Dah swanga, ntarudi tena mungu akipenda, nikiona picha hizo inanikumbusha mbali sana, pale town maeneo km Katandala, jangwani, izia, chanji, bangwe, sumbawanga wenyeji kule, kizwite, mazwi, hahahaha nchi hii bana nzuri sana ila wana MTANDAO wanaiharibu sana.Kule ukilima mahindi yakifika steji ya mahindi mabichi yale mabua yake yanaliwa kama miwa wanaita MIGAGI. utakuta mtu kaenda shamba kakata fungu kubwa eti anapeleka home kula na watoto hahahaha.Nakumbuka enzi za Mwalimu kulikuwa na Tajiri mmoja anaitwa Bhojak mitaa ya jangwani pale, Kulikuwa na singa singa flani maridadi sana na engineering company yake ya kujenga majengo akiitwa Bainz, pale mpango kabambe wa maji kulikuwa na kota za wazungu nadhahi ni wa denish au swedish wale walikuwa wana kauwanja kao ka tennis basi tunapita pale kuokota mipira ya ile ya long tennis inayotoka nje ya fence. Nilikuwa naishi maeneo ya regional Block kule basi hawa wazungu walikuwa kila jioni lazima wafanye jogging kuelekea king'ombe na kurudi. Nawakumbuka sana mzee Mzindakaya na Paul kimiti hawa wazee ni wa long time mno. DAH One day Ntarudi nawakumbuka sana friendz wangu wa school pale jangwani miaka hiyoo