Oa mwanamke anayekupenda!


Utajengaje familia na MTU asiyekupenda..mfano yule niliyemuacha ...hakuheshimu...ana kudharau..KIBURI..hata unyumba anakunyima ..ana kuoa mpaka akijisikia..
anakutolea Kauli za kuudhi...n.k

Familia inajengwa katika msingi WA KUHESHIMIANA, KUPENDANA, AMANI...familia Gani huku mnachukiana...mna DHARAULIANA..KIBURI..

nafikiri tunatofautiana .. labda KWA sababu mwanzo sikuzoea KUDHARAULIKA kutokuheshimiwa nikishindwa kuvumilia dharau..

MANA MIND YOU THAT...utaishi naye MKATABA WA maisha ,utaishije naye maisha Yako yote na MTU asiyekuheshimu ..mtajengaje hiyo familia..
OA MWANAMKE ANAYEKUPENDA
 
Hata kama anakupenda vipi. Lakini kuna siku atakubadilikia hutoamini kama kweli ni yeye,, mwanamke si wakumuamini hata kidogo..
 
MTU anakusemesha Kauli za dharau.. anasema hivi sijui ilikuwaje mpaka nikazaa na WEWE?n
kwanza sijui ulinipataje.. Mimi siyo hadhi Yako..x wangu alikuwa ananihudumia..KWAKO hapa pesa huna..pamoja na kujitahidi lakini bado hakuheshimu..na maneno MENGI ya dharau

Utajengaje familia na mwanamke anayekudharau??
 
Naunga mkono hoja.
 

OA MWANAMKE ANAYEKUPENDA
 
Haiwezekanii
 
Mkuu sidhani kama wewe na huyo mtuhimiwa wako mlioana…………. Mlibebana ili kuona kama MNAPENDANA ili muoane

Tatizo la KUPENDANA sio lake tu, hata kwako pia………… inawezekana mliweka mbele mapenzi kwanza, na tatizo la mapenzi kila mtu ana KIPIMO chake kwamba nikifanyiwa hivi ndio kweli napendwa
Na hakika hata yeye akiulizwa atakua na hadithi kama zako

Mkuu sisemi ukaokote hata Malaya anayejiuza uoe……. Hapana
Tafuta mwanamke anayejielewa na mwenye akili ya kuweza kutunza watoto wako na kuwa mshauri wako mkuu……..na sio unaye/anayekupenda sana sababu huo upendo LAZIMA utapoa lakini kilichokifanya umuoe kitabaki
 
Ni sahihi lakini endapo upendo ukiisha hata suala la kutunza watoto.. sidhani kama utaliona sababu hapo mwanzo kulikuwa na upendo ndani yake....
 
Ni sahihi lakini endapo upendo ukiisha hata suala la kutunza watoto.. sidhani kama utaliona sababu hapo mwanzo kulikuwa na upendo ndani yake....
Mkuu ukiona wanandoa wanaishi pamoja miaka sijui 20 ujue hakuna DHORUBA hawajawahi kupitia Lakini waliweka misingi ya FAMILIA kwanza

Hakuna ndoa ambayo ule upendo wa mwanzo 100% ukaendelea hivyo hivyo maisha yenu yote………. Kuna wakati unashuka hadi negative 0 lakini utawaona wakiwa mbele za watu tabasamu kubwaaaa
Mwisho wa siku wanakubali yaishe na maisha yanaendelea
 
Ni sahihi lakini endapo upendo ukiisha hata suala la kutunza watoto.. sidhani kama utaliona sababu hapo mwanzo kulikuwa na upendo ndani yake....

inatokea mwanamke ANAYEKUPENDA pia anakuwa anajielewa,moambanaji,superwoman,pia akwa mshauri MZURI KWAKO...na mara nyingi mwanamke ANAYEKUPENDA anakuwa na SIFA hizo zote na anakuwa na future na maisha yenu na familia.

Ila asiyekupenda hata BAJETI TU Hana ,Hana HURUMA na WEWE,Hana future na WEWE anakuwa ni gold digger.. inawezekana tunaongea kitu kimoja katika angel tofauti..au tunaongea vitu tofauti.
 
Sasa inabidi umpate ambae ni mnyenyekevu na anekubali yaishe.. lakini ukutane na KIGINGI.. mkuu utatamani muachane tuu....
 
Mkuu sijamaanisha uoe asiyekupenda………….. Msingi usiwe kupendwa sanaaaa, msingi uwe je huyu mwanamke ana akili ya kusimamia familia yako kama msaidizi wako hata mapenzi yakiisha?

Hata huyo unaye mlalamikoa lazima mwanzoni alikuonyesha upendo ndio maana ukamchukua mkazaa naye, na upendo ulipokwisha sasa hakuna rangi unaacha kuona
 
Zamani tulikua tunaoa ili KUJENGA familia………… Siku hizi mnaoana kwasababu mnapendana
Aisee, tahadhari ya kwanza ni kuhakikisha hautafuti ushujaa kwenye tabia za watu eti nitambadilisha tabia yake. Tahadhari ya pili heshimu maneno ya wahenga, kama wahenga walishanyoosha kidole sehemu kuwa uwe mwangalifu, usiwabishie vinginevyo huwe umejiandaa kisaikolojia. Tahadhari ya tatu ukianza mjadala wa kuwa na familia kwa kumwambia tukapime afya zetu kwanza tucheki maradhi tuliyonayo na tuyatafutie ufumbuzi, The Rhesus factor ( wataalamu nisaidie kutafsiri) na kadhalika na huyo unayemlenga haonyeshi seriousness unapoeleza haya, anachekacheka tu. Jua hapo hakuna kitu. Yaa Nne ingawa si umuhimu sana ukiona unaitwa majina mazuri tu pale unapotoa mkwanja, ndala mkononi na kimbia haraka sana.
Ya tano na hii ni.muhimu sana, kuwa makini na maneno anayojitamkia mifano, aah mimi nikiwa sehemu nikaona hapaeleweki sijiulizi mara mbili naondoka, sitaki shida mimi, raha jipe mwenyewe! Huyo kukusaliti ni dakika sifuri utakapopata changamoto

Nina imani hii itasaidia wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…