Nyumba ya Mbunge Zitto Kabwe Mkoani Kigoma yaungua moto

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Nyumba ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) iliyopo Mwandiga, mkoani Kigoma yaungua moto. Bado chanzo hakijajulikana.
DJ2oz_FX0AAoJZ3.jpg
DJ2ozGAWkAEfO0N.jpg
DJ2oyMyXcAAhLTC.jpg


Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amezungumzia tukio la kuteketea moto nyumba yake jioni ya leo na kueleza kuwa licha ya moto huo kuunguza vitu mbalimbali, hakuna mtu yeyote aliyepata madhara.

“Tumepata ajali kidogo. Nyumba yangu ninayoishi katika eneo la Kibingo, mji mdogo wa Mwandiga, Kigoma imeteketea kwa moto jioni hii. Alhamdulillah, kuwa hakuna binaadam aliyeumia.”

Zitto Kanwe ambaye yupo jijini Nairobi amelishukuru Jeshi la Zima Moto kwa namna lilivyoshughulika na ajali hiyo. Mbali na Polisi, Zitto ametoa shukrani zake kwa majirani wake ambao kwa pamoja wamesaidia katika kuzima moto huo.

“Nawashukuru Jeshi la Zimamoto, majirani zangu pamoja na wananchi wenzangu kwa ushirikiano walioutoa mpaka kuuzima moto husika.”

Katika taarifa yake, Zitto amesema kwa sasa jeshi la polisi wanaendelea na uchunguzi kuweza kubaini chazo cha moto huo na hivyo ni vyem wananchi wakawa watulivu ili polisi wafanya kazi yao kwa utulivu.
 
Taarifa tulizozipokea muda huu ni kuwa nyumba ya Kiongozi wa Chama, Ndugu Zitto Kabwe ya Mwandiga, Kigoma imeungua moto muda huu.

Kamati ya ACT Amani inafuatilia jambo hili. Taarifa zaidi zitawajia punde.

Mohammed Babu
Mwenyekiti - Kamati ya ACT Amani (Ulinzi na Usalama)
 
Back
Top Bottom