Nyoka aina ya Cobra alazamisha ndege kutua kwa dharura

BANDOKITITA

JF-Expert Member
Oct 4, 2022
1,177
2,281
Rubani wa Afrika Kusini, Rudolf Erasmus ambaye alitua kwa dharura baada ya kugundua nyoka mwenye sumu kali aina ya cobra akiwa amejificha chini ya kiti chake.

Rudolf Erasmus alikuwa akiendesha ndege ndogo binafsi mapema wiki hii akiwa na abiria wanne kutoka jiji la Bloemfontein kwenda Pretoria, alihisi kitu cha baridi kikishuka kwenye sehemu ya chini ya mgongo wake. Alitazama chini kwa haraka na akaona kichwa kikubwa cha nyoka huyo aina ya Cape Cobra kikirudi uvunguni mwa kiti,” alisema..

“Ilikuwa kama vile ubongo wangu haukuwa ukitambua kilichokuwa kikiendelea,” rubani huyo aliliambia shirika la habari la Associated Press.

Baada ya kufikiri kwa haraka, aliwajulisha abiria wake juu ya utelezi wa vyoka huyo.

“Kulikuwa na kimya cha kushangaza,” alisema. Kila mmoja alitulia hususani rubani.

Erasmus alimpigia simu mdhibiti wa safari za anga ili kupata ruhusa ya kutua kwa dharura katika mji wa Welkom uliopo katikati ya nchi ya Afrika Kusini. Bado alilazimika kuendelea kuruka kwa dakika nyingine kati ya 10 hadi 15 na kutua akiwa na nyoka amejikunja miguuni mwake

“Niliendelea kumtazama kumuangalia yuko wapi. Alikuwa na furaha uvunguni mwa kiti,” Erasmus alisema. “Huwa siogopi nyoka, lakini kwa kawaida siwakaribii.”

“Napenda kumpongeza Rudolf kwa hatua za kijasiri alizochukua na kwa jinsi alivyoshughulikia tukio hili ambalo lingeweza kuwa tukio baya la safari za anga,” alisema mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Afrika Kusini (SACAA) Poppy Khoza.

“Alibaki kuwa mtulivu katika hali hiyo ya hatari na kuweza kutua salama bila kusababisha madhara yoyote kwake na abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo, na akiionyesha dunia kuwa yeye ni balozi wa usalama wa anga wa ngazi ya juu.”

Erasmus aliviambia vyombo vya habari kuwa alimgudua nyoka huyo akiwa katikati ya safari, baada ya kuhisi kitu cha baridi kikimkandamiza mgongoni.

“Kwanza nilifikiri ilikuwa chupa yangu ya maji… lakini baadaye nikagundua kuwa ni kitu kingine na (hivyo mimi) sikusogea,” alikiambia kituo cha habari cha News24. Tukio hilo lilitokea Jumatatu.

Cape Cobra ni aina ya nyoka wenye sumu ya hatari ya neurotoxic ambayo inahitaji matibabu ya haraka ya dawa ya kuzuia sumu, nyoka hawa hupatikana sana maeneo ya kusini-magharibi mwa Afrika Kusini.
Vipi hili tukio lingemkuta Mbongo, ingekuwa zaidi ya Majaliwa mpiga mbizi aliepelekwa fire, sasa sijui huyu angepelekwa. Eb toa ubashiri wako.
 
Back
Top Bottom