Nyimbo za Dini sehemu za Starehe

Nyimbo za Dini sehemu za Starehe

Kuna kitu kimoja ambacho wengi hawakijui tokana na upofu wa Kiroho. Kimsingi dunia inaendeshwa na mambo mawill. Neno la Mungu(Unabii) na wakati(Majira). Neno la Mungu (Unabii tena uliotoa Yesu mwenyewe unasema) Sharti injili ihubiriwe kila Mahali na watu wote wasikie kuhusu Yeye(Mathayo 24:14) kwa hiyo sasa ndio wakati(Majira) ya utimilivu wa Neno hilo.
Unachopaswa kufanya ni kutii, kunyenyekea na kumuamini Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wa Maisha yako kwani yeye ndio njia kweli na uzima sababu majira ya ukamilifu wa dahari yametimia sasa. Unasubiri nini mwana JF, fanya maamuzi sasa kwani kesho yako ni fumbo na umilele wako umekaribia. Ataenda wapi kwenye umilele wako? Sasa ndio muda wa kuandaa makazi yako ya umilele wako
 
Mara ya mwisho hili songi nimepigiwa pale mianzini A town december mwaka jana sijui baa gani ile....aseee vyombo vimekolea yani niliinuka kwa utamu niliinjoi mnoo halafu akamalizia na mkono wa bwana alooooo acha tu.
Huu wimbo mkono wa bwana wanaupenda 😀 niliona hata harusini pia watu waliolewa Ndo wanaimba balaa na kucheza🤣🤣🤣
 
MATHAYO 7
Kuhusu kuwahukumu wengine
(Luka 6:37-38,41-42

1“Msiwahukumu wengine, msije nanyi mkahukumiwa na Mungu;
2 kwa maana jinsi mnavyowahukumu wengine, ndivyo nanyi mtakavyohukumiwa; na kipimo kilekile mnachotumia kwa wengine ndicho Mungu atakachotumia kwenu.
3 Kwa nini wakiona kibanzi kilicho jichoni mwa ndugu yako, na papo hapo huioni boriti iliyoko jichoni mwako?
4Au, wawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi jichoni mwako,’ wakati wewe mwenyewe unayo boriti jichoni mwako?
 
MATHAYO 7
Kuhusu kuwahukumu wengine
(Luka 6:37-38,41-42

1“Msiwahukumu wengine, msije nanyi mkahukumiwa na Mungu;
2 kwa maana jinsi mnavyowahukumu wengine, ndivyo nanyi mtakavyohukumiwa; na kipimo kilekile mnachotumia kwa wengine ndicho Mungu atakachotumia kwenu.
3 Kwa nini wakiona kibanzi kilicho jichoni mwa ndugu yako, na papo hapo huioni boriti iliyoko jichoni mwako?
4Au, wawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi jichoni mwako,’ wakati wewe mwenyewe unayo boriti jichoni mwako?
Ukimaanisha???
 
Lazima zipigwe baa ndipo kuna wana wapotevu...ili wamrudie mungu....ndio maana yesu mwenyewe alikuwa anawatafuta wenye dhambi ili awaokoe..hata akirudi duniani sehem ya kwanza ataanzia kidimbwiiiiii
Ikiwa ni kwa kazi hiyo basi hazina tija, maana zinapigwa kila siku na mambo ni yale yale!!!
 
Yesu mwenyewe alikuwa anakwenda kwa wenye dhambi na anaongea nao na kula nao, sembuse nyimbo tu!
Tena siku hizi kuna hizi liveband huwa wanapiga cover unakuta walevi ugimbi umeshapanda kichwani watu wanasifu na kuabudu ukuu wa Mungu.
 
TUMEUONA MKONO WA BWANA , ASEEEEE HILI SONG LINA BAMBAAAAA MNOOOOOO
Mwaka juzi tulienda club moja hiv,aisee ilipigwa hii mida ya saa kumi usiku ilikuwa balaa! Halafu Dj akaongezea na Hakuna mungu kama wewe... nilishangaa sn vile watu walilipuka shangwe wakiwa nyingiii
 
Back
Top Bottom