Nyumba ndogo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyumba ndogo!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by BabyGal, Jul 17, 2011.

 1. BabyGal

  BabyGal Senior Member

  #1
  Jul 17, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 189
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii ndio thread yangu ya kwanza inayohitaji michango kwahiyo naomba nianze kwa kuwasalimia wote.
  Salama aleykum kwa ndugu zangu waisilamu na Bwana Yesu asifiwe kwa ndugu zangu wakristo.

  Siku hizi nyumba ndogo zimekua zaidi ya fasheni ambayo wengi hawataki iwapite. Wakina baba wanazidi kuzijenga na kina mama wanazidi kulia nazo.Mimi sina upande kwenye hili swala kwasababu mara nyingi wakina mama wenyewe ndio wanaosababisha hivyo wakina baba wengi wanalazimika kua nazo kujipatia amani na furaha ya moyo.Na utandawazi huu mtu unakuta yuko bize na tv,computer au magazeti yake ya udaku hata hana muda wa kumuuliza mume siku yake iliendaje.Wakati wa kulala bize na simu hata kumpa mumewe busu la kumtakia usiku mwema hatoi.Baridi inapiga badala ya kumkumbatia mume mama yuko bize kuchat na mashoga zake au kuchangia matatizo ya ndoa za wenzake mtandaoni wakati yake inapoteza muelekeo.

  Mume hata atamani vipi kuongea anashindwa kukwambia ukweli kwasababu wewe sio msikilizaji.Mwisho wa siku inabidi akatafute yale anayokosa kwako kwingine.We unakua umempa ndoa jina tu ila matendo yote na raha alizostahili kutoka kwako anapata kwingine.Mkigundua mna wasaidizi ndo viroho vinaanza kupaa na machozi yanawatoka.Sasa badala ya kuweka simu zenu chini muanze kurekebisha nyumba mnaanza tena kulia mitandaoni na kwa marafiki ili muambiwe “shoga mumeo hajatulia.“ wewe ujione hujakosa.Na ndio maana mara nyingi hua hamuelezei tabia zenu zilizopelekea wenzenu kuwatenda bali mnakimbilia tu kuelezea yeye alivyoanza kubadilika.Wakati aliyetangulia ni wewe.

  Mi nnachojaribu kusema ni kwamba sisi wanawake ndio creators wa situation kama hizi.Wengine mtabisha kwamba kuna wanaume hawatulii mara hawathamini wanayofanyiwa sasa mbona huko kwenye nyumba ndogo hua wanakua na adabu?!Unajua kwanini?!Kwasababu anajua anaheshimiwa tofauti na nyumbani ambapo kazi zote zinazomhusu mume mama kamwachia housegirl na majukumu yake ya ndani zaidi amesahau au hata kuyapuuza.

  Nawashaurini kama mama umehusika kwa namna moja au nyingine kumbadili mumeo mpaka akatafuta pakujipumzisha na kero zako au hata kua mlevi acha kulaumu ,kubali makosa na ujitahidi kurekebisha mambo.

  Mwanamke jiwezeshe!Pamoja tunaweza!
   
 2. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Babygal umesahau...wengine hupata mapumziko hapo hapo ndani toka kwa house girl....matokeo yake ni kumfukuza msichana wa watu na matusi kibao bila kuangalia kila leo, dada fanya hivi, dada osha chupi za mme wangu, dada fagia chumbani, kila kitu....dah senki you Babygal for this...
   
 3. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  ukishindwa kumpgiga adui,basi jiunge nae.

  Nadhani wamama wenye nyumba wanahaja ya kujiunga na Nyumba ndogo.mana wameshidwa kuzitokomeza.
   
 4. BabyGal

  BabyGal Senior Member

  #4
  Jul 17, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 189
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wajifunze mbinu wanazotumia kuwafanya wawanunulie magari na hata nyumba wakati nyumbani kabadili cover ya sofa ni ishu.
   
 5. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,279
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Umeolewa BabyGal?

   
 6. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,096
  Likes Received: 7,334
  Trophy Points: 280
  Nyumba kubwa zingine kesi kweli,
  Mtu ndo kwanza umeingia kutoka kazini hata mkoba wa ofisini hujatu wala kuvua viatu, zinaanza shutma, mara kwanin hukunipigia mchana, mbona vocha ulituda kidogo, umechelewa ulikua wapi?
  Nyumba ndogo mnazitengeneza wenyewe nyumba kubwa.
   
 7. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mbinu ni jambo moja,je heshima wanayopewa kwa nyumba ndogo?
  Nadhani kujiunga nao ndo soln .
   
 8. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,279
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Na vidumu vinatengenezwa na nani? Blaming aisaidii inaleta ligi tu. Ndoa zinajengwa kwa communication si vidumu wala vimada period!

   
 9. BabyGal

  BabyGal Senior Member

  #9
  Jul 17, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 189
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndo naelekea!
   
 10. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,279
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  What do you mean by kujiunga na nyumba ndogo? Na nyumba kubwa nayo iwe nyumba ndogo ya ndoa nyingine?? Fafanua!

   
 11. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #11
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,279
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Nakutakia safari njema. Baada ya miaka kumi rudia hii thread yako.


   
 12. BabyGal

  BabyGal Senior Member

  #12
  Jul 17, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 189
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Blaming hua inaanza na kina nani kama sio wakina mama?!Hawazingatii chanzo bali wanalaumu matokeo tu.Alafu unapoongelea communication unajua ni wanawake wangapi sio wasikivu wala wasikilizaji?!
   
 13. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,279
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Nilivyosoma tu thread yako nilijua kuwa bado uko single. Hamna mwanamke aliye kwenye ndoa anaweza andika ulivyoandika hata kama ndoa yake ni ya 100% furaha. Subiri uianze safari ndio utajua vizuri yanayojiri. Siwezi kubadili mawazo yako utajifunza through experience.


   
 14. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  .........kuna baadhi ya wanaume hata uonyeshe mapenzi i vp, hata uwe busy na yeye lakini akikuchoka ni kwamba kakuchoka. Nimeona baadhi ya ndoa wanawake hawajui hata mitandao na bado waume zao wanatafuta nyumba ndogo.

  .......haya babygal vp kuhusu vijijini ambapo utakuta mume mmoja wake zaidi ya 4 napo utasema wanawake wapo busy na internet? Nakwambia hivi hii ni tabia ya mtu kutafuta nyumba ndogo na wala sio tatizo mwanamke.

  Mie kila siku nasema dawa ya cheater ni kumuacha na kuendelea na maisha yako........maisha mafupi jamani haya, hakuna kubembelezana kama ukijua mume ana nyumba ndogo. Uking'ang'ania kuishi na cheater mwishoni utaletewa gonjwa bure ushindwe kulea watoto wako.
   
 15. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #15
  Jul 17, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  kuna wadada are good at blaming other wadada kuwa wako irensposible na ndoa zao ngoja uolewe uyaone.....akicheat kick his ass and move on hakuna haja ya kudwell kny self pity situation.....amecheat amekuumiza for one and second unataka ujilaumu it was all your fault???kwa kisa gani hasaa?yeye kama aliona nakosea alitakiwa kutafuta solusheni ndani through communication sio kwenda nje! period
   
 16. BabyGal

  BabyGal Senior Member

  #16
  Jul 17, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 189
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndivyo mnavyopenda kila mtu aamini.Kwamba hajui chochote mpaka awe ndoani.Well uzembe ni uzembe tu na wamama wengi ni wazembe.
   
 17. BabyGal

  BabyGal Senior Member

  #17
  Jul 17, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 189
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huko kwa kuchokana ni kwingine kabisa kwasababu mtu anajua kabisa kachokwa ila hataki kuukubali ukweli.Nnaowaongelea mimi ni wale wazembe wasiojua kujikagua na kuona makosa yao matokeo yake kesi kwa wazee wa dini kila kukicha.
   
 18. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #18
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,279
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Kila la heri wewe mchapa kazi. Nina imani ndoa yako itadumu miaka 50 bila mumeo kuchovya pembeni.

   
 19. BabyGal

  BabyGal Senior Member

  #19
  Jul 17, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 189
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Samahani kwa kukuchukiza dada maana unavyochuria hiyo yangu sio kawaida.Najua watu wengi hawapendi ukweli na huu ni ukweli mmoja wapo usiotakiwa kusikiwa na kina mama.
   
 20. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #20
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ..........haya mdada, naona wewe ndio wale wanaolea wanaume utafikiri mtoto, eti kisa nisiachwe au asiende kutafuta nyumba ndogo. Maisha ya sasa ni ya kuleana sio kumtetemekea mwanaume utafikiri ndio anayekuwezesha kupumua.
   
Loading...