Painful Poem: Art in Dreams

Ankoh Mazukuh

Member
Jan 16, 2023
27
29
Sasa kwanini ukunifanyia haya yote ufanyayo sasa?
Nasikia sauti za vilio, nasikia sauti zikipaza angani.
Nasikia watu wakiomboleza, natamani baadhi yao niwafute machozi lakini siwezi, siwezi mwanakwenda, siwezi mwanakwenda, maana nimeesha kwenda.

Sauti naongea kutoka juu, nasikika kutoka chini, chini, yaani chini ya aridhi wadudu na funza wakinishambulia.
Roho yangu rehani, naiaga dunia kwa style hii,
Bye bye wanadhiara, goodbye huku niendapo natangulia tu bali nyote mtafika, bye bye nawapenda sana, ipo siku tutaonana.

Still bado najiuliza, sasa kwanini ukunifanyia hayo yote?
Kwanini mwanadhiara kwanini? Maana nilikupenda, haikuwahi pita siku nisikufikirie.
Hakika nilikupenda sana, kiasi cha kuamua kuja huku nilipo baada ya kushindwa kuvumilia.

Nilishindwa kwa maana ulikuwa mzuri sana, kila alie kuona mbele yako alikupenda mno kiasi kilicho nifanya niogope kuwa na wewe, lakini..
Moyo unatak moyo da, moyo moyo wangu nilikukosea nini kiasi ukanitesa kiasi kile?
Dah hakika napumzika. Nimechoka mwanadhiara, nimechoka, nimechoka acha nipumzike pahala pema peponi, Amin.

Inaniuma sana, maana bado nakujali, naumia sana ninapo kuona jinsi unavyotamani nifufuke naumia sana.
Natamani hata nirudi nikuone, lakini swali moja laniletea ukakasi, kwanini mwanadhiara kwanini, kwanini pindi nikiwa hai haukuwahi kunitamkia unanipenda?
Kwanini mwanadhiara kwanini, nilikupenda na kukujali na kukupa penzi la kweli na wala hakujua kushinda kwangu hata kipindi naugua, haukuweza pata taarifa kwa maana ulipuuzia nilipokwambia naumwa cancer ya moyo kwa sababu ya kulikosa penzi lako.

Hivi utajiita muuaji, ama mkunga mwadilifu kwa maana nimekufa kwa ungojwa ambao dawa yake wewe ndio mmiliki?
Ama utajiita mbinafsi kwa kushindwa kurudisha fadhila nilizokupa, ama utajiona mjinga?
Mwisho utaawaza kitanzi ama madawa?

Please nakuomba usiangukie huko, bado nakupenda ila siwezi kukwambia tena maana mdomo umeshafunga na macho hayaoni tena.
Siwezi mwanadhiara siwezi tena!

Nafurahi kuona jinsi unavyoijali familia yangu japo hawakupendi.
Napata faraja pindi ujapo makaburini kuipamba maua nyumba yangu ya milele.
Ile picha yangu nzuri uliyoiweka chumbani kwako fahamu kuwa napata tabasamu la moyoni kila uitazamapo na kuikumbatia.
Na vile unavyonifikiria kila muda nafurahi kuona jinsi unavyonipenda sasa japo siwezi tena, siwezi mwanadhiara siwezi rudi siwezi.

Pole sana kwa kukuachia kovu kwenye moyo wako, kweli sasa wanipenda kuliko siku zote za maishani mwako.
Lakini kwanini haukufanya haya yote pindi nikiwa hai hata nami nitabasamu?
Tazama sura yangu kwa mara ya mwisho, tazama haiwezi hata kutabasamu,tazama mwanadhiara tazama jinsi nilivyo mkavu.

Aisee bye bye mwanadhiara, nilikupenda sana lakini haukuona thamani ya penzi langu.
Hakika upendo wa kweli upo, sema upo kaburini!
Ona nimekufa sasa, naumia kwa kuwa nimekufa na furaha yako. Ona hauwezi kula usiku kutwa unashinda unalia.
Pole mwanadhiara pole, maana siwezi tena.

Natazama upande wa duniani nawaona ndugu marafiki na jamii nzima wakilia na kuomboleza.
Dah naumia sana kumuona rafiki yangu wa karibu akiumia. Dah kaza mwanangu jikaze, maisha ndio yanaenda hvyo ila ipo siku tutaonana tu.
Upande wa pili namuona yule binti alinipendaga sana, yupo na bwana mwingine wanaupiga mwingi.
Dah, asa najiuliza ni kama ningemwamini kuwa mimi na yeye nimpaka kifo ni vipi kama ningempa nafasi ya mwanadhiara?
Dah mapenzi buana!

Kule vile naiona familia yangu ikiumia sana, huku wakimdhihaki mwanadhiara kwa kosa la kusababisha kumpoteza ndugu yao kwa ungonjwa wa cancer ya moyo.
Maana walitambua ni jinsi gani nilimpenda ni kiasi gani nilijitoa kwa ajili yake, lakini yeye alichukulia poa tu.
Japo moyoni najisemea mwacheni jamani huyo ni familia yenu, mpeni nafasi yangu bado nampenda, hakika nilimpenda kweli!

Ghafla nasikia sauti ikiniita huku nikishikwa bega, ikiniambia
Karibu nyumbani kijana hii ndio nyumba yako ya milele hakika umepokea uzima wa milele, karibu ukaketi na Bwana Muumba wako.

Huku hakuna majonzi kama unavyowaona ndugu zako huko na muda umeisha kuishi humo pole sana.
Lakini usijali, wakiifwata njia ya haki hakika wataiyona neema ya Mungu baba.
Karibu kijana mwema karibu, huku kunayo furaha tele ilyojaa upendo.
Sahau mateso yote uliyopitia, sahau nakwambia sahau kijana.

Karibu!

Ah hivi sasa hivi saa ngapi? Dah, ndio kwanza saa saba hivi, kutakucha kweli nikampokee mpenzi wangu kutoka kwenye dhiara yake? Dah muda umeenda halaf sijui ndoto gani hizi nimeota dah, sema skumbuki vizuri. Acha nilale maana nikijaribu kuifikiria itaniletea ukakasu.

Story by @ogmunix___
MUNIXPIC ENTERTAINMENT
IMG_20230331_104603.jpg
 
Back
Top Bottom