Nyuma ya pazia Bunge live

Sasa kama miaka yote iliyokuwa bunge live na bado wabunge walikuwa wanalala na hawafanyi kazi. je,sasa kutokuoneshwa ndio kunatofauti gani?kama kuna wabunge hawafanyi kazi hadi bunge lioneshwi live basi hao wana matatizo.
 
Inataka kuwa kama Korea kaskazini, live coverage ni ya kiongozi mkuu tuu mengine subirini mtapewa repoti na vyombo vinavyo chuja habari

hili halikubaliki
 
Sasa kama miaka yote iliyokuwa bunge live na bado wabunge walikuwa wanalala na hawafanyi kazi. je,sasa kutokuoneshwa ndio kunatofauti gani?kama kuna wabunge hawafanyi kazi hadi bunge lioneshwi live basi hao wana matatizo.

Wewe kama mwananchi,utajuaje mwakilishi wako amesema nini bungeni?Na je,ni nani atakuwa anaamua habari hii ni ya muhimu na hii si ya muhimu.Yaani wabunge wachache michango yao ndio itachaguliwa,huoni hapo kuna mwanya wa ukandamizaji?jifikirishe tu kidogo
 
Naunga Mkono Hoja Yako Mtoa Post,
Hili Halihitaji Elimu Kubwa ya kiwango cha P.h.d Kulijua,
Imetokana Na Uimara Na Hoja Nzito Za Wa Wabunge Wa Upinzani,huku wabunge wa chama cha magamba na majipu wakikoroma na kumwagika udenda, Jambo Ambalo Limezidi kukishushia Heshima chama chakavu (CCM )mbele ya wananchi. ndio maana wame amua wasionekane live ili kujaribu kujivika nguo kidogo. katika karne hii ya sayansi na teknoloji jambo hilo ni ujuha mkubwa. linapaswa kulaaniwa na kila mwenye pumzi.
 
Bunge kuonyeshwa au kutokuonyeshwa live, kunawapunguzia nini Wabunge jukumu lao la kuishauri na kuisimamia Serikali?

Wakae ndani humo humo waisimamie Serikali kwa hoja zenye mashiko sio fitina fitina na uchochezi tu, baadhi Wabunge wanataka kugeuza Bunge kama ukumbi wa kufanya siasa ili kujipatia umaarufu mwepesi mwepesi huku wakionekana live.

Sasa tuone kama Bunge lisiporushwa live watatueleza walikwenda Bungeni kuonekana live, au walikwenda kuwasilisha hoja za msingi juu ya matatizo ya wananchi na kuisimamia Serikali kuhakikisha inawajibika?
 
Mimi sikumpa..Magufuli kura yangu....japo waliiiba kura akashinda.sipendi unafiki na roho ya chuki na visasi .Jamani...2020 tusimpe kura japo wataiba..lakini anapaswa kujua jatumtaki!!!!
 
na ww utajuaje kama mbunge wako kawasilisha hoja kama bunge lisipokua live?
 
Mkuu usitegemee jipya CCM ni ile ile.
 

shame on u,yaani mipango ya mustakabali wa maisha ya watanzania upangiwe gizani?Hao tumewatuma wakapange matumizi ya fedha zetu halafu waingie mitini kujadili.Kwanin wanaogopa uwazi?Tutajuaje kama wabunge wanawajibika kuisimamia serikali?
 
A burning candle should not hestate its frame. Cjui hawajiamini? Rusha live tuone serikali ya dr. iavyonyanyambuliwa kwa hoja za vyama mbadala maana group dynamic theory inakubaliana na informal groups cha kufanya ni ku-excel na idea zao katika kufikia organisational goal. Siasa kama huwezi kujenga hoja unapoteza mvuto dakika sifur.
 

Rais kufungua bunge live,waziri mkuu kuhutubia bunge live,mawaziri kuhutubia bunge live,mawaziri kujibu maswali live ila "wabunge kujadili hotuba ya Rais,waziri mkuu na bajeti za wizara gizani"
Hii maana yake nini?uhuni tu
 
shame on u,yaani mipango ya mustakabali wa maisha ya watanzania upangiwe gizani?Hao tumewatuma wakapange matumizi ya fedha zetu halafu waingie mitini kujadili.Kwanin wanaogopa uwazi?Tutajuaje kama wabunge wanawajibika kuisimamia serikali?
Shame on me? No, shame on u brother, kwani hakuna namna nyingine ya sisi kujulishwa kilichokuwa kikiendelea Bungeni iwe na Wabunge wetu au hizo Media, badala ya watu kukaa mwanzo mwisho wanaangalia live, nyinyi hamna kazi za kufanya?
 
Hakuna haja ya matusi au lugha chafu..mjadala huu una afya nzuri.Tujadili kwa kina na kwa hoja ili watawala wetu watusikie.Kwa kukosoana tutajenga nchi na tuwe wakweli.
 
Ile clip ya Wenje kwenye Bunge la Serikali iliyopita kuhusu Mkurugenzi Wilson kabwe nadhani utakuwa umeiona leo.Kwa hayo machache tu inatosha wewe kukubali upinzani ni very strong.

Kanisome tena.

Wenje yupo bungeni?
 
Watafanya kazi kwa adabu kama wapo kwenye kamati.
Wabunge wa upinzani huchangia kwa kukosa adabu pale matangazo yanaporushwa papo. Wakati mwingine hutaka bunge lisitishwe kusubiri hitilafu irekebishwe ili mtu wao aongee na kutukana. Ilifanyika hivyo kwenye Bunge la katiba wakati Tundu Lisu akichangia.
Natamfaham muda wa wapinzani kuhutubia papo kwenye Tv ni kipindi cha bunge nje ya hapo ni nadra sana. Wanahaki ya kulia
 




Kwa mchango huu kiukweli sijakuelewa hata kidogo.

Mimi sishabikii vurugu kabisaa bungeni,lakini kwa kitendo hiki kiukweli hakuna sababu ya uchaguzi 2020 kwani ntashindwa kujua mbunge wangu kafanya nini na kajitahidi vipi kadri ya uwezo wake?? Nikuibie tu siri kwamba
""" moshi mzito wa moto usijidanganye kuufunika kwa neti"" kiukweli tulipofika utambuzi wetu hauzuiliki tena kwa kuzima vyombo vya mawasiliano
Katika mengi ambayo serikalu imefanya kiukweli wengi tunaipongeza, lakini kwa hili la kuzima au kuzuia matangazo kwenye chombo muhimu kama hicho kiukweli mimi nalipinga kwa akili yangu ya juu na kwa hili nikipewa sababu zozote nikakubaliana nalo basi nikamwe akili.



CCM tujikubali tunaweza,,,
Lakini kwa kuzuia matangazo nanyosha mikono

Kama mipira hua inarushwa sembuse bunge????

Kama nilivosema

"" KUAMBIWA SABABU YOYOTE KUHUSU HILI NA NIKAKUBALIANA NA HILI, NAOMBENI MNIKAMATE MNIPELEKE NIKAPIMWE AKILI"""


Wahusika lioneni hili
 
Shame on me? No, shame on u brother, kwani hakuna namna nyingine ya sisi kujulishwa kilichokuwa kikiendelea Bungeni iwe na Wabunge wetu au hizo Media, badala ya watu kukaa mwanzo mwisho wanaangalia live, nyinyi hamna kazi za kufanya?

Kwahiyo huyo mbunge wako ndio aje kukuambia kilichotokea bungeni?wakati gani?Hivi mbunge siku hizi ndio muhabarishaji wa mambo yaliyotokea bungeni?Na mwandishi afanye kazi gani?Hizi akili za wapi jamani?Kuna wabunge wangapi wanachangia kwa siku na kwa dakika ngapi kila mmoja?Je,chombo gani kitaweza kuhabarisha kila lilitokea bungeni?kwa utaratibu upi?
Fundi cherehani,muuza duka,mama ntilie,machinga,boda boda,wastaafu na watanzania wengine ambao kazi zao huweza kufanya wakiwa wanasikiliza bunge,sasa una maana gani kusema hamna kazi za kufanya.Usikariri,hebu tuambie hasara kubwa mbili za kurusha bunge live.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…