Nyumba ya Mh. Mariam Kassembe sh. 400mil

Nyumba ya Mh. Mariam Kassembe sh. 400mil

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,252
Reaction score
16,171
Katika sakata la vurugu za bodaboda dhidi ya polisi (tigo) kule Masasi watu wameshuhudia vurugu zikibadilisha mwelekeo kutoka kwa polisi hadi viongozi wa CCM na serikali yake Wilayani Masasi kulikopelekea nyumba na majengo yanayomilikiwa na baadhi ya wabunge wa CCM na ofisi za chama cha CCM chenyewe kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kutokana na sababu mbalimbali. Miongoni mwa nyumba zilizochomwa moto ni pamoja na za wah. Mariam Kassembe na Ana Abdallah.

"... ndugu mtangazaji, ukiondoa samani za ndani ambazo zote zimeungua, yumba yangu ilikuwa na thamani ya sh. 400mil"
alisikika akisema Mh. Mariam Kasembe wakati akihojiwa na mtangazaji wa kipindi cha patapata cha WAPO redio. Kassembe alivitaja vitu vingine vilivyoharibiwa ni pamoja na matrekta 2, gari na mifugo. " .... kama wewe (mtangazaji) ulivyo huna kitu hata mimi nimebaki sina kitu chochote sasa" aliongeza kusema Mh. Kassembe. Mh. Kasembe anaonekana na yeye hajui kwanini nyumba yake imelengwa pia katika vurugu hizi.

Maswali niliyokuwa najiuliza kuhusu Mh. Kasembe ni kwamba:

1.Wakati yeye akimiliki nyumba hiyo ya 400milioni, matrekta 2 na gari amewafanyia nini vijana (waliochoma nyumba yake) wa Masasi na majirani zake wanaomzunguuza katika kuwaondolea kero zao mabalimbali?

2. Wakati mikoa ya kusini ikilalamikia kutelekezwa na serikali kiuchumi viongozi wao mnamiliki mali kubwa katikati ya watu maskini, hii ni haki? mbona Nyerere hakufanya hivyo kule kwake Mara, Butiama na Msasani?

3. Ina maana kasembe hafahamu kwamba mikoa ya kusini iko nyuma kimaendeleo ikiwa chini ya Serikali inayoongozwa na chama chake tangu tupate uhuru?

4. Ina maana Kassembe hajui kama polisi ni chombo cha dola inayoongozwa na chama chake?

5. Ina maana Kassembe anashindwa kuona uhusiano uliopo kati ya waendesha bodaboda nchini, rushwa ya polisi, umaskini, serikali, wabunge wa chama tawala na chama tawala?

Nadhani tutakujashudia watumishi wetu siku zijazo wakitendewa vitendo vibaya zaidi kama kubakwa n.k na vijana wetu ambao wako irritable kwa kila jambo. Hawaoni nafuu yoyote wala hope ya maisha yao. Hata hizi bodaboda wanazoendesha huwa zinawaletea matatizo makubwa kiafya (fractures, vifua kuuma, kutekwa) huku wakikimbizana kupata kodi za matajiri wao, TRA, matumizi yao na rushwa za polisi barabarani. Iko siku waendesha bodaboda kote nchini watakuja kuungana dhidi ya jambo fulani!!!!!!
 
Yeye wacha alie lie na kuwalingishia thamani ya nyumba kitakachofuata watamchoma moto yeye.
 
wakati wazazi wake wakimsisitiza elimu dunia na akhera ,hao wengine ni akhera tu sasa hivi matunda ya elimu yake yanaonekana japo ya kuunga unga wanachoma moto hahahaahah
 
Wacha na yeye afeel pain kama tunayofeel maskin ambao hatuna nyumba bora za kuishi labda atajifunza ki2l

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Tuchambue mambo kwa makini. Hivi ni ajabu mbunge kumiliki nyumba ya mil400? Mshahara wake kwa miaka mitano ni mil420 na bado wanachukua mikopo. Kwa hiyo kuwa na vitu hivyo si ajabu. Bodaboda wajue adui yao ni nani, si mbunge wala nyumba wala matrekta ni mfumo. Tupigane kuondoa mfumo si kuharibu mali.
 
Ndo wachome? Sababu ya bei tu?

Ninachokiona hapo ni chuki ya wananchi juu ya baadhi ya wana siasa. Haiwezekani upigane na polisi halafu ukachome nyumba ya mheshimiwa fulani.
Ina maana wananchi hawako pamoja na wana siasa katika mitazamo ya maisha ya kila siku.
 
Sio sahihi kupora, kuharibu mali au kuchoma nyumba ya mtu mwingine yeyote bila kujali sababu zinazokusukuma kufanya hivyo. Huu ni utamaduni mpya unaojenga mwelekeo mbaya sana kwa taifa kwani leo limetokea kwa wabunge kesho linaweza kutokea kwa mtu mwingine yeyote kati yetu. Pole sana kwa wabunge na viongozi wengine waliochomewa nyumba na kuharibiwa mali zao nyingine.
 
Dawa ya watu wa mtwara inakuja too soon...
 
Hakuna kitu kibaya kama umaskini

Ni bora umaskini wa mali kuliko akili, angalia tu kwenye mirathi, kinyumba kimoja kinasababisha ukoo uuane.


MAskini tuna roho mbaya sana
Ninachokiona hapo ni chuki ya wananchi juu ya baadhi ya wana siasa. Haiwezekani upigane na polisi halafu ukachome nyumba ya mheshimiwa fulani.
Ina maana wananchi hawako pamoja na wana siasa katika mitazamo ya maisha ya kila siku.
 
Thamani za nyumba zetu sinema tupu!..........milioni 400? Masasi?

VURUGU+MTWARA+NA+MASASI+%25281%2529.jpg
 
Nyumba ya Tzs Mill 400.Siwezi kuwalaumu vijana pengo la walionacho na wasionacho ni kubwa,na hii itaendelea labda serikali ibadili muelekeo wa maisha yake.
 
" .... kama wewe (mtangazaji) ulivyo huna kitu hata mimi nimebaki sina kitu chochote sasa" aliongeza kusema Mh. Kassembe... Mwiso wa kunukuu..

.
Kumbe anajua kabisa watu walio nje ya system hawana kitu eeh? Sasa umefika wakati wale wenye nacho hawana amani ya kukila.
Kuna wakati kwa kila jambo, wakati wa kucheka na wakati wa kulia....
.
 
Ha ha ha hii ni zaidi ya over price,,, hata kama ni inflation hii ni kali..


Hivi anaijua million 400 ilivyo? Pesa lazima tuipe heshima yake.. Hiyo nyumba hata million 100 tu kufika kwa mbinde..

Nyumba za million 400 ni viota kweli kweli vimejaa mikocheni na mbezi beach sio hiyo nyumba ya vifaa vya kichina kutoka Good one, sunda etc kama inavoonekana hapo juu
 
Hakuna kitu kibaya kama umaskini

Ni bora umaskini wa mali kuliko akili, angalia tu kwenye mirathi, kinyumba kimoja kinasababisha ukoo uuane.


MAskini tuna roho mbaya sana

Umaskini janga la kitaifa...we acha tu. Badala ya kuhangaika na wanayoyaweza wamevamia kitu ambacho piga ua hawakiwezi ng'oo.
On the other hand, this is a business opportunity. kachukue jimbo Kongosho...Mbunge wao naona wamemchoka
 
Last edited by a moderator:
" .... kama wewe (mtangazaji) ulivyo huna kitu hata mimi nimebaki sina kitu chochote sasa" aliongeza kusema Mh. Kassembe... Mwiso wa kunukuu..

Nimepapenda sana hapa.....sijui katumia criteria gani kutambua kwamba mtangazaji hanakitu, bilashaka yawezekana wanauhusiano wa karibu sana au katumia kigezo cha kwamba watangazaji wengi hawana kitu! Nchi inavihoja hii!
 
Back
Top Bottom