umukagame
JF-Expert Member
- Apr 10, 2014
- 1,044
- 672
Kuna baadhi ya wanaume wamebarikiwa sana,,ukikosea tu ukajirudisha ndo Kwisha
"Usiniache kwenye dunia ya maumivu, Usiniache kwenye mvua ya sononeko,.. Njoo unirudishie tabasamu kwenye maisha yangu.. Njoo unibusu nabusu lako litokomeze maumivu haya ..Bado nahitaji joto tamu la huba toka kwako .. Njoo basi unifute machozi.. Nirudishie zile siku tamu ambazo baridi iliponisurubu usiku.. kimbilio langu lilikuwa kumbatio kwenye mwili wako .. Bila uwepo wako kwangu, tafsiri ya neno maisha ni ukatili.. Njoo basi uniambie unanipenda tena..
Kila ufikapo usiku nimekuwa kiumbe nayezama kwenye bahari ya machozi. Sababu moyo wangu umepondeka sana..
Nirudishie furaha ktk maisha yangu.. Njoo nakoleo ya upendo ili niitumie kulizika neno huzuni.. Tabasamu lako ni wakili pekee awezaye kunitoa ndani ya hili gereza la mateso ya upweke..
Njoo ufungue kinywa chako chenye meno meupe yaliyo ktk mpangiko sanifu.. kisha utoe kibali ili ulimi wako unitamkie kuwa bado unanipenda ...Njoo basi hata unidandanye kuwa bado nathamani kwako ili tu unisogezee siku za kuitazama hii dunia inukayo jasho la dhambi.
Yanini nikudanganye kuwa ntakuhonga dunia?! ..Bila ulazima nijiongezee kifurushi cha dhambi ya kujitakia?!!.. Ilikhali najua dunia njia?!!.. Neno nakupenda sitoacha kukwambia.. Sababu neno nakupenda licha ya uchache wa herufi zake.. lina thamani zaidi chochote chini yahizi mbingu. Hasa linaposimama kama kamusi kwenye swala la kuzitafsiri hisia za moyo uliobeba shehena nzito ya upendo wa kweli.. Kama huu upendo nilionao mimi kwako.''
Huyu mtu utamjibu nini