Nyumba za watoto yatima Dar es Salaam?

Kingdom_man

JF-Expert Member
May 19, 2010
405
500
Habari wana jamvi.
Naulizia Orphanage centres hapa Dar za ukweli ambazo zinasaidia watoto yatima ni zipi na zipo wapi kwa hapa Dar.

Asanteni.

Yakobo 1:27"Dini iliyo safi, isiyo na uchafu mbele za Mungu Baba, ndio hii:
kuwasaidia YATIMA na wajane katika dhiki zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu."
 
Asa'rile

JF-Expert Member
Jun 29, 2012
438
195
kuna moja ipo maeneo ya Mwenge nyuma ya Kakobe, waweza ulizia pale namna ya kufika , sio mbali.
Aidha Mkuu, watoto yatima wengine tunao humu mitaani/ majumbani. waweza tu kuwatembelea na ukafanya hiyo Ibada njema sana, kupita ibada za makanisani
 
Asante sana Mdau.
Naona bora watoto yatima wa vituo rasmi, hawa wa mitaani wengine ni waongo.
 
kindafu

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
1,325
2,000
Habari wana jamvi.
Naulizia Orphanage centres hapa Dar za ukweli ambazo zinasaidia watoto yatima ni zipi na zipo wapi kwa hapa Dar.

Asanteni.

Yakobo 1:27"Dini iliyo safi, isiyo na uchafu mbele za Mungu Baba, ndio hii:
kuwasaidia YATIMA na wajane katika dhiki zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu."

Mkuu Kingdom_man nakupongeza kwa kusudio lako zuri la kufanya hiyo "Ibada" ila nikutahadharishe uwe makini kwani baadhi ya vituo ni "Biashara" za watu! Nakushauri ukishatambua vituo vitakavyokidhi vigezo vyako, jipe muda utembelee vituo husika uzungumze na watoto husika, walezi wao na pia uongozi ili kubaini maeneo halisi ambako hiyo "Sadaka/Ibada" yako inaweza kuboresha maisha zaidi kwa walengwa! Hilo ni bora zaidi kuliko kupeleka tu "mbuzi na mchele wa Sikukuu"!
 
Hilo nalo neno.
Sawa kiongozi nitalizingatia hilo.
Asante sana
 
BAOBAO

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
1,874
1,250
Nawasihi pia, mtembelee kama mimi,kituo cha kulea watoto wenye HIV+; kinachoitwa KIJIJI CHA MATUMAINI,pale mjini Dodoma.
 
Da Asia

JF-Expert Member
Sep 25, 2011
731
1,000
Mkono wa kulia ukitoa wa kushoto usijue na wa kushoto ukitoa wa kulia usijue. Ndivyo sadaka inavyotaka. Ungeuliza tu vituo vya watoto yatima vilipo ungeelekezwa bila kutangaza nia yako. All in all Mwenge Opharnage Centre mbele kidogo ya meeda unakata kulia kama umetokea meeda. Kingine kiko mtogole, barabara kubwa iendayo sinza kabla hujafika kwenye junction ya kuingia knyama kushoto kwako from magomeni utaona kibao cha yatima. Nimesahau jina. Mbweni pia kuna kituo kikubwa jina linenitoka lakini ukipita njia ya shule ya mhe komba, bakili muluzi, mbele kule utaelekezwa. Kila la kheri.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Aisee. sasa dada mimi niliposema nataka kwenda kutoa msaada ni wapi? quote me please!!
Duh saa zingine bora kukaa kimya tu!
Thanks anyways

Proverbs 18:2
"A fool takes no pleasure in understanding, but only in expressing his/her opinion."
 
mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
10,749
2,000
SOS Village kipo njia panda ya Sam Nujoma na njia iingiayo Stand mpya ya daladala ya kituocha Ubungo,hupeleka hadi nje kusomesha watoto yatima,lakini sasa hawapokei watoto kama lengolako lilikuwa hilo basi usihangaike.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom