Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,884
Ramani za ujenzi wa nyumba husumbua vichwa sana vichwa wengi wanapohaha kutafuta na kubuni ramani iweje. Na pengine tunaangukia kuchagua ramani ambayo umalizaji wa paa lake hutugharibu sana pesa. Nyumba kama hii ni very simple, low cost lakini ina mvuto.
Ramani hii inatoa fursa ya kuongeza vyumba kirahisi maana alternative ya kuendeleza upanuzi wa nyumba yako ni wazi na rahisi. Na hata mpango wa ujenzi kwa awamu una mshiko sana hapa.
Tunaweza kukwepa gharama kubwa za ujenzi wa nyumba kwa kutumia ramani ya mjengo wa kawaida ambao hautatugharamu sana pesa ila tu umaliziaji wake tu ukaweza kuwavunja shingo wapita njia wakaahau kama kofia walizovaa zimedondoka baada ya kufika mbali toka kwenye nyumba yako na kupata wageni wasiotarajiwa kuiba ramani na umaliziaji wako.