Nyimbo za Dini sehemu za Starehe

Nyimbo za Dini sehemu za Starehe

Kusema ukweli huwa nakereka sana kusikia nyimbo za dini, zinapigwa kwenye sehemu za starehe, hasa Bar. Sehemu hizi ni sehemu Shetani na jeshi lake wanafanya kazi zao kwa ufanisi, na anaona ni kama kuikosea heshima dhana ya kuwa nyimbo za dini ni sehemu ya kuabudu.

Kwenye hizi Bar, zinapopigwa nyimbo hizi wakati watu wamelewa, naona ni kama kumkebehi Mungu.

Na pia ni kuzikosesha heshima nyimbo hizi, ambazo zilipaswa kuzikumbusha nyoyo Utukufu wa Mungu.
Wacha akili za kipuuzi, aliyekuambia Bar ni sehemu ya kishetani ni nani? Kuna sehemu ya kishetani zaidi ya haya makanisa ya kina Mwamposa au Misikitini?
 
Dunia na vyote vilivyomo ni vya Mungu....utasemaje bar ni sehemu ya shetani.

Kuna ule wa "Yesu unipende leo kuliko jana", ukipigwa halafu vyombo tayari vimekolea unatamani hadi kumpa dj hug.
Kuna dude limeimbwa na Zabrone Singers linakwenda kwa jina la "MKONO WA BWANA" acha kabisa. Mpaka baadhi ya ndugu zetu Waislam wanausikiliza
 
Hapana ni vi, uri tu ili apate neno nao hapo hapo walipo wafuatwe na neno
Utampata wapi mlevi umpe neno?
Wakati akiamka tu kalewa
 
Sehemu hizi ni sehemu Shetani
Nani aliekwambia dini NI kanisani tu ? Mwamposa alianza kuhubiri Bar moja ipo pale Sinza jioni walevi kabla ulevi haujakolea alikua anapewa kinasa na kipaza sauti anaanza kuhubiria walevi kwanza akimaliza walevi wanaendelea kupiga gambe km kawaida
 
Kuna dude limeimbwa na Zabrone Singers linakwenda kwa jina la "MKONO WA BWANA" acha kabisa. Mpaka wale wanaokula futari wanao
Ndio hio Mkono wa Bwana imetafasiriwa kinyume yaan ni wale wanaopewa Bia za offer ndio huimba kwa furaha kwa yule alietoa offer wanye Bure, umuimbia kua wameuona Mkono wake maana alinyoosha tu wale pale wape bia buckets 3 wanywe wagalegale, likipigwa humgeukia na kumuimbia 'tumeuona Mkono wako Bwana'
 
Jamani anayetibiwa si mgonjwa hao ni kwamba wanaonekana wamepotea hapo ndo wanapata ujumbe wa Mungu ili watubie .
 
Mi nikiwa nakula vitu vyangu vikishakolea napenda sana ukipigwa HAKUNA MUNGU KAMA WW BWANA,

2. Kuna ule mwingine 'CHINI CHINI CHINI, CHINI HATA JUU, WATU UNAWAINUA....'

Huwa nainjoy sana nyimbo za Mungu nikiwa Bar.

Pale ni pahala ambapo nafsi hufurahi, watu wa Mungu tupo
 
Injili Haina mipaka,
Yesu ni WA wote,
Acha zipigwe tu.

Aaah!
Aaaah!
Tumeuona mkono wake!
Bwanaaaaah!

🤣🤣🤣
 
We mtoa uzi vipi babu izo nyimbo zinatakiwa zipigwe uko uko bar wale walevi ndo wanaohitaji kukumbushwa unataka zikapigwe church tena inatakiwa wasikilizishwe kondoo waliopotea
Kichwa kimeshachanganyika wataelewa nini? Na tunajua Bar si sehemu ya staha
 
WANAOZIIMBA TU NI WATU WA SHETANI FULL KUJICHUBUA NA WENGI WAO HAWANA NDOA NA HAWASALI TENA NI WAZINZI WA KUTUPWA,HAPO UNASEMAJE?

Sent from my SM-G950U using JamiiForums mobile app
Utakapoulizwa utoe ushahidi wa uzinzi wao unaweza? Au ndivyo unavyowadhani? Dhana inaweza kukupeleka kupata dhambi, hata hivyo kama wewe unalijua na viongozi wa dini zao wanalijua walipaswa kuwanasihi kwa sababu wao wanakuwa ni kioo kwenye jamii yao. Ama vipi ni bora wajiondoe kundini kabisa, kama yule Mzee Yusufu alijisema yeye amerudi rasmi kuimba taarabu na hawezi kuchukuliwa kama kigezo cha ntu wa dini.
 
Wacha akili za kipuuzi, aliyekuambia Bar ni sehemu ya kishetani ni nani? Kuna sehemu ya kishetani zaidi ya haya makanisa ya kina Mwamposa au Misikitini?
Misikiti inaingiaje kwenye ushetani hapo?

Pombe ni zana ya shetani karika kumuingiza mtu kutenda dhambi. Kwa sababu anapoteza uwezo wake wa akili wa kawaida. Ni wangapi washafanya maasi wakiwa wamelewa na waliporudiwa na akili wakaanza kujutia?
 
Hapana ni vi, uri tu ili apate neno nao hapo hapo walipo wafuatwe na neno
Utampata wapi mlevi umpe neno?
Wakati akiamka tu kalewa
Na akiwa keshalewa anaelewa nini? Neno linapaswa kuipata akili inayoweza kutafakari.
 
Nani aliekwambia dini NI kanisani tu ? Mwamposa alianza kuhubiri Bar moja ipo pale Sinza jioni walevi kabla ulevi haujakolea alikua anapewa kinasa na kipaza sauti anaanza kuhubiria walevi kwanza akimaliza walevi wanaendelea kupiga gambe km kawaida
Sijasema dini ninkanisani tu! Umenisingizia hapo, sitaja jila la sehemu yoyote ya ibada. Najua dini na ibada inaweza kufanyika popote kwa sharti pawe pasafi. Nakataa Bar si sehemu mojawapo.
 
Kusema ukweli huwa nakereka sana kusikia nyimbo za dini, zinapigwa kwenye sehemu za starehe, hasa Bar. Sehemu hizi ni sehemu Shetani na jeshi lake wanafanya kazi zao kwa ufanisi, na anaona ni kama kuikosea heshima dhana ya kuwa nyimbo za dini ni sehemu ya kuabudu.

Kwenye hizi Bar, zinapopigwa nyimbo hizi wakati watu wamelewa, naona ni kama kumkebehi Mungu.

Na pia ni kuzikosesha heshima nyimbo hizi, ambazo zilipaswa kuzikumbusha nyoyo Utukufu wa Mungu.
Likipigwa Lile la hakuna mungu kama wewe😂😂 Lile goma Haina mpinzani
 
Jamani anayetibiwa si mgonjwa hao ni kwamba wanaonekana wamepotea hapo ndo wanapata ujumbe wa Mungu ili watubie .
Sasa ikiwa aliyekunywa haruhusiwi hata kuendesha gari, unadhani ataweza kutafakari neno???
 
Back
Top Bottom