Mohamed Said JF-Expert Member Joined Nov 2, 2008 Posts 23,285 Reaction score 33,882 Feb 11, 2023 #1 NYUMBA ZILIZOKUWAKO DAR ES SALAAM YA 1950s Hapo chini ni mfano wa nyumba nyingi zilizokuwapo Dar-es-Salaam miaka ya 1950. Nyumba hizi zilikuwa na vyumba sita vyumba vitatu kila upande vikiangaliana na katikati kulikuwa na ukumbi mrefu. Uani kulikuwa na mabanda madogo jiko, vyoo na bafu. Nyumba nyingi zilikuwa na karo ambalo lilitumika kama mahali pa kuoshea vyombo au kufua nguo. Nyingi ya nyumba hizi zilikuwa za kupangisha kwa hiyo utakuta nyumba moja ikikaliwa na familia tofauti. Baadhi ya nyumba zilikuwa na baraza mbele kwa ajili ya wakazi kukaa na kupumzika hasa wanaume mfano wa hiyo nyumba picha ya pili. Wanawake kwa kawaida wao wakipumzika uani au ukumbini. Nyumba hizi zimetoweka Kariakoo lakini nimebahatika kuziona nyumba hizi Magomeni Mapipa.
NYUMBA ZILIZOKUWAKO DAR ES SALAAM YA 1950s Hapo chini ni mfano wa nyumba nyingi zilizokuwapo Dar-es-Salaam miaka ya 1950. Nyumba hizi zilikuwa na vyumba sita vyumba vitatu kila upande vikiangaliana na katikati kulikuwa na ukumbi mrefu. Uani kulikuwa na mabanda madogo jiko, vyoo na bafu. Nyumba nyingi zilikuwa na karo ambalo lilitumika kama mahali pa kuoshea vyombo au kufua nguo. Nyingi ya nyumba hizi zilikuwa za kupangisha kwa hiyo utakuta nyumba moja ikikaliwa na familia tofauti. Baadhi ya nyumba zilikuwa na baraza mbele kwa ajili ya wakazi kukaa na kupumzika hasa wanaume mfano wa hiyo nyumba picha ya pili. Wanawake kwa kawaida wao wakipumzika uani au ukumbini. Nyumba hizi zimetoweka Kariakoo lakini nimebahatika kuziona nyumba hizi Magomeni Mapipa.
King Kong III Platinum Member Joined Oct 15, 2010 Posts 62,903 Reaction score 95,238 Feb 11, 2023 #2 Ni kweli kabisa ,kulikuwa na karo la kuoshea vyombo na kufulia kwenye nyumba nyingi za kizamani ,pia zilikuwa za udongo kisha wanapiga plasta ya cement halafu bati zilikuwa asbestos.
Ni kweli kabisa ,kulikuwa na karo la kuoshea vyombo na kufulia kwenye nyumba nyingi za kizamani ,pia zilikuwa za udongo kisha wanapiga plasta ya cement halafu bati zilikuwa asbestos.
M mmteule JF-Expert Member Joined Oct 3, 2011 Posts 6,035 Reaction score 15,071 Feb 11, 2023 #3 Wazee wa Zamani hawakuzingatia Parking. Wao Kiwanja waliziba mbele chooote ndio wanakaa wao uani wanaweka Mabanda ya Wapangaji. Hapo Magomeni Mapipa waliezeka kwa kutumia Mabati ya mapipa yaliyokuwa tupu baada ya lami kutumika toka KAJIMA aliyeweka lami maeneo hayo. All in all nyumba za Udongo zinadumu sana kuliko hizi tofali 50 kwa mfuko wa Cement
Wazee wa Zamani hawakuzingatia Parking. Wao Kiwanja waliziba mbele chooote ndio wanakaa wao uani wanaweka Mabanda ya Wapangaji. Hapo Magomeni Mapipa waliezeka kwa kutumia Mabati ya mapipa yaliyokuwa tupu baada ya lami kutumika toka KAJIMA aliyeweka lami maeneo hayo. All in all nyumba za Udongo zinadumu sana kuliko hizi tofali 50 kwa mfuko wa Cement
Watu8 Platinum Member Joined Feb 19, 2010 Posts 76,816 Reaction score 110,069 Feb 11, 2023 #4 Tanga mjini napo kungalu na nyumba kama hizi...
Kobello JF-Expert Member Joined Feb 20, 2011 Posts 9,277 Reaction score 9,020 Feb 11, 2023 #5 Zipo sana Temeke. Wafanyakazi wengi wa viwandani na serikali (ngazi za chini) tangu enzi za mkoloni waliishi mitaa hiyo.
Zipo sana Temeke. Wafanyakazi wengi wa viwandani na serikali (ngazi za chini) tangu enzi za mkoloni waliishi mitaa hiyo.
Dormant Account JF-Expert Member Joined Apr 5, 2022 Posts 11,307 Reaction score 32,796 Feb 11, 2023 #6 Aiseee kitambo
Satoh Hirosh JF-Expert Member Joined Mar 30, 2021 Posts 7,216 Reaction score 29,400 Feb 11, 2023 #7 Hizi nyumba bado zipo nyingi kwenye miji ya zamani kama Tandika (Temeke ),Magomeni,Mwananyamala na hata Faya/jangwani ( Kariakoo) bado zipo baadhi. Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Hizi nyumba bado zipo nyingi kwenye miji ya zamani kama Tandika (Temeke ),Magomeni,Mwananyamala na hata Faya/jangwani ( Kariakoo) bado zipo baadhi. Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Satoh Hirosh JF-Expert Member Joined Mar 30, 2021 Posts 7,216 Reaction score 29,400 Feb 11, 2023 #8 Pia mji wa Lindi hata leo ndiyo nyumba zilizojaa,mji umechoka Sana ule. Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Pia mji wa Lindi hata leo ndiyo nyumba zilizojaa,mji umechoka Sana ule. Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
sheiza JF-Expert Member Joined Sep 29, 2010 Posts 7,634 Reaction score 11,693 Feb 11, 2023 #9 Satoh Hirosh said: Pia mji wa Lindi hata leo ndiyo nyumba zilizojaa,mji umechoka Sana ule. Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app Click to expand... Nyumba za lindi mjini 90% zinafanana. Zina udongo na mawe.
Satoh Hirosh said: Pia mji wa Lindi hata leo ndiyo nyumba zilizojaa,mji umechoka Sana ule. Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app Click to expand... Nyumba za lindi mjini 90% zinafanana. Zina udongo na mawe.
Satoh Hirosh JF-Expert Member Joined Mar 30, 2021 Posts 7,216 Reaction score 29,400 Feb 13, 2023 #10 sheiza said: Nyumba za lindi mjini 90% zinafanana. Zina udongo na mawe. Click to expand... Mji usioendelea,utadhani umepigwa mute na remote control.
sheiza said: Nyumba za lindi mjini 90% zinafanana. Zina udongo na mawe. Click to expand... Mji usioendelea,utadhani umepigwa mute na remote control.