Jinsi wazazi tunavyowaharibu watoto wetu wenyewe

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
14,769
10,650
  • Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Leo tuone ni mambo gani ya msingi kabisa ambayo kama wazazi tumeyaacha na kupelekea kuharibu maadili ya watoto wetu
  • 1. Kumpa uhuru uliovuka mipaka
  • Kwa kawaida mtoto awe wa kiume ama wa kike huwekewa mipaka, mfano muda wa kutoka nyumbani, utaratibu wa utokaji, muda wa lazima kuwapo nyumbani, namna ya kuongea na wazazi na ndugu na jamaa n.k. Siku hizi wazazi tumewapa Watoto wetu uhuru kupitiliza, mtoto anaweza kutenda DHAMBI KUBWA ya kuondoka nyumbani akapotea hata masaa mawili lakini bado mzazi asishituke. Hata akigundua atamwita tu mzururaji na kesi itaishia hapo. Siku akirudi na mimba ndipo wazazi tunajidai kuchachamaa, tuna react kwenye matokeo badala ya kutibu chanzo. Mtoto akija kuwa shoga tunaanza kupambana naye kwa kosa tulilolifanya wenyewe kwa kutomjengea misingi bora.

  • Siku hizi ni kawaida tu wazazi wanapokuwa wakijadili mambo mbalimbali kukuta vitoto navyo vikijiingiza katikati ya maongezi kuongoza mijadala. Wakuu, enzi za ujima hii ilikuwa ni dhambi kubwa na iliadhibiwa papo kwa papo. Kijana amaye bado hana analojua kuhusu dunia ni utovu w adamu kuingilia maongezi ya wakubwa zako, sio kima chako, kitakachotokea ni kujidanganya kuwa anajifunza dunia wakati unamwingiza kwenye ulimwengu asioufikia bado. Ni kumvusha kwenye rika lake na kumwingiza kwenye rika lisilomhusu, na hivyo akiingia huko atakuwa mbaya kwa sababu hajui miiko na mipaka yake.
  • 2. Kutofuatilia Maisha yake
  • Wakati sahihi wa kijana kukoma kutendewa kama mtoto ni pale ama atakapoolewa, ama atakapooa. Lakini kutokana na Maisha ya kisasa, niseme tu hata pale atakapojitegemea na kuwa na Maisha yakemwenyewe. Lakini katika kipindi chote atakachoishi kwa wazazi, huyu atatendewa kama mtoto, atawekewa taratibu famiia kama wengine tu. Siku hizi haya hayapo, unakuta kijana anatoka na Rafiki zake kwenda matembezi, mzazi wala hahitaji kujua anakwenda wapi, kufanya nini hasa, atakuwa na marafiki wa aina gani!! Kuna jambo ambalo laweza kuonekana ni kituko hii leo, zamani wazazi walishiriki kutuchagulia marafiki. Naam ndivyo ilivokuwa, mzazi anaweza kukuambia sitaki kabisa nikuone na fulana ama Watoto wa familia Fulani. Hata kama alikuwa Rafiki yako chanda na pete, mara moja urafiki huo ulikufa. Wazazi waliangalia tabia za Rafiki za mtoto wao na pia familia wanazotoka kama zina maadili. Leo hii mambo haya yamepuuzwa na wazazi hatuna muda tena. Tunawanyima Watoto wetu msingi wa kutambua marafiki wabaya na wazuri, tunaathiri Maisha yao ya baadaye kwa kutowajengea msingi bora wa mahusiano.
  • 3. Kumlea kihuni / kikahaba
  • Unakuta kijana anavaa kihuni mbele ya wazazi, ananing’iniza kitambaa mfuko wa nyuma, anajifunga kichwani kama TUPAC, anavaa suruali imemshuka kiasi boxer inaonekana mpaka mferijini, anavaa suruali imechanwachanwa mapajani, anavaa herein, amechora tattoo n.k. Haya ni malezi mabovu kabisa ambayo jamii imeruhusu, wewe mzazi simama na mwanao wala usilaumu teknolojia. Mtoto ana nafasi kubwa ya kumsikiliza mzazi kuliko watu wa mitaani, chora mpaka ambao hatakiwi kuuvuka na umaanishe, naye atatii tu kwa sababu wewe ndiye unayejua kula yake. KIjana anakuja amekuwekea relaxer, au ame-bleach sehemu ya nywele zake, ametoga masikio anakuvalia herein, amevaa pete na mikufu inamfika kiunoni, unaanzaje kumvumilia?

  • Upande wa mabinti ni vita kwa sababu wanawake wa jamii forums hawako tayari kuusikia ukweli, ila nitasema tu. Ni aibu kubwa mtoto wa kike kuanza kujipamba kikahaba mbele yako mzazi. Binti anavaa mavazi ambayo yalipaswa kumfanya hata baba yake mwenyewe ajifungie chumbani kuepuka kuona tupu ya mwanaye. Binti anaanzaje kuweka kalikiti, kuvaa vimodo, kuweka rasta, kujichubua Ngozi n.k. mbele yako mzazi? Binti akiwa bado mikononi mwa wazazi wake anajipodoa utadhani jini, anaaga wazazi wake kuwa anatoka matembezi na Rafiki zake. Siku za nyuma wazazi wangehoji, “unamvalia nani hivyo? Kwa nini umejipamba hivyo, kwaani unakwenda kukutana nan ani?” Safari ingekufa hapo hapo bila mjadala wowote, lakini siku hizi mabinti wanauliza mama zao, “nimependeza?” Na mama anatoa maoni jinsi ya kuboresha Zaidi mwonekano, bila kujali kuwa anamsogeza binti yake kwenye kinywa cha mamba na anamwandalia mazoea ya kuvaa hovyo.

  • 4. Kuruhusu lugha za kihuni
  • Wazazi wengine hawajali kabisa lugha anazotumia mtoto. Yaani mtoto anaweza kuongea lugha za matusi, maneno ya kihuni n.k. wala hawaoni hatari iliyo mbele. Lugha za hovyo ni dalili wazi kuwa mtoto ana marafiki wabaya na ameanza kuiga tabia zisizofaa. Jukumu ni lako mzazi kupinga kwa nguvu zote matumizi ya lugha hizi zisizofaa.

  • 5. Kumkabidhi alelewe na House Girl
  • Familia nyingi za kisasa zimeanguka kwenye mtego huu. Wanawake wameyaasi majukumu yao na kukimbilia majukumu ambayo kiasili ni ya waume zao. Mpangilio huu mpya wa familia umeacha pengo kubwa kwenye malezi ya Watoto. Leo hii ni aibu kwa mwanamke kuwa mama wa nyumbani kiasi kwamba hata mume anaweza asijisikie vizuri kwa sababu hiyo. Malezi ya Watoto, mume, shughuli za nyumbani ikiwamo manjonjo ya mapishi, usafi wa nguo zikiwamo za mume, limegeuka jukumu la house girl n.k.

  • Kwa mwenendo huu Watoto wamekuwa wakifuata maongozi ya wasichana wa kazi Zaidi kuliko wazazi wanaokutana nao maasaa machache sana ndani ya wiki. Uhuru kwa Watoto umekuwa mkubwa mno kwa sababu hakuna wa kuwasimamia katika kipindi hiki cha hatari ambapo wanatamani kujaribu kila kitu. Zamani wafanyakazi wa ndani waliitwa yaya, hawa walikuwa watu wazima ambao wengi wao ni wajane. Walikuwa wanaelewa maana ya malezi ya Watoto, maadili mem ani nini lakini pia walikuwa wasaidizi wa mke. Muda mwingi walikuwa eneo la nyumbani pamoja yaya akisaidia kazi mbalimbali kama anavyoelekezwa. Mtoto hakuwa na sauti mbele ya yaya, kama ilivyo kwa wazazi.

  • Baadaye zikaibuka shutuma za mayaya kufanya uchawi na kjaribu kudhuru familia. Upepo ghafla ukahamia kwa vibinti vidogo. Kwanza ilianza kwa Watoto wa ndugu walioko vijijini, kuwaomba waje mjini wasome, lakini wakaishia kuwa wafanyakazi wa ndani, kisha ikawa ni kutafuta mabinti waliofeli darasa la saba na hawana mwelekeo. Hawa ndio wakawa mbadala wa mayaya na hata malipo yao yakawa ni sawa na bure.

  • House girl akasimama kama mbadala wa mke wa ndoa, kwenye majukumu karibia yote ya nyumbani, isipokuwa ngono. Jukumu muhimu kabisa katika ndoa, malezi ya Watoto akakabidhiwa mtoto aliyefeli shule na Maisha ili amfunze misingi ya Maisha mtoto mwenzake, What a joke! Labda niseme neno moja kabla sijashambuliwa humu, wazazi kumtoa binti yao akafanye kazi za ndani ni dalili kwamba ama wao wamekosa mbinu za kukabili Maisha hivyo kumtoa binti kwa matumaini ya kupata ujira, ama tabia ya binti yao imewashinda wakaona ni heri aende kuishi mbali nao kwani hawawezi tena kumbadili. Sasaasilimia kubwa ya mabinti hawa wanaangukia kundi la pili, wameshindikana kwa wazazi. Ndio maana Zaidi ya 80% ya vibinti hivi vitakuwa tayari kufanya ngono na baba mwenye nyumba almradi ametaka mwenyewe. Huwa hakuna kesi za kubikiri, ni kesi za kutembea na baba mwenye nyumba. Ni aina ya wasichana walioharibika tayari.

  • Sasa iweje umkabidhi msichana wa aina hii aendeshe mji? Tunathamini kukusanya mali kuliko kuangalia future za Watoto wetu kwa kisingizio cha hali ngumu. Vibinti vingine vimefikia hatua kuwafundisha ngono Watoto wadogo n.k.

  • 5. Kutomfundisha majukumu ya nyumbani
  • Kwa sababu tu wazazi wameajiri house girl, mtoto hapati nafasi ya kujifunza mambo madogo madogo ya kawaida kama kufua nguo, kufagia nyumba, kupika n.k. Kazi yam toto ni kubadili channel za tv na kuweka video tu. Unakuta toto nalo limegeuka ni bosi wa nyumba!! Wazazi muelewe, ndani ya nyumba kuna mume kwanza halafu mke, basi. Mtoto atakuwa boss kwenye mji wake, hana haki ya kukohoa ndani ya mji wa mtu mwingine. Mtoto atafanya kazi KAMA house girl pale anapokuwa na nafasi, amsaidie majukumu YOTE bila kuchagua , huo ndio utaratibu. Mama amwongezee majuku mengine ambayo anadhani ni mafunzo ya kumjenga mwanaye ili kumwandaa kwa siku za usoni. Katoka tumboni, hana anachokijua, kutomfundisha ni kumfundisha kuwa shighuli za nyumbani ni za hadhi ya house girl, ndio maana mabinti wengi sana siku hizi wanaingia kwenye ndoa hawamuda mahitaji ya msingi kabisa (basics) ya ndoa kama, kufua. Kupika n.k.

  • 6. Upendo wa kijinga kwa mtoto
  • Wako wazazi wanaodhani kuwa kumdekeza mtoto ni upendo na kuonyesha unamjali. Tabia hii imewaumiza Watoto wengi sana na kuharibu Maisha yao.

  • Wako wazazi wanawadekeza Watoto wao kiasi cha kuwanunulia simu za miknoni, kuwawekea TV chumbani n.k. Mtoto unamnunulia simu ili awasiliane na nani? Kama ni marafiki zake huoni kuwa ni vema Zaidi akanukuu namba kisha akaja komba simu kwako ili uweze kumfuatilia? Kwa nini mtoto anayekutegemea kwa kila kitu awe na mawasiliano yake? Tena simu za smart ndizo zinazonunuliwa, ili waweze kujiunga kwenye mitandao ya kijamii. Habari ya group la tuition ni habari za kijinga kabisa, ni sawa na kumtoa mwanao afundishwe na ulimwengu.

  • Kwa wanaofuatilia, mambo yanayoendlea kwenye TV yanachangia kwa kiasi kikubwa kumomonyoa maadili. Ukimwekea mtoto TV chumbani mwake utakosa udhibiti wa vipindi anavyofuatilia, pia utashindwa kumjua mwelekeo wake. Unampa uhuru wa kuivinjari dunia anavyotaka.

  • 7. Kumtetea pale anapowakosea wengine.
  • Watoto wenzake wnapokuletea mashitaka kuwa mwanao amefanya jambo Fulani, unawakalipia na kumkingia kifua mwanao. Waalimu wakikuonya kuhusu tabia Fulani ya mwanao unakuja juu. Huku ni kumchimbia kaburi mwanao kwani ataendelea kufanya hivyo akijua yuko baba au mama atanitetea. Tuhuma zinapoletwa dhidi ya mwanao kwa Ushahidi wa Watoto wengi fahamu kuwa ni kweli n ani heri kumuadibisha mtoto ili ajue kuwa hulei ujinga. Mtu mzima ama mlezi akikuletea tuhuma Fulani huhitaji kutafuta Ushahidi mwingine kwani kupishana rika kwa mtu huyo na mwanao hakuwezi kumfanya awe na kinyongo chochote dhidi yake. Hiyo ni hatua ya mtu mwenye mtazamo wamalezi mema.

  • 8. Kumwonyesha MICHEPIKO yako
  • Huu ni upumbavu uliopitiliza. Wako wazazi ambao wanakuwa karibu na Watoto mpaka kuwageuza wasiri wao. Yaani binti anawajua wanaume wanaomlala mama yake mbali na baba yake na kijana anajua michepuko ya baba yake. Tena wengine wanafikia hatua ya kuwaambia baba yako huyu, ama mama yako huyu ila usimwambie baba yako ama mama yako. Huku ni kufungua lango la ngono kwa mwanao, ni kozi tosha ya kuwa Malaya au kahaba n ani rahisi Zaidi kufuzu.

  • 9. Kwenda naye sehemu za starehe
  • Unapomzoeza mwanao kwenda “viwanja” ni kumjengea tabia hiyo ambayo itakuja kuwa ngumu kuiacha. Ukimjengea mwanao tabia ya kwenda naye baa kulewa ni kumfundisha Maisha ambayo atayafuata kwa uaminifu.

  • 10. Kuwalaani Watoto bila kujua
  • Hapo zamani tulifundishwa kuwa mzazi wako akitaka kukulaani basi atakuonyesha utupu wake. Tendo hili liliogopwa mno na Watoto wote nyakati hizo, lakini leo hii hofu hiyo haipo tena. Watoto wanaishi chini ya laana ya wazazi bila kujua. Unakuta mzazi anatoka mbele ya Watoto amevaa kimini mpasuo mapaja yote yako nje. Akikaa kwenye kochi basi mpasi kijisehemu cha chupi kinaonekana (kama alibahatika kuvaa) vinginevyo kinena kinakuwa wazi.Watoto wakike kwa wale wa kiume wanajua kila siku leo mama kavaa chupi ya rangi Fulani, au mama kanyoa mavuzi. Hii ni kuwalaani Watoto wasio na hatia!! Niliwahi kwenda mahali Fulani kwa Rafiki yangu, tukiwa tumeketi sebuleni mkewe akaja kunisalimu na kuketi kwenye mkeka akinyonyesha mtoto. Mwanaye wa kiume tulikuwa tumeketi naye kwenye kochi. Baada ya muda alitaka kuinuka, kwa sababu alivaa sketi fupi huku amejitanda kanga juu kuficha nyonyo, alipokuwa akiinuka akachanua mapaja na hakuwa amevaa chupi. Haraka nilijaribu kuangalia upande lakini pia nilijuta sana kumtazama wakati akiinuka. Sasa nikajiuliza mwanaye ambaye alikuwa akimtazama kakiona kishimo cha manyoya? Je, haya ndiyo maisha yake ya kila siku? Tuseme tu ukweli, wamamamnaovaa nusu uchi mnakuwa mnawalaani Watoto wenu wenyewe.

  • 11. Kuishi na mtoto aliyeharibika akili
  • Katika Makala zilizopita niliwahi kuzungumzia kijana aliyeharibika akili. Kwa kifupi hawani wale wanaovaa kihuni au kikahaba, wanatoga masikio, wanachora tattoo, wamenyoa kama vichaa, wamebleach nywele, wanajichubua Ngozi n.k. Kama uan mtoto wa kike au wa kiume wa aina hii, kuendelea kuishi naye ni kubariki wadogo zake wafuate Maisha hayo. Watoto hujifunza Zaidi mabaya kuliko mazuri, kama ilivyokwa sisi watu wazima ambapo hufurahia Zaidi Maisha ya dhambi kuliko kufuata maagizo ya Mungu. Watoto wana nafasi kubwa ya kumfuata mkubwa wao kwani itaonekna kuwa ni jambo la kawaida kama wazazi wao watalivumilia. Usiruhusu kuishi na mtoto wa namna hii ndani mwako, ndivyo ilivyokuwa tangu kale.

  • Bahati mbaya kwenye kundi hili wanaingia hata mabinti wanaozalia nje ya ndoa, huyu ameshakuwa mtu mzima, keshajua siri zote za Maisha, sim toto tena. Huna cha kumfunza kama mzazi, Zaidi atapanda mbegu mbaya kwa wadogo zake, labda kama amebakwa, ama umri wake ni mdogo mno, kitu ambacho unapaswa wewe kama mzazi ujiulize ulikuwa wapi usichukue hatua mapema? Ukiruhusu hali hii, mara nyingi mabinti wengi watakaofuatia watazalia nyumbani pia.

  • 12. Umbea na usengenaji
  • Mama unakaa na binti yako kuwasengenya wanawake wenzako. Mnapiga soga kutwa kuchwa utadhani ni genge la makahaba, hujui kwamba ndio unamjenga mwanao kuwa na tabia hizo. Mtoto hapaswi kujua maongezi ya wakubwa, yeye ana sehemu yake tu ambayo ni mafundisho kwake. Tena unakuta mtoto anakuja kusimulia umbea kwa wazazi na wao wanacheka na kuanza kumponda anayesengenywa.

  • 13. Kumfanya chanzo cha kipato
  • Mtoto anakuwa analeta pesa na zawadi mbalimbali wakati hana kazi anayoifanya kumuingizia kipato, wazazi nao wanabariki. Hii ni kumtoa mtoto ama awe kahaba, ama awe mhuni anayehifadhiwa na mashangingi ya mjini. Mtoto anakuzwa kabla ya wakati na future yake anaharibika.
  • 14. Kubariki boyfriend ama girlfriend
Mtoto analeta boyfriend ama girlfriend nyumbani kwa wazazi. Wazazi kwa sababu ni wa kisasa wanaona ni kawaida tu, wanabariki mtoto wao kufanya ngono. Hii ni hatari, vijana ambao hawajawa na mbele wa nyuma unawakabidhi vipi mwanao wamchezee? Mzazi umepaswa kubariki kijana anayekuja kutaka uchumba, afuate taratibu zote na si nje ya hapo. Kina kaka wawalinde dada zao dhidi ya huu ubaradhuli wa kimagharibi, kwani ni jukumu lao halali kabisa. Siku hizi hakuna jema, wakubwa kwa wadogo wamekumbwa na pepo la ngono, hivyo HAKUNA mahusiano katika ya mvulana na msichana, lazima wataishia kitandani tu.

Yako mengi mno ambayo yanaweza kuandikwa, lakini niombe tu, ewe mzazi chukua hatua. Mlinde mwanao dhidi ya uchafu uliotapakaa duniani kwa sasa, amini kuwa inawezekana na itakuwa.

Mkuu umesahau wakina mama kukaa na watoto wao wa kiume jikoni. Wakati enzi zetu ukikaa jikoni unaweza kula stick [/QUOTE
 
Mambo ya msingi sana haya, siku izi tuko bize sana kuweka ukuta imara kwenye msingi mbovu, huku tukisindikizwa na kale kamsemo ketu....
"Sitaki mwanangu apite nilipopita"
Kumbe ndo tunaharibu wanetu.

Maandiko yanasisitiza kumlea mtoto katika njia impasayo na yeye hatoiacha hata atakapokua mzee.

Wazazi tujitathmini sana kuhusu malezi ya wanetu na Mungu atusaisie.
 
Uko sahihi sana umenikwaza sana kumtaja tupac kwenye number tatu hili nitaliletea uzi wake
 
Uko sahihi sana umenikwaza sana kumtaja tupac kwenye number tatu hili nitaliletea uzi wake
Tupac alikuwa msema kweli na ndicho kilichogharimu maisha yake. Mimi nimefanya rejea tu ya staili yake ya ufungaji kitambaa kichwani mkuu, kwetu huku ni ishara ya usela. Sorry kama nimekukwaza
 
Mkuu umesahau wakina mama kukaa na watoto wao wa kiume jikoni. Wakati enzi zetu ukikaa jikoni unaweza kula stick
 
Wazazi wengi tunawaogopa sana watoto wetu. Tunaamini tukiwakemea na kuwaadhibu tutawajengea kutokujiamini, kumbe ndio tunayathibitisha maovu yao.
Tunaunda bomu litakalotulipukia. Infact limeshaanza kutulipukia.
 
Back
Top Bottom