Nakusalimu mwafrika nakusalimu habari gani, nikaribishe tuketi niseme yaliyo ndani../
Umesahau kuhusu hadithi za kale za upendo wako nataka leo tukae tuijadili kesho yako.../
Kutoka kupiga ramli na kutii mizimu, umeanza kufata amri za tv na simu.../
Na ubaya ni kwamba umeanza kuikacha sanaa, na kufata siasa ambayo inakulaza na njaa.../
Na kila unachokiona unataka kubeba, vichache vimekushinda na unataka kuongeza..../
Juzuu katekisimu mpaka novena, sio zako zako ilikua ni kutamba ngonjera..../
Umezubaa majirani wameanza kufika kwako, na unaamini kua watakubebea shida zako..../
Kwasababu ujinga umezidi umasikini, unamjengea jirani kwako unachimba unabaki chini.../
Zamani ulikua unasembe ya kusaza, uliabudu kazi uliweka jembe kwenye shamba.../
Ghafla ukauza panga ukapanga jembe kwenye kabati, ukanunua kioo ujirembe ili uende na wakati.../
Umechagua urembo umetupa werevu, unauza mifugo unafuga kucha na ndevu.../
Familia ife mwafrika uzame mitini, au uombe msaada wakati unakufa na fashion mwilini.../
Mwafrika unamzigo mkubwa wa madeni, hauna mali ardhi yako ni future ya wageni.../
Unalala ndani kungoja hisani ya wenye nguvu, nyumba iko wazi we uko ibadani unaabudu..../
Ujasiri ni kujimudu mwafrika haujui hili, umejaliwa nguvu na unashindwa kuzihimili.../
Unavamia diplomasia unatunga hotuba, na hakuna mwenye hisia kua upo nyuma ya muda.../