Nyerere vs Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyerere vs Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bujibuji, Jul 28, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,381
  Likes Received: 22,253
  Trophy Points: 280
  Hawa watu wana mizaha sana, lakini kwanini hotuba za Kikwete hazina nguvu wala msisimko kama zile za Mwalimu?

  Hata kiutendaji Nyerere alimzidi sana Kikwete.

  Je kulikoni kwenye kambi ya Kikwete?
   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Nyerere alikuwa na vision,alijua wapi analipeleka taifa.

  Kikwete hana vision aliingia ikulu akidhani ni mahali pa kucheka cheka. Aliingia Ikulu akiwa na deni la kuwalipa fadhila waliomsaidia kuingia Ikulu.

  Kikwete hayuko tayari kufanya maamuzi makubwa kwasababu anaogopa kuwaudhi maswahiba wake. Kwa upande wa nyerere alikuwa tayari kufanya maamuzi makubwa na magumu kwa faida ya taifa.

  Azimio la Arusha ni moja ya maamuzi makubwa kuwahi kutokea tangu Tanzania ipate uhuru.
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Mkubwa huhitaji kumlinganisha ka lolote huyu baharia na Nyerere, hana jipya!
   
 4. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nyerere namsifu tu kwa kutunza rasilimali zetu. Kwa hili BIG UP mzee Nyerere huko ulipo, Lakini kwa uchumi na maaisha ya waTz kwa ujumla sina cha kusifia. Miaka yote aliyoongoza Nyerere watanzania wameishi kwenye dibwi la umasikini wa kutupwa. Aneyebisha na atoe hoja.

  Miaka yote hiyo kama vision zake zingekuwa sahihi tungekuwa mbali sana kiuchumi, lakini hatuwezi hata kujilinganisha na nchi kama kenya ambayo ukabila umekuwa ukiwatafuna kila kukicha. Sisi hatuna vita, je Nyerere alitufikisha wapi.

  Jamani nashauri tuwe wakweli na si kusifia tu hata pumba. JK, kwa demokrasia big YES. Lakini uchumi umedorora, haoneshi tofauti na na nyerere, wote watu wamebaki kuwa masikini wakutupwa. ila watu wanauhuru, hatusikii mauaji ya wahubiri au kupigwa kwa wahubiri wa dini si sheikh nani wa mchungaji mtikila aliyepigwa na polisi, wote ni mashahidi.

  Je tutarajie Kikwete kuja na vision mpya au ndo kasha-lost tayari?
   
 5. Companero

  Companero Platinum Member

  #5
  Jul 28, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Herufi za mwanzo za majina yao zinafana. J na J. Kufanana kwao huishia hapo.
   
 6. K

  Kamuna JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 297
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Kimsingi ni makosa kuwalinganisha Nyerere na Kikwete.Hawa watu wako in two extreme side of the bar.Mmoja yupo kwenye integrity side na mwingine yupo kwenye usanii zaidi.
   
 7. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Huko sasa ndio kumkosea heshima baba wa taifa kabisa unafikiria kuwa compare the two individuals? Yaani ni sawa na kuulizia yupi hatari kati ya simba na fisi mbele ya nyati.
   
 8. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kikwete = Kingwendu
   
 9. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #9
  Jul 29, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyerere alitawala wakati mwingine na Kikwete anatawala sasa wakati dunia inabadilika kwa haraka sana
   
 10. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #10
  Jul 29, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Masihara haya!
  Unamfananisha Ronaldo de Lima na Gaudence Mwaikimba!!
   
 11. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #11
  Jul 29, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Ni kweli kabisa Nyerere katika utawala wake alifanya makosa mengi, na yeye alikiri na akawasisitiza warithi wake kwenda na wakati na kurekebisha makosa yake. Lazima tuone tofauti hapa, mara baada ya uhuru kwa kweli taifa lilifanyiwa majaribio mengi sana na katika majaribio haya kuwa na uhakika kuwa makosa mengi yangefanyika. Utakumbuka tumepokea uhuru enzi za hamasa za Ujamaa wa nchi za mashariki, kiongozi yeyote wa wakati huo ilikuwa ni lazima achague kuwa atakuwa upande gani wa vita baridi. Ama ubepari ama ujamaa. Sisi tukaangukia ujamaa na tunajua jinsi ulivyotuletea madhara. Hayo yalikuwa na majaribio ya mwelekeo wa nchi baada ya uhuru.

  Baada ya uhuru hatukuwa na wazalendo wasomi wengi ambao Nyerere angewakabidhi majukumu ya ujenzi wa nchi. Utakumbuka Nyerere kwa makusudi alizuia uchimbaji wa madini yetu kwa hofu kuwa hatuna wataalamu na hao wa nje watakachofanya nikutuibia tu.

  Ni tofauti kabisa na sasa, Kikwete hayuko katika majaribio tena, kila kitu kiko wazi, tafiti ngapi zimefanyika. Sasa hapa ndipo tunapokuja katika suala la uwezo wa organization. Sio siri sasa tunaona tofauti kubwa sana kati ya enzi za Mkapa na hizi za Kikwete. Wakati wa Mkapa taifa lilikuwa na nidhamu, uchumi ukapanda, mfumuko wa bei haukuwa wa kutisha. Doh sasa mambo ni tofauti kabisa, na kwa kweli tumerudia enzi za ruksa, mambo yanakwenda hovyo, kila mtu anaweza kufanya ama kusema atakalo bila hata hatua zozote kuchukuliwa, nchi kama vile haina mwenyewe, watu wanaiba pesa nyingi tu na ni kama vile watu wanampigia mbuzi gitaa acheze.

  KUMLINGANISHA JK NA NYERERE NI SAWA NA KULINGANISHA USIKU NA MCHANA.
   
 12. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #12
  Jul 29, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Kuchekesha ni kipawa..
  Kuchekesha huku unaeleza vitu vya msingi ni kipawa tofauti kabisa na hicho cha kwanza..!
   
 13. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #13
  Jul 29, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Tafadhali sana mkuu usilinganishe mlima kilimanjaro na kichuguu
   
 14. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #14
  Jul 29, 2010
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  kwanza kabisa humu ndani ya JF hakuna kubishana bali kinachotuleta humu ni kuelimishana. Siyo sahihi kwamba Nyerere enzi zake alikuwa ni hodari tu wa kutunza rasirimali bali pia alikwa ni mweledi wa kuziendeleza. kuanzia Mwinyi, Mkapa hadi Kikwete wamekuwa wakiiuza mashirika yanayoitwa mashirika ya Umma. Jiulize mashirika hayo yalianzishwa na nani?

  Mashirika zaidi ya 400 yameshauzwa mpaka sasa na kati ya hayo zaidi ya asilimia 99 yalianzidhwa wakati wa mwalimu. Mwalimu anapokea Tanganyika toka kwa wakoloni alikuwa na wahandisi wawili tuu, lakini ni mambo mangapi ameyafanya katika eneo ya uboreshaji wa miundo mbinu.

  wakati uchumi wa Tanzania uko juu ndipo Mabepari na mabeberu walipoanzisha vita dhidi ya Tanzania, kwanza kuitumia Kenya kama kituo chao cha mashambulizi pia kwa kuzuia bidhaa malighafi za tanzania kuingia kwenye soko la Dunia. Hali hiyo ilisababisha nchi kukosa fedha za kigeni.

  Kubwa kuliko yote Mwalimu hakuwa Fisadi wala hakuulea Ufisadi wala hakufadhiliwa na Mafisadi.
   
 15. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #15
  Jul 29, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  nfyiiiiiiiii.... we mwanawe! wapi na wapi????
   
 16. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #16
  Aug 2, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu ngwendu,

  Nadhani umezaliwa juzi hata hujui Nyerere alitufanyia nini sisi Watanzania baada ya nchi kupata Uhuru. Nyerere alikuwa na sera madhubuti zilizokuwa zikilenga MAENDELEO YA WATU WOTE na si ya wachache na wala si ya maendeleo ya vitu. Labda nitoe mfano ambao unaweza kukuhusu hata wewe na familia yako.

  Mimi ni mmoja wa Watanzania tuliozaliwa kijijini na kukulia huko. Katika familia yetu tulikuwa watoto kumi. Ingawa tulikuwa na shule karibu kabisa na nyumbani, baba yangu aliweza kupeleka shule kaka zetu wawili tu kwa kushindwa kuwalipia ada wengine 4 ambao walikuwa wameishafikia ama kupita umri wa kwenda shule. Tulipopata Uhuru Nyerere akaja na sera yake ya elimu bure kwa wote wakubwa na wadogo. Kutokana na sera hiyo watoto wote 9 tuliweza kwenda shule hadi kufikia elimu ya Sekondari bila matatizo na leo hii wote tuna kazi nzuri, watoto wetu wameweza kusoma, na hata wajukuu watanufaika kupata maisha bora kutokana na sera za Nyerere. Tusingelipata nafasi hiyo maisha haya bora tusingeliweza kuyapata.

  Naamini kabisa kuna familia nyingi sana nchini mwetu zilizoweza kunufaika na sera hii ya Nyerere ya Elimu Bure kwa Wote. Wakati Mwalimu anaacha uongozi asilimia 98 ya wananchi walikuwa wanajua kusoma na kuandika ukilinganisha na asilimia 20 ya wakati wa utawala wa mkoloni. Wasomi wote waliokuwepo nchini wakati Mwalimu anaachia uongozi walisoma bure ndani na nje ya nchi. Ni urithi ulioje na wa kudumu wa siasa za Nyerere ambazo zilikuwa zikijali maendeleo ya WATU.

  Umezungumzia suala la uchumi. Nyerere alikuwa na mipango mizuri katika kutaka kujenga uchumi wa Tanzania tatizo lililokuwepo ni kukosekana kwa wataalamu wa kutosha kuweza kufanikisha mipango iliyokuwepo. Mfano mmoja umeishauzungumzia wa kuhifadhi rasilimali zetu hadi sasa waliopo wanazichezea na hatimaye tutabakiwa na mashimo bila faida yoyote ya maana.

  Mkuu ngwendu, si vyema kusingizia Nyerere kwa uchumi duni. Nyerere alijitahidi sana kufanya yaliyotakikana kukuza uchumi wa nchi. Wachina hivi sasa wamesonga mbele kiuchumi kutokana na kuwa na viwanda vya kila kitu. Nyerere naye katika uongozi wake aliona umuhimu wa kujenga viwanda. Tulikuwa na viwanda vya kila aina nchini mwetu wakati wa awamu ya Nyerere. Viwanda hivyo vilikuwa ni vyetu wenyewe Umma wa Tanzania na si mali ya Muhindi wala muwekezaji yeyote kutoka nje. Tulikuwa na viwanda vya nguo vya kujitosheleza kabisa - Mutex, Mwatex, Urafiki, kiwanda vya matairi bora kabisa pale Arusha, Kiwanda cha ku-assemble magari pale Kibaha. Kulikuwa na viwanda vya Sukari, Kiwanda cha karatasi Mgololo, viwanda vya kutengeneza viatu - Moro Shoe n.k., kulikuwa na kiwanda cha kusafisha almasi Mwadui .... viwanda vya chuma, hata viwanda vya kutengeneza nyembe za kunyolea ndevu vilikuwepo. kulikuwa na viwanda vya kutengenezea sabuni, viwanda vya kusindika mafuta (hata kijijini kwetu kijiji cha ujamaa Nzihi tulikuwa na mashine ya kusindika mafuta na kutengeneza sabuni zetu wenyewe - asante siasa ya UJAMAA NA KUJITEGEMEA!) Vijiji vingi vilivyozingatia utaratibu wa kuendesha vijiji vya ujamaa vilipiga hatua kubwa kimaendeleo hadi pale walipoingia wahuni na mafisadi waliohujumu juhudi hizo. Halikadhalika, vilianzishwa viwanda vidogo vidogo chini ya (SIDO) ambavyo mpaka leo wapo wananchi wanaonufaika kiuchumi kutokana na juhudi hizo. Nenda Gerezani pale Kariakoo uone matunda ya viwanda vidogovidogo mafundi seremala na fundi vyuma wanatunza familia zao na kurithisha ujuzi kwa watoto wao kutokana na viwanda hivyo tangu enzi ya Mwalimu.

  Uchimi pia unahusu uimara wa Mabenki nchini. Tulikuwa na benki yetu wenyewe ya NBC ambayo ilikuwa na mtandao nchi nzima lakini tukaihujumu sisi wenyewe. Nakumbuka kipindi hicho wapo wafanyakazi wa kawaida tu wa NBC waliokuwa wakiibia benki na kununua magari kuwakoga wenzao! Hatimaye, benki ikaanza kuzotora na akatokea kiongozi aliyejiona ana akili nyingi na kuibinafsisha benki hiyo kwa Makaburu ambao walihamisha fedha zetu nyingi na kupeleka kwao. Cha kustajaabisha ni kwamba kiongozi huyo eti aliona Makaburu (waliowanyanyasa Waafrika wenzetu Afrika Kusini kwa karne nyingi wanaweza wakatusaidia sisi Watanzania!)

  Nikirudi kwenye suala la uchumi, nchi ilikuwa imeanza kujitosheleza kwa kuwa na viwanda vya kutosha kuweza kuinua uchumi wa nchi badala ya kutegemea bidhaa za kuagiza kutoka nchi za nje. Kilichokuwa kinahitajika ni kutatafuta mbinu bora za kuweza kuviendeleza. Ilitegemewa kwamba awamu zilizofuata zingeliweza kuelewa na kuzingatia umuhimu wa nchi kuwa na viwanda vyake. Ukizingatia kwamba tayari sasa nchi ilianza kuwa na wasomi na wataalamu wa kutosha, na kama viongozi waliofuata akiwemo JK wangeliweza kutilia mkazo sera za kuviendeleza viwanda vilivyokuwepo ama kuvifufua vile vilivyokuwa vikilegalega kwa kuwatumia kikamilifu na kuwapa motisha wataalamu wetu, leo hii tungelikuwa kama hiyo Kenya unayoisifia na hata kuizidi.

  Katika hotuba yake moja ambayo inarushwa sana katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi. Mwalimu anaeleza jinsi ambavyo katika Awamu yake yalikuwepo mema ambayo yalianzishwa kwa manufaa ya Taifa ambayo yalipaswa kuchukuliwa na kuendelezwa na awamu ya zilizofuata. Halikadhalika alikiri kwamba yapo makosa yaliyotendeka na kueleza kwamba ni dhahiri makosa yangelitendeka kwa sababu wakati huo nchi ilikuwa haina wataalamu wa kutosha kuweza kutenda mambo kwa usahihi uliohitajika. Akasema kwamba kinachoshangaza ni kwamba viongozi waliomfuatia badala ya kuchukua yale mema na kuyaendeleza wameyaacha na kung'ang'ania mabaya.

  Hatuwezi kumsingizia Nyerere kwa kuanguka kwetu kiuchumi. Uzembe na ubinafsi wa wale waliopewa majukumu ya kusimamia sekta za kiuchumi ili zifanye kazi kwa ufanisi wakiwemo baadhi ya viongozi na wananchi waliokuwa na tamaa ya kujinufaisha binafsi bila kujali Watanzania wenzao na taifa linaumiaje kwa ujumla, ndio sababu kubwa ya kuanguka kwetu hadi leo hii.

  Halikadhalika, jambo jingine lililotokea ni kwamba kila kiongozi aliyeingia madarakani tangu awamu ya pili hadi hii ya nne, kutokana na inferiority complex hujaribu kuongoza nchi kwa kutaka kumpiku Mwalimu badala ya kuchukua mema. Matokeo yake wanakuja na mipango mbadala isiyoleta maendeleo yoyote ya maana kwa wananchi na nchi kwa ujumla. Kwa hiyo, leo hii tunajaziwa bidhaa feki madukani na tumeshindwa kabisa kuendeleza viwanda vyetu ili viweza kuzalisha bidhaa bora na kusaidia kukuza uchumi. Eti Sasa hivi cha muhimu ni maendeleo ya vitu na si ya watu. Tumefika mahali viongozi wetu wanatuambia kwamba uwingi wa magari ya wakazi wa Dar es Salaam unaosababisha foleni za kijinga barabarani ni maendeleo!

  Tukiachilia mbali ya uchumi wa nchi. Kenya unaowafisia juzijuzi katika harakati za uchaguzi uliopita wameuana kwa maelfu. Tanzania kila chaguzi zinapita kwa amani, utulivu hata pale panapokuwa na uibaji wa kura. Hatujawahi kusikia wananchi wenyewe kwa wenyewe wakiuana zaidi ya viongozi kwa ubabe wao kutoa amri FFU wawashughulikie wananchi wanaodai haki yao ya kidemokrasia. Utulivu huu wa wananchi na amani inayotamalaki havikuota kama uyoga bali vimefanyiwa kazi. Mwalimu alijitahidi kujenga amani nchini kwa ku-discourage ukabila na udini katika kila nyaja. Watanzania walikuwa wakiishi kama ndugu. Hakukuwa na tabaka la maskini na matajiri uchwala wanatajirika kwa kuiibia nchi na kudhulumu jasho la walipa kodi kwa kujilipa mishahara minono.Tusishangae huko twendako tukawa kama Kenya kwa sababu ya viongozi wetu kupuuza misingi iliyowekwa na Nyerere ya kupalilia na kudumisha amani nchini.

  Mkuu Ngwendu,tumuombee Nyerere astarehe kwa amani. Aliyoyafanya kwa taifa letu ni makubwa na mengi mno yanaweza kujaza kurasa kibao za maandishi. TUM-ENZI!
   
 17. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #17
  Aug 2, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Boramaisha, kigarama na mbalinga, Asanteni sana kwa hoja. Nijuavyo watu wengi humu jf wemezoea kutukana watu lakini nyinyi mmejenga hoja kutetea hoja. kweli mnastahiki kuwemo humu jamvini, Once again asanteni sana,
   
 18. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #18
  Aug 4, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu ngwendu,

  Sasa ninachokiomba ni Dr. Slaa ayachukue yale mema yote aliyofanya Mwalimu kwa taifa hili na ambayo yanaweza kuwa na manufaa katika zama hizi. Zaidi ya yote, aelekeze akili na mawazo yake kwa Watanzania wanyonge kama ambavyo Mwalimu alivyofanya baada ya nchi kupata Uhuru. Mwalimu angeliweza sana kuwa kama Marais wengine wa Afrika ambao baada ya kupata madaraka walikimbilia kujilimbikizia mali na kuwaacha solemba wananchi walioshiriki katika kumng'oa mkoloni.

  Nasema hivyo kwa sababu kwa jinsi hali ilivyo viongozi wa CCM hawana tofauti na hao viongozi wa Afrika waliokimbilia kujilimbikizia mali badala ya kuwahudumia wananchi waliowapigia kura na kuwapa dhamana ya uongozi.

  Kura yangu dhahiri itaenda kwa Dr. Slaa kwa sababu tunataka mageuzi sasa na si vinginevyo. Namuomba Mwenyezi Mungu ashushe malaika wake wamlinde Dr. Slaa katika kipindi chote cha kampeni dhidi ya mafisadi na waganga na manajimu uchwala wa CCM.
   
Loading...