Nyie wachora ramani waongo sana

Mnyiramba

JF-Expert Member
Jun 19, 2022
1,112
2,957
Kuna class mate wangu baada ya kumaliza secondary aliamua kwenye kusomea mambo ya kuchora ramani na ujenzi kwa ujumla, basi baada ya miaka kadhaa kupita nikamtumia picha ya nyumba na ukubwa ninaotaka nyumba za vyumba viwili tu sema vile vyumba vya kujinafasi mita 5 kwa 5, baada ya kuichora akanitumia picha na pia nikamwambia anipigie makadirio itachukua matofali mangapi na bati ngapi!

Alivyopiga hesabu akaniambia tofauti 1100 tu mzigo Tayari unaisha! Nikasema maisha si ndio hayo najenga chap chap! Nilichokutana nacho hizo tofali 1000 zimeisha tu kwenye msingi halafu kiwanja ni tambarare!

Hadi nilivyoandika hapa nimekimbia msingi na aliyechora ramani tumegombana hadi urafiki umeisha
 
Inategemea alimaanisha tofali za ukubwa gani na ww umetumia za ukubwa gani

Ukute alikuambia tofali za blocks ww ukatumia za kuchoma ( bricks) hapo lazima mgombane tu!

Karibu nikusaidie kuifanyia makadirio upya kama hutojali

Nimetumia tofali za blocks mkuu sio za kuchoma jamaa ameniponza sana mahesabu yangu ilikuwa milioni 3 tu ngoma ishapendeza matokeo yake hata kifusi cha msingi sijamwaga
 
Kuna class mate wangu baada ya kumaliza secondary aliamua kwenye kusomea mambo ya kuchora ramani na ujenzi kwa ujumla,basi baada ya miaka kadhaa...
Ujinga wa mjinga mmoja umeshindwa kumwambia hukohuko ila ulichoweza ni kukimbia kazi yako
 
Mkuu sijawahi kujenga hata kibanda cha kuku ndio maana niliingizwa mkenge kirahisi na mtaalamu fake
nina mshakaji wangu mbishi sana alikua na picha na clip ya nyumba fulan kali sana toka 2017 akisema atajenga nyumba kama hii akikaa vizur.

Akamuliza fundi makadirio ya tofali,cement kila kitu ili boma likamilike,, nyumba ya vyumba vi 3 vya kulala, chumba kimoja master, choo public, jiko, sehem ya kulia chakula na sehem ya kupumzika.

Jamaa akafanya kimya kimya et akitaka aje anioneshe boma likikamilika..sasa makadrio ya yule fundi yalikua ni uongo jamaa akaona mbona hela inatosha tu hii baada ya kupiga hesabu kutokana na makadirio ya fundi akakurupuka kuanza ujenzi.

Kaishia kwenye msingi na hela imekata anamtukana kila siku yule fundi..kumbe nilivokua nambishia hiyo hela halitosis yeye akaona mimi namshauri vibaya akamsikiliza fundi alafu mimi akanificha kwanza
 
Back
Top Bottom