Nyumba ya Mbunge Zitto Kabwe Mkoani Kigoma yaungua moto

Hiyo ndio Nyumba Ya Zitto Kabwe? Duuu Maisha ya wanachi wake yapoje sasa kama hiyo ndio Nyumba yake? Hela anapeleka wapi?

ama kweli MFICHA MARADHI KIFO HUMUUMBUA!
 
Hatari sana hii!!

Kile "kisomo cha jana" safari hii kitasingiziwa mengi kuliko tunavyomsingizia shetani.

Ukweli unaanza kujitokeza nyuma ya uhalifu huu siyo Serikali, kama ndivyo unavyotaka kutuelewesha. Serikali itakuwa na watu wajinga kufanya vitendo hivyo wakati ikinyooshewa vidole.
 
Tumepata ajali kidogo. Nyumba yangu ninayoishi katika eneo la Kibingo, mji mdogo wa Mwandiga, Kigoma imeteketea kwa moto jioni hii. Alhamdulillah, kuwa hakuna binaadam aliyeumia.

Nawashukuru Jeshi la Zimamoto, majirani zangu pamoja na wananchi wenzangu kwa ushirikiano walioutoa mpaka kuuzima moto husika. Kwa sasa Jeshi la Polisi wanafanyia kazi kujua chanzo cha ajali.

Naomba wananchi wawe watulivu wakati Polisi wanaendelea na uchunguzi husika.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama - ACT Wazalendo
Nairobi - Kenya
Septemba 16, 2017
 
Back
Top Bottom