Nyie CCM kipi hakipo hapoo......? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyie CCM kipi hakipo hapoo......?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sinafungu, Sep 26, 2011.

 1. sinafungu

  sinafungu JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2011
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 1,406
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Tuliambiwa huko nyuma na ninyi, Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne
  1. watu
  2. ardhi
  3. siasa safi
  4.uongozi bora
  sasa leo imetimia miaka 50 ya uhuru Nchi iko ktk giza, hospitali madawa hakuna , shule ni za kata madawati hakuna, akina mama wanajifungulia njiani , barabara mbovu. (gari za wagonjwa uchangie mafuta). TUNAOMBA MYUJUVYE KIMEPUNGUA NINI KATI YA HAYO MANNE ..........?
   
 2. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Subiri uambiwe wewe ni mchochezi, CCM watakuambia kikubwa wanachojivunia ni kudumisha Amani inayoifanya Tanzania kuwa nchi ya mfano. Ukiwauliza Amani maana yake nini? watarudia kukuambia wewe ni mchochezi!!!!!! Sitaki kusikia kitu kinachoitwa CCM
   
 3. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  1. Watu wameongezeka from 8mil (1961) to nearly 43 mil (2011)
  2. Ardhi bado ile ile baada ya jaribio la Idd Amin Dadaaaa kushindikana kuipunguza. Sana serikali iko busy kuwapa kuwapa wageni ile ardhi yenye rutuba WAWEKEZAJI......
  3. Siasa zimeongezeka maana sasa hata kwenye mikutano ya kisiasa mwanasiasa anaruhusiwa kuingia na bunduki na kuionyesha kwa makusudi kabisa na akitoka kula bata usiku ana ruhusa kupiga risasi mbili tatu angani.
  4. Uongozi bora ndo usiseme, tumepiga hatua sana, UFISADI uko juu hadi raha, UWAZI kwenye mikataba inasainiwa hadi guest/hotelini huko majuu, UWAJIBIKAJI uko juu maana mtu analiingizia hasara taifa na anasema hang'oki, au analiingizia hasara taifa na anawajibika kwa kujiuzulu tu na kuendelea kutafuna hizo cash..... na mengineyo...

  CCM na Tanzania ya miaka 50 oyeeeeeeeee!
   
Loading...