Nyumba ya gharama nafuu - Small , simple but beautiful

unasema gharama nafuu tupe gharama zake ni tsh ngapi hadi ikamilike na ina vyumba vingapi

Ukubwa wa nyumba au udogo wake si idadi ya vyumba, inategemea na plan yako. Hali kadhalika gharama ya ujezi wake hadi ikamilike si sawa na kwenda dukani kununua mchi wa sabuni, kuna mengi yanayofanya nyumba ijengwe kwa gharama nafuu au ghali, ni akili yako, ujuavyo akili ni nywele.
 
Kitu kimoja kinachoongeza gharama za ujenzi Tanzania ni utamaduni uliozoeleka na wa kulazimishwa kisheria kujenga jumba lenye uimara usio na lazima, ma nondo na ma zege na matofali mazito mazito na ma kokoto yasiyo lazima. Nchi za wenzetu wanajenga nyumba za mbao na hazibomoki, kwa nini?
 
Mwalimu si unajua kila mtu ana taste zake?

Asitulazimisha sote hizo taste zake kwa kumkashifu aliyejenga kuwa "alitaka sifa" wakati hata hamjui.

Hilo jengo limepigwa katika angle ambayo inalifanya lisionekane hata likoje vizuri, seuze kujua kuwa linavutia au la. Picha hiyo iliyoletwa inashindwa hata kuonyesha kuwa hilo jengo ni refu kuelekea ndani ya picha, na kuwafanya watu wafikiri ni plan nzuri kwa mtu mwenye kiwanja kidogo, wakati si kweli.

Watu waache kujaza wengine opinion zao kwa kutuletea vielelezo visivyo yakinifu
 
292455_2023742587376_1058331074_31809291_6172102_n.jpg

Ramani za ujenzi wa nyumba husumbua vichwa sana vichwa wengi wanapohaha kutafuta na kubuni ramani iweje. Na pengine tunaangukia kuchagua ramani ambayo umalizaji wa paa lake hutugharibu sana pesa. Nyumba kama hii ni very simple, low cost lakini ina mvuto.

Ramani hii inatoa fursa ya kuongeza vyumba kirahisi maana alternative ya kuendeleza upanuzi wa nyumba yako ni wazi na rahisi. Na hata mpango wa ujenzi kwa awamu una mshiko sana hapa.

Tunaweza kukwepa gharama kubwa za ujenzi wa nyumba kwa kutumia ramani ya mjengo wa kawaida ambao hautatugharamu sana pesa ila tu umaliziaji wake tu ukaweza kuwavunja shingo wapita njia wakaahau kama kofia walizovaa zimedondoka baada ya kufika mbali toka kwenye nyumba yako na kupata wageni wasiotarajiwa kuiba ramani na umaliziaji wako.

Ughali au unafuu wa nyumba unategemea vitu vingi (ramani ya nyumba yenyewe, wapi unajenga, aina gani ya materials unatumia kujenga, finishing ya aina gani unafanya, mafundi wa aina gani unatumia, idadi ya vyoo, vyumba n.k) sio tu "pictorial view" kama unavyotuonyesha. Hii nyumba bado ni ya gharama. La msingi tuwekee plan yake, ili tufanye tathmini.
 
Wapi ramani tuibe mchoro... Mie nampango wa kujenga ka ghorofa kamoja hii sijaipenda kiaina naona gharama zake haziwezi tofautiana kwa sana na mpango wangu
 
Kitu kimoja kinachoongeza gharama za ujenzi Tanzania ni utamaduni uliozoeleka na wa kulazimishwa kisheria kujenga jumba lenye uimara usio na lazima, ma nondo na ma zege na matofali mazito mazito na ma kokoto yasiyo lazima. Nchi za wenzetu wanajenga nyumba za mbao na hazibomoki, kwa nini?

Haya bora umetamka kitu muhimu sana. Kijijini niliamua kujenga kibanda cha wazee miaka michache iliyopita. Plan yangu ilikataliwa na wazazi wangu kwa maana kwamba waliona ni ghali mno na inaweza kusababisha nyumba isikamilike kwa wakati. Wakaja na wazo kwamba wao watasimamia zoezi la upatikanaji wa tofali za kuchoma kwa gharama nafuu kwa vile baba aliniambia mwenyewe ni mzoefu wa kufyatua matofali hayo na kuyochoma.

Alifanikisha zoezi hilo la tofali kwa ufanisi mkubwa na tofali zilifyatuliwa na kuchomwa tanuru eneo la kujengea nyumba ili kupunguza gharama za kusombelea matofali, bahati pale kulikuwa na udongo mzuri unaofaa kwa tofali za kujengea. Alisema bora kusombelea maji ya kufyatulia tofali kuliko kusombelea tofali ni ghali zaidi.

Nyumba haikujengewa kutumia saruji, bali matofali ya kuchomwa yalijengwa kwa udongo wa mfinyanzi kadiri ya uamuzi wa baba mzazi na niliheshimu kadiri ya ushauri na uzoefu wake na alinionyesha nyumba zilizojengwa kwa mtindo huo na zilionekana safi na zipo miaka mingi tu. Aliniusia kitu kimoja nisiwe mtumwa wa kitabu kwa kila kitu nitaingizwa mjini kwani kule ni kijijini, hivyo nisiwaletee mambo ya mjini yanayocost sana. Nilishtuka kidogo kwa kauli hiyo lakini niliona mzazi mpaka aniambie hivyo kuna kitu alinisoma na hivyo alijaribu kuniweka sawa.

Sikuingia gharama za kusimamisha kuta isipokuwa kumlipa fundi mjenzi wa huko huko kijijini anayejulia ujenzi wa aina hiyo. Ukweli niliokoa karibu nusu ya pesa niliyokusudia, kwani kuimarisha kuta za nyumba ni kuweka plasta ndani , nje tofali za kuchoma zinavyomeremeta ni pambo maridhawa.

Nashauri ujenzi ambao kwa sasasa tunaweza kuepa gharama ni kuta za ndani ambazo si lazima kutumia tofaili au blocks, na kazi hiyo ya kugawa vyumba inaweza fanyika wakati wo wote kadiri ya mahitaji, kwani cha msingi ni kuta za nje na paa lake.
 
OB-RS502_0210Ga_D_20120208161702.jpg
OB-RP935_0203So_D_20120201153414.jpg

Picha kushoto na kulia ni plan za nyumba mbili tofauti

Nyumba hii kwa mbali inatoa taswira nzuri ambayo mjengo wake very simple but looks very beautiful. Kuna majengo yanaonekana makubwa kwa nje umbo na mwonekano wake huku yakigharimu pesa nyingi, ambapo jambo la msingi idadi ya vyumba ni kama ya nyumba hii ambayo inaonekana simpple, low cost but beautiful appearance.

Ushauri huu haumfungi kila mmoja, hapa tunajaribu kupeana ushauri wenzagu wa kiwango changu ambao wanajaribu kufikia goals za kuwa na nyumba zao kutokana na kile kidogo walichonacho mkononi. Na maanaisha aliye na kidogo ushauri huu unaweza kutumika kufanya plan ya kibanda chako ambacho unaweza kufanikiwa kukimaliza kwa muda mfupi kidogo na nafasi ikikuruhusu basi utaenda kuandaa kingine unavyotaka wakati uko ndani ya paa la kibanda chako.
 
We Candid tunashukuru kwa ukarimu, kwani wengi wenye mikondo na ujuzi wa vitu hivyo ni siri yao na ukivitaka lazima zikutoke mfukoni. Tunahitaji kuelimishana kwa mtindo huu na hata tulio nje ukitaka tenda tutaamini kwa vile uko mtume katika hili. Bora nianze kidogo kinachowezekana na kukamilika mapema, nikiwa na pa kupaza ubavu wangu ndipo nijaribu ndoto kubwa. Nikihamaki tu kuingia ndoto kubwa nisije ishia njiani.
 
Nashauri ujenzi ambao kwa sasasa tunaweza kuepa gharama ni kuta za ndani ambazo si lazima kutumia tofaili au blocks, na kazi hiyo ya kugawa vyumba inaweza fanyika wakati wo wote kadiri ya mahitaji, kwani cha msingi ni kuta za nje na paa lake.
Candid Scope bana umenichekesha sana, yani nyumba rahisi rahisi wewe umemjengea babaako tena kijijini, lakini yako ya Bunju sio ya matofali ya kuchoma ya kufyatulia hapo hapo saiti! Sitaki kabisa kukaa kijijini usawa huu, ngoja nizeeke...

Anyhow, kuta za ndani that is a no brainer, hakuna haja ya tofali la saruji, absolutely, lakini pia wenzetu mbona hata kuta za nje wanajenga na sheet rock na mbao na hazibomoki? For the life of me sielewi kabisa kwa kweli.

Cheki hawa mafundi seremala wanajenga ukuta wa nje, notice hiyo foundation, kibongo bongo lingemwagwa jamvi la nchi 6, la kokoto nyeusi, na nondo za milimita 16... hahahahahah

url
 
292455_2023742587376_1058331074_31809291_6172102_n.jpg

Ramani za ujenzi wa nyumba husumbua vichwa sana vichwa wengi wanapohaha kutafuta na kubuni ramani iweje. Na pengine tunaangukia kuchagua ramani ambayo umalizaji wa paa lake hutugharibu sana pesa. Nyumba kama hii ni very simple, low cost lakini ina mvuto.

Ramani hii inatoa fursa ya kuongeza vyumba kirahisi maana alternative ya kuendeleza upanuzi wa nyumba yako ni wazi na rahisi. Na hata mpango wa ujenzi kwa awamu una mshiko sana hapa.

Tunaweza kukwepa gharama kubwa za ujenzi wa nyumba kwa kutumia ramani ya mjengo wa kawaida ambao hautatugharamu sana pesa ila tu umaliziaji wake tu ukaweza kuwavunja shingo wapita njia wakaahau kama kofia walizovaa zimedondoka baada ya kufika mbali toka kwenye nyumba yako na kupata wageni wasiotarajiwa kuiba ramani na umaliziaji wako.
Candid, kweli ni nyumba nzuri, kwa macho yangu, naiona kama ni ya single bedrom, sitiing jiko choo na bafu. Japo unaiita ya gharama nafuu, ili ipendeze, hicho kigae tuu na hizo poles zinatoboa funika bovu. Hiyo nyumba hivyo ilivyo mpaka hizo pavements blocks zake na hicho ki garden, its not less than 15M!. Jee hiyo ndio gharama nafuu?. Wale ndugu zetu pale Mabwe Pande, wataweza?.
 
Candid Scope bana umenichekesha sana, yani nyumba rahisi rahisi wewe umemjengea babaako tena kijijini, lakini yako ya Bunju sio ya matofali ya kuchoma ya kufyatulia hapo hapo saiti! Sitaki kabisa kukaa kijijini usawa huu, ngoja nizeeke...

Anyhow, kuta za ndani that is a no brainer, hakuna haja ya tofali la saruji, absolutely, lakini pia wenzetu mbona hata kuta za nje wanajenga na sheet rock na mbao na hazibomoki? For the life of me sielewi kabisa kwa kweli.

Cheki hawa mafundi seremala wanajenga ukuta wa nje, notice hiyo foundation, kibongo bongo lingemwagwa jamvi la nchi 6, la kokoto nyeusi, na nondo za milimita 16... hahahahahah

url

Kuna wale wahind pale Millenium Bussness Park, wameleta pre-fab nyumba za gharama nafuu, nilipouliza gharama halisi ya hiyo pre-fab huouse, nikakuta nyumba ya room 3, sitting, dinning na jiko, inakwenda mpaka 30M. Mimi na familia yangu ya watu 10, tunahitaji nyumba ya 4 bedroms, sitting, dinning, jiko, master, store, laundry, study room, home office, etc, bado tutarudi kule kule, kusema ukweli, vitu vizuri ni gharama, huwezi kukwepa, only unaweza tuu kupunguza!,
 
Hizi baadhi ya nyumba za gharama za kati, ningependa tuzione pale Mabwe Pande.file:///Users/user/Desktop/3663490596_aee9c73b27.jpgfile:///Users/user/Desktop/3720-2.jpgfile:///Users/user/Desktop/3720-2.jpgfile:///Users/user/Desktop/img_3885.jpgfile:///Users/user/Desktop/istockphoto_669415-beautiful-modern-house.jpg
 
Candid, kweli ni nyumba nzuri, kwa macho yangu, naiona kama ni ya single bedrom, sitiing jiko choo na bafu. Japo unaiita ya gharama nafuu, ili ipendeze, hicho kigae tuu na hizo poles zinatoboa funika bovu. Hiyo nyumba hivyo ilivyo mpaka hizo pavements blocks zake na hicho ki garden, its not less than 15M!. Jee hiyo ndio gharama nafuu?. Wale ndugu zetu pale Mabwe Pande, wataweza?.

Note: Aliyeleta mada haimaanishi ufanye hiyo finishing, maana yangu nimevutiwa na hiyo ramani, ukiichukulia ramani hiyo na kufanya tathmini ya ujenzi unaotaka huku ukikwepa yasiyohitajika kwa sasa utakuta unaweza kuijenga nyuma hiyo kwa gharama nafuu ikaonekana nzuri na ukaishi umeridhika.

Kama utahitaji kutengeneza bustani ya kuvutia ni shauri ya wewe mwenyewe huku ukitumia zaidi nguvu zako kuliko makampuni yatakayokutengenezea kwa mamilioni. Vigae si kitu cha lazima kwenye uwanja, na kama utapenda hivyo ni ridhaa yako na pengine unaweza kufanya hivyo wakati nafasi itakapokuruhusu kuboresha zaidi nyumba yako, kwani kwa sasa unachoangalia mahali pa kuishi kuepa gharama za homa zisizoisha za kulipa pango.

Note; mapambo hayo kama nguzo, vigae uwanjani ni mambo extra ambayo wengi huwa hawayahitaji labda baadaye nafasi ikimruhusu. Natanguliza shukrani kama umenielewa.
 
Kuna wale wahind pale Millenium Bussness Park, wameleta pre-fab nyumba za gharama nafuu, nilipouliza gharama halisi ya hiyo pre-fab huouse, nikakuta nyumba ya room 3, sitting, dinning na jiko, inakwenda mpaka 30M. Mimi na familia yangu ya watu 10, tunahitaji nyumba ya 4 bedroms, sitting, dinning, jiko, master, store, laundry, study room, home office, etc, bado tutarudi kule kule, kusema ukweli, vitu vizuri ni gharama, huwezi kukwepa, only unaweza tuu kupunguza!,

Achana na kutumia imported construction material kwa ajili ya kuweka partition ndani ya nyumba yako. Miti na mbao tulizo nazo hapa nchini zinatosha sana na ukiweka juu ya frames hizo plywood nk kisha weka juu yako paint mtundu atajua kama anagongesha kitu kizito vinginevyo atakachojua ni block za matofali ya saruji.

Jambo la msingi tuwe wabunifu wa kufanya mambo haya badala ya kutegemea tu imported commercial construction material ambayo ni very expensive, Sao Hill wanatakiwa wawe wabunifu katika hili.
 
Ndugu zangu. Inaonyesha kuwa amahamua kujenga. Lakini imefika wakati muanze kuishinikiza serikali kuu na za mitaa kuweka utaratibu wa kupima maeneo. Nyumba mnazotoa hapa ni nzuri sana, lakini kama hakuna mitaa na huduma muhimu ni sawa na mazizi ya ng'ombe tu.
 
Hizo nyumba za mbao kila mwaka zina bomolewa na matornado hulo Uamerekani, lakini bado wanaendelea kuya jenga. Kila mtu anacho alichozoea. Uamerekani isipojengua na mbao basi hiyo sio nyumba. Hapa bongo isipojengwa na tofali basi hiyo sio nyumba. Ukuta ikilia ngoma watu hawaitaki.
Pia ukijenga nyumba lako na mbao ya sao Hill, nathani itaku gharimu zaidi kuliko Tofali.
 
Back
Top Bottom