuma. Sio hizo sababu ulizotoa.
Ila kuwa makini kwa huo upendo uliopitiliza maana binadamu yoyote akijua anapendwa lazima maringo yaje.
Mpende lakini usizidishe mpaka akakuona boya ukaja tena hapa kuomba ushauri.

Mahali niliyotoa haizidi pesa niliyo wahi choma club kwa pombe na malaya,kupenda sio teo tendo la kupretend liko automatic sasa acts of love zikimlewesha basi coz ic she gives me back the same
 
Acha kuuliza kama ni kawaida au ajabu, furahia wakati huu sasa hivi kama kuna mengine yatakuja mbele yakukute ukiwa bize na furaha mpaka yasijue pa kupitia, kuliko yakukute unashangaa kama ulivyo ndivyo unavyotakiwa kuwa ama laa.

Hata hivyo acha kushika shika simu yake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom