NYOTA YAKO LEO JUMAMOS JUNI 14/2025:
UKIWA NA SHIDA YOYOTE YA KINYOTA NA TIBA, NIPO MOROGORO MJINI NAPATIKANA KILA SIKU OFISINI KWANGU FOREST KILEKA KUANZIA SAA 12 ASUBUHI MPAKA SAA 12 JIONI.
MAALIM ANAPATIKANA MUDA WOTE.
★MAPACHA– GEMINI ♊ (May 21– Juni 20)
Leo Jitahidi kukutana na wakubwa zako wakusaidie kukupa ushauri bila hivyo itakuwa vigumu kwako kutatua matatizo yako yanayokukabili hasa yale yanayohusiana na mapenzi na ndoa.
•Safari zako ulizopanga hazina tatizo lolote nenda na utafanikiwa na utarudi salama.
★KAA– CANCER 🦀 (Juni 21– Julai 22)
Ili kukamilisha mipango yako ni lazima ukutane na mtu mmoja mkubwa akiwa yupo hapa au yupo mbali akusaidie kuondokana na yanayokusibu vinginevyo hakuna mafanikio katika jambo lolote.
•Utapata bahati nzuri sana Leo na haja zako zitatimia bila kutarajia.
★SIMBA LEO 🦁 (Julai 23– Agosti 22)
Leo hata kama ukikubaliana na mtu yoyote jambo lolote ujue atakwambai usubiri kwanza au atakucheleweshea mahitaji yako kuwa na subira na tumia hekima utafanikiwa.
•Haja zako zitatimia Leo ingawa kwa shida kidogo lakini Vumilia na uwe na subira zaidi leo.
★MASHUKE– VIRGO ♍ (Agosti 23– September 23)
Pamoja na kwamba leo itakuwa siku nzuri kwa kila jambo lako utakalolifanya unashauriwa kuwa usianzishe mambo mapya endeleza yale ya zamani na utafanikiwa tu.
•Safari zako ni nzuri lakini jizuie na tamaa sio nzuri zitaharibi ndoto zako.
★MIZANI– LIBRA ⚖️ (September 24– Oktoba 23)
Leo kuna uwezekano wa urafiki wako kuvurugika unashauriwa kuwa makini katika kuchagua marafiki wengine watakutaka wewe ili kupata kitu na sio marafiki wa kweli.
•Utapata maudhi kidogo Leo na bado inaonekana unashida fulani ndogo ya kiafya haikuwazishi sana lakini inakunyima furaha shida hiyo itaisha na sio tatizo kubwa ni mtihani wako na mara nyingi wewe ukiumwa ni daraja lako la mafanikio ukipona kuna mambo yanakutokea au yanabadilika na kuwa mazuri hivyo stahmili hali hiyo ni ya mapito kwako na ina kheri na wewe.
★NG'E– SCORPION 🦂 (Oktoba 24– November 21)
Leo jaribu sana kuwa karibu na watu wa dini ili uweze kubarikiwa mambo yako fanya ibada kwa mujibu wa imani yako na toa sadaka kwa watoto yatima maskini na wajane na utafanikiwa.
•Safari sio nzuri kwako leo kwakuwa utapata maudhi maudhi na utapoteza muda wako kwa mengi licha ya kuwa utafanikiwa kila kitu.
★MSHALE– SAGITTARIUS 🏹 (November 22– December 21)
Leo usipokuwa makini unaweza kupoteza vitu vya thamani kubwa kuwa makini katika mambo yako hasa nyie ambao mnaotumia usafiri wa umma katika kufanya safari zenu za hapa na pale.
•Maswala yako ya kipato yatazidi kunawiri kwa upande wako na watu wako wa karibu watazidi kuchanganyikiwa juu yako hivyo jihadhari na makosa madogo madogo yanaweza kukutoa kwenye furaha na faraja uliyonayo kwa sasa.
★MBUZI– CAPRICORN 🐐 (December 22– January 20)
Leo jihadhari sana kujumuika na vikundi visivyofaa hasa nyakati za jioni kama una matatizo yanayokusumbua jaribu sana kuwasiliana na wataalamu ili wakusaidie kuondokana na matatizo hayo hata kupata ushauri.
•Mahusiano yako yatakuwa mazuri punde tu baada ya kusikia habari mbaya dhidi ya nyumba ya mtu au biashara ya mtu kuungua au wewe mwenyewe kujeruhiwa na moto japo kidogo tu ujue kuna kitu kizuri mno kinaenda kutokea kwenye Mahusiano yako.
★NDOO– AQUARIUS 🏺 (January 21– February 19)
Leo inaonekanakana kuwa mambo yako yapo hatarini kuharibiwa na watu wengine hasa wale ambao wako katika serikali au katika dini unatakiwa kuwa mpole kuwa muda huu ili kupisha dhahama hiyo iondoke.
•Maswala yako ya biashara yatatanuka au yatastawi zaidi na utazidi kuyaona matunda ya juhudi zako za kila siku dhidi ya utafutaji wako.
★SAMAKI– PISCES 🐟 (February 20– March 20)
Leo jaribu kuwa muangalifu na mtu yoyote ambaye utashirikiana nae katika jambo lolote wengine watataka kukuingiza katika mambo ambayo yatakuletea balaa kubwa na hasara kuwa makini sana.
•Tegemea kupata furaha na faraja kubwa katika siku hii ya leo pia amani itazidi kutawala katika nafsi yako.
★PUNDA– ARIES 🐏 (March 21– Aprili 20)
Tumia muda huu kukamilisha mambo yako uliyokuwa umepanga kuyafanya Fanya safari kutana na wadau wa biashara zako na tekeleza wajibu wako kazini Mambo mazuri yanakuja.
•Haja zako Leo ni ngumu kukamilkka au kutimia kwakuwa siku ni nzito kwa upande wako.
★NG'OMBE– TAURUS 🐂 (Aprili 21– May 20)
Leo ni siku mbaya kwako kuna uwezekano wa wewe kupata balaa katika mambo yako jaribu sana kuwa muangalifu katika kila jambo ambalo umepanaga kulifanya au la si hivyo unaweza kuharibikiwa pakubwa.
•Safari sio nzuri hata kidogo labda jua likizama na siku kubadilika ndo mambo Yako yanaweza Kuwa mazuri.
★★★★★★★★★★★★★★★
Kwa ushauri na mengineyo wasiliana na nami, siku njema na mafanikio mema
Dogoli kinyamkela 💀☠️ MTABIRI WA NYOTA NA MTAALAM WA MAMBO MBALI MBALI YANAYO HUSIANA NA NYOTA ZENU.