Nywele hizi ni utalii tosha

Nywele hizi ni utalii tosha

Bubu Msemaovyo

Platinum Member
Joined
May 9, 2007
Posts
4,189
Reaction score
3,552
Kama mtu unaweza kubuni jinsi ya kupata kipato basi mama huyu anao mradi tosha wa kumuingizia kipato kwa nywele zake Rasta ndefu kiasi hiki.

Rasta ndefu.jpg
View attachment 108771


Asha Mandela (47) kutoka Atlanta, Georgia amefuga nywele hizo kwa miaka 25. Inasemekana zina urefu wa futi 55. Asha amegoma kuzikata nywele zake licha ya kushauriwa na madaktari kutokana na madhara ya kupooza ambayo anaweza kuyapata. Alisema nywele hizo zimekua kama sehemu ya mwili wake, ni maisha yake hivyo kamwe hawezi kuzikata.

Rasta.jpg

Asha huzichukulia nywele hizo kama mtoto wake. Humchukua siku mbili kuziosha na kuzikausha nywele hizo.

Rass.jpg
View attachment 108777
View attachment 108778
View attachment 108779

"Akili ni nywele kila mtu anazake"

Huyu Dada Mungu akimchukua kaburi lake litakuwa ni makumbusho ya taifa.
 
Watu wanafuga Kuku,Mbuzi,n.k wapate
kitoweo yeye anafuga nywele.
 
Naona anaitafuta Guiness Book of Records kwa nguvu, kila laheri ataipata tu.
 
Akizifungia nywele mgongoni mtoto atamweka wapi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom