Oa ujue thamani ya mwanamke

Oa ujue thamani ya mwanamke

Mkuu ndoa bado changa sana hiyo, kuna rafiki yangu aliishi kwa amani sana kwenye ndoa. Amekuja kusalitiwa live na mkewe ndoa ikiwa na miaka 18. Mpaka mda huu naandika walishaachana!
Sikuombei mabaya la hasha! Muombe sana Mungu katika ndoa yako asije yule mwovu akawatenganisha.
 
Poa bro..Fikisha salamu kwa familia

Zimefika, nikuwa namwambia douta leo kwamba napitisha karatasi ya mchango wa kumpeleka kijana English media, isije akashindwa kuongea na Akili Kubwaz tukipata mwaliko wa Chai pale Double Tree.
 
Zimefika, nikuwa namwambia douta leo kwamba napitisha karatasi ya mchango wa kumpeleka kijana English media, isije akashindwa kuongea na Akili Kubwaz tukipata mwaliko wa Chai pale Double Tree.
Teh teh.. Kweli aisee.. Aunt zake itabidi iwahusu hii..
 
Ili ufurahie ndoa pata mwenza sahihi wa ku-compliment madhaifu yako, ukipata 'msikule' ndoa ni chungu. Waliosema kosea kujenga ila sio kuoa hawakukosea hata kidogo.
 
Hongera sana mpendwa, na mzidi kumtanguliza Mungu kwenye ndoa yenu. Msiache kumshukuru Mungu hata kama ndoa yenu ina siku moja, kuna watu walifunga ndoa, kufika kwenye honey moon tu zikavunjika, nyie kufikisha hiyo miaka kwenye ndoa ni kwa neema tu. Watu tumeshazoea na tunapenda kweli kusikia habari mbaya kuhusu ndoa, sijui kwa sababu ndoa zetu zishajifia ndo maana tunatamani na za wenzetu zijifie pia? Mtu akimsifia mkewe, utawasikia tu watabiri wa ndoa za watu "ndoa yenu bado mpya ooh huwajui wanawake wewe lazima tu atakuumiza", sasa usimsifie mkeo kwa sababu tu unahisi mbeleni atasumbua, jamaniiii. Mpende muheshimu, mjali na mthamini mkeo as if there is no tomorrow. Enjoy ndoa yako kiasi kwamba hata ukitwaliwa leo, utasema tu Mungu ahsante kwa ajili ya ndoa yangu. Hakuna maisha yasiyo na changamoto, hamuwezi tu kucheka siku zote 365, so tatizo likitokea, shirikianeni kwenye kulitatua, then uchekeni wakati ujao

Wengine hapa kuwaonyesha wake zao wanavyowajali au kuwapenda watakwambia si sawa. Ila subiria sasa wanavyoicare michepuko yao mtcheew. Unampenda mkeo, just muoneshe eeh, otherwise una Mtu mwingine wa kumuoneshea. Kwa nini uishi na Mtu kwa machale/kutokumiani as if kuna kitu kibaya amekufanyia? Kwa nini uishi maisha yako kwa kutumia mifano ya walioharibu maisha yao? Ndoa ni yako, itengeneze iwe vile unavyoitaka wewe. Nawatakia maisha ya amani na furaha, zibeni masikio kwa sisi tunaoendekeza mifano ya walioshindwa. Nyie mkishindwa ndo furaha yetu, maana mtaongeza list yetu ya walioshindwa eishh
 
kweli wabongo tunadanganyana sana vijiweni lakini wenzetu wazungu wako real kuonesha feelings sasa waswahili ndio maana wanagongewa kilahisi sababu ya kujifanya makauzu externaly kumbe ndani Hoi
Mimi kama nampenda mtu nitamuonyesha kwa maneno, matendo na kila kitu mpaka labda mwenyewe aniambie yatosha.

Siwezi kuudhurumu moyo wangu nafasi hiyo adimu.
 
Ndoa halisi huanza baada ya miaka kumi toka siku ya kufunga ndoa. Mungu akufanyie kicheko mkuu daima
 
Uongeze maombi shetan awapitie mbali maana akisogea karbu hata nyumban utapaona kamaa chooo
 
eeh enjoy mwaya... Ndiyo raha ya ndoa mwaego
 
Back
Top Bottom