Nyoka Amng'ata Mtu Uume (could it be in defence?!)

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
Hizi habari kutoka Australia zinashitua kinamna yake! Nyoka alimuuma jamaa aliyekuwa anajisitili porini. Sasa sijui nyoka huyo alifikiri nini kichwani mwake...duuh, ni bora tu hata angemng'ata dole gumba la mguuni..... Mimi nadhani saa nyingine wanyama wengine huwa wako overly defensive sana bana kuona wameingiliwa kwenye anga zao na wapinzani!

Source link: http://www.news.com.au/story/0,23599,23776403-2,00.html

SteveD.
 

Wanasema watu wa huduma ya kwanza kwamba unaweza kufunga kamba kwa kuikaza ili sumu isiendelee kusamba sasa sijui jamaa aliweza kufanya hilo!
 
hao nyoka wangeletwa dar wakasambazwa barabarani kote kwani wanaume wamezidi kukojoa hovyo ... mitaani ndiyo usiseme kila kichochoro kinanuka mikojo ... dereva wa daladala anazunguka nyuma ya daladala utamuona kajibanza na kukojoa hapohapo ...
 
hao nyoka wangeletwa dar wakasambazwa barabarani kote kwani wanaume wamezidi kukojoa hovyo ... mitaani ndiyo usiseme kila kichochoro kinanuka mikojo ... dereva wa daladala anazunguka nyuma ya daladala utamuona kajibanza na kukojoa hapohapo ...

ni wanaume tu wanaokojoa?
 
ni wanaume tu wanaokojoa?

ujamalizia neno hovyoooo ... kweli mnakojoa hovyo jiana tena mchana kweupe .. hiyo miti/ maua ilopandwa barabara i.e tazara na kwengineko ni mashahidi wakubwa kwa haya ... pengine na binaadamu wengine wataniunga mkono hasa wanaokerwa na tabia hii ... wengine hukojoa mbele za watoto ... akilewa kidogo anauliza ... nimwage radhi nisimwage huku watoto wamemzunguka wakisema mwaga ... huyoooo anafanya kweli

Mwanaume huyo ... wanawake ... sijaona ... ila pengine moshi nasikia wanawake hukojoa wima wima ... mhhhh!
 

Naima hata wanawake wanakojoa vichochoroni labda hujabahatika tu kuwaona. Wakulaumiwa si wanaume wala wanawake bali ni city council ambayo haioni umuhimu wa kujenga vyuo jijini ili kukidhi haja ya wakazi na hata wageni wa jiji. Ukishikwa na haja Dar, akili inaweza kukuzunguka uende wapi kujisitiri. Njemba pale Dar hazikawi kuzuka New Africa, Kilimanjaro Hotel na mahoteli ambayo yamejengwa hivi karibuni.
 
Mwanaume huyo ... wanawake ... sijaona ... ila pengine moshi nasikia wanawake hukojoa wima wima ... mhhhh!

...aaah da naimaomari,

jamaa alikuwa kachuchumaa, sijui yapi yalimsibu mpaka akaamua kuchuchumaa...


...The deadly brown snake slithered between his legs and lunged at his manhood as he crouched on a roadside near Laura,...

...anyway, ndio hivyo tena, sijui ingekuwa mwanadada huyo nyoka angefanya kituko gani wallahi!!!...
 
...anyway, ndio hivyo tena, sijui ingekuwa mwanadada huyo nyoka angefanya kituko gani wallahi!!!...[/QUOTE]

Duh....Ingekuwa taabu tupu.........
 
tatizo kubwa hilo, duh jamaa alipata bahati ya tiba na ole wake arudie kuchimba dawa kwenye vyoo vya kike...

Naimaomari, wanaume wanakojoa sana barabarani kwa kuwa wanaonekana ila wanawake wanajificha mno ktk vichaka hivi vya dar na huwa akipanua miguu tu anajitutumua hapo hapo kwani ukizunguka nyuma ya nyumba nyingi za bongo utakuta ardhi imechimbika kama shimo la mdako ambapo mara nyingi ni matokeo ya mashambulizi ya kike kupitia mkojo, ila kibaya zaidi ni kuwa mwanamke akipata nafasi ya kuchuchumaa kichakani huwa anamaliza mpaka na ile haja nzito....

tabia ikemewe kwa watu wote si wakuwanyooshea vidole (vya macho) wanaume tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…