Nyimbo unayoipenda kuliko zote duniani

Nyimbo unayoipenda kuliko zote duniani

Kama ni moja ni wimbo na wingi wake ni nyimbo.
Kwangu mimi ni 'MAMA' kutoka kwa Tancut almasi.
Watu wazima wenzangu watakuwa wanawakumbuka hawa vijana kutoka Iringa zama hizo,wakiongozwa na Kasaloo Kyanga na Kyanga Songa ilikuwa na burudani tupu.
 
Mkuu kwa kutaja wimbo huo pengine utakuwa unajua nyimbo nyingi za Tancut Almas. Kuna wimbo wao mmoja niliusikia mara chache sana mwaka 1992 wenye kibwagizo kisemacho "wamama mwipulike" ila sijui jina la wimbo. Kama unaufahamu (au mdau yeyote) naomba unitajie jina la huo wimbo. Hayo maneno ya kibwagizo nadhani ni lugha ya kihehe.
 
Mimi list yangu ya nyimbo nizipendazo sana ni ndefu. Na kuna wimbo mmoja ambao unashika namba moja lakini kwa sababu zisizoweza kuzuilika sitaweza kuutaja hapa hadharani. Sababu ya kutoutaja ni haya matumizi ya ID fake hivyo kutu-limit kutaja baadhi ya mambo. Lakini ni wimbo ambao kiukweli uwa natamani hata siku nimekufa huo wimbo upigwe wakati naagwa kabla ya kupelekwa kaburini (samahani kwa maneno hayo). Nyimbo zingine zinazofuatia ni:
2. Take a Chance on Me wa ABBA,
3. Ghost Busters wa Ray Parker Jr,
4. Mshenga na. 2 wa Mbaraka Mwinshehe,
5. You are My Everything wa Surface
6. Till I Met You wa Ray Parker Jr
7. Earth Song wa MJ
8. Locked in Love wa Brandy
9. Walimwengu(?) wa Salum Abdallah
10. Kidela wa Abdul & Ali Kiba
Hiyo ndiyo top ten yangu kwa sasa. Japo huo wa kwanza ambao sikuutaja jina hautakuja kubanduka kwenye namba yake.
 
Boyz II Men,Whitney Houston,Celine Dion,Backstreet Boyz hao hawajawahi kuniangusha,
Chris de Burgh-Lady in Red,
Wimbo flani wa Dully anampelekea mpenz wake maua na kuyachoma moto.
Bob Rudala-Nimekuchagua wewe.
Mr.Paul-wimbo flani anaelezea mpenzi wake alivyojitokeza nitaucheck jina lake.
Album ya mwanzo ya Marlow uliokuwa na wimbo Busu la pink

Zipo nyingi kwa kweli.
 
Mkuu kwa kutaja wimbo huo pengine utakuwa unajua nyimbo nyingi za Tancut Almas. Kuna wimbo wao mmoja niliusikia mara chache sana mwaka 1992 wenye kibwagizo kisemacho "wamama mwipulike" ila sijui jina la wimbo. Kama unaufahamu (au mdau yeyote) naomba unitajie jina la huo wimbo. Hayo maneno ya kibwagizo nadhani ni lugha ya kihehe.
Dah sorry mkuu huo wimbo siupati kabisa lakini naamini palipo na wengi hapaharibiki jambo,atatokea muungwana tu wa kutoa jina la huo wimbo.
 
Mm naomba mwenye mashairi yake haka kawimbo sikuwa na kaseti nilikuwa nasikia kwa kukaibia ibia
Unaimbwa hivi
Sheiraaaa, ooh sheiraaaaa.
Mpenzi sheira kuwa na huruma ,......
Wengi wapo wanaokupenda ila huyu nimempata kwa bahati.

Naomba wimbo mzima nakapenda sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom