Nyerere: Salaam zenu mnaomkejeli!


Umeletwa ushahidi hapa kwamba nchi za kiislamu ama zilizo na idadi kubwa ya waislamu kama Uturuki, Pakistani, Saudi Arabia na india wanao watu wao wanaowaita "baba wa taifa".
Kwa ubishi wako unajifanya wewe ndiye muislamu kuliko wao. Yani dini wakuletee wao halafu wewe unajidai kuifahamu kuliko wao wenyewe! Kwamba wao hawafahamu kwamba neno baba ni la kikanisa!? kama huu ndio uislamu mnaofundishwa hapa Tanzania, basi mna kazi kubwa ya kufanya.
 
Aliyakuta zaidi ya hayo, usitujaze ujinga kuwa kayaleta yeye, neno "Sheikh" kiarabu ni kama Kiswahili "Mzee" kwa hiyo ukisikia mtu anaitwa Sheikh Nyerere wala usishangae. Ni simply imemaanishwa Mzee Nyerere, lakini si "baba". NO.

Mama Faiza Foxy unaumiza sana kichwa chako, wewe mwite unavyotaka, nao hao wanaotaka kumwita Baba wa Taifa, mjomba wa Taifa, babu wa Taifa waachie, hakuna kipengele kwenye katiba kinachokulazimisha kumwita Mwl. Nyerere Baba Taifa, hiyo ni heshima tu chagua unaloona linakufaa.

Chama
Gongo la Mboto DSM.
 
Hatutaki heshima za Kikatoliki, hukohuko kanisani, huo ndio udini wenyewe, kwanini mlazimishe kitu ambacho kinawaudhi wengine?

Mama Faiza Foxy labda mimi nilipitwa kuna siku ambayo serikali yetu iwe tangu mh. Raisi (mstaafu) Benjamini Mkapa au hii ya sasa ya mh. Jakaya Kikwete ilitoa shurutisho la kuwataka watanzania wamwite Mwl. Nyerere Baba wa Taifa? Wewe kwa nafsi yako ulipendelea tumwite vipi?

Chama
Gongo la Mboto DSM
 

Sijaelewa msingi wa hoja yako kwani universally, George Washington is regarded as father of his nation - USA;

Kuhusu hoja ya kutawaliwa na wazungu ndio kigezo cha kumuita mwanaharakati aliyeongoza mapambani dhidi ya ukoloni BABA WA TAIFA is a fallacy from the outset; China ina founding father wake Sun Yat - Sen, anaetambulika kidunia, katika jamii ambayo ilikuwa predominantly non - Christian;
 

Sasa hueleweki, kitendo cha kuwahifadhi na kuwapa mafunzo ya kijeshi wapinzani wa Idd Amini ndani ya aridhi yetu kinaashiria nini kama siyo dalili za uchokozi? Umekubali kuwa baada ya mwanza kupigwa Tanzania haikujibu, kwa nini? Je waliotaka kumpindua Amin mwaka 72 si walikuwa wanatokea katika aridhi ya Az, je huo sio uchokozi? Kwa ni nini Nyerere alikiuka mkataba wa Mogadishu, alikuwa na nia gani?
 
Aliyakuta zaidi ya hayo, usitujaze ujinga kuwa kayaleta yeye, neno "Sheikh" kiarabu ni kama Kiswahili "Mzee" kwa hiyo ukisikia mtu anaitwa Sheikh Nyerere wala usishangae. Ni simply imemaanishwa Mzee Nyerere, lakini si "baba". NO.

Maana yangu hapa ni kwamba upande mwingine wa dini, watanzania wengi hawajali kuwaita neno lolote la kuonyesha heshima kwao hata kama haitokani na dini yao, iwe ina maana ya neno kaka, mjomba, ndugu n.k; hiyo ndio Tanzania ya Nyerere ninayoizungumzia na nitakayojivunia mpaka tamati yangu duniani kama Mtanzania;
 
FF ni mabaki yale ya 1990s ya kutaka kusilimisha Africa baada ya kushindwa "HASIRA KAMA MTOTO MWENYE UTAPIAMLO" kila siku uislam , ukristo. uislam, ukristo, uislam ukristo these parots"!!!!
 

Suala la Nyerere na ubaba wa muungano nimelielezea kwa kina kwenye hoja yangu ya msingi, tafadhali rejea;

Kuhusu Mahatma Ghandi, kama ulinisoma vizuri, nilisema kwamba mara nyingi, sio wakati wote, kiongozi wa harakati hizo uendelea na kuwa Rais wa kwanza wa taifa huru husika. Na ondokana na mtazamo kwamba ubaba wa taifa unakuja pale tu mapambano ya uhuru yanapoisha na kiongozi huyo kuwa rais wa kwanza; Nyerere hakuwa baba wa taifa mwaka 1961 au Mwaka 1970; Hata kina Ghandi na wengineo, heshima hiyo haikuja kwa namna hiyo; naomba utumie muda kidogo kutafakari mambo na pia uwe unafanya utafiti kidogo, itasaidia mjadala huu utawaliwe na hoja za kutojirudia rudia na badala yake hoja ya kusonga mbele;

Kuhusu Kambona, naona haujui historia ya nchi hii vizuri, jaribu kuisoma kidogo uelewe nafasi ya Kambona katika harakati hizo kama inafanana na kina Nyerere, Kunambi, Kandoro na wengineo;

Ni muhimu ukasoma historia ya harakati za taifa hili ili ubaini what qualifies taifa letu - father of the nation au founding fathers; mtazamo wako ni kama as if hata mapambano ya kumtoa mkoloni Mwalimu aliwaburuza watu na kutumia mabavu na udikteta, kitu ambacho sio inherent na mapambano yoyote ya kujikomboa; soma historia ya nchi yako Tanzania ili uelewe nini kilichojiri mpaka mwalimu akastahili sifa hiyo badala ya kina kawawa na wengineo;
 
TEC inaongozwa na nani? Pope unamlinganisha na nani hapa nchini? Sheria tulizonazo zimetoka wapi? Unazikumbuka zile AMRI 10 za Mungu? FF huyu wa sasa sio yule wa mwanzo!
 

Wacha kuruka ruka wewe, inaelekea hujui Nyerere ameanza kuitwa baba wa Taifa lini, kwa kukusaidia tu ni kwamba hoja yako iko emotional, ina flaws nyingi.

Wewe unadai heshima ya BABA WA TAIFA NI SUALA LA KISHERIA, Lete hiyo Sheria basi inayotamka kwamba Nyerere ni Baba wa Taifa la Tanzania, unazunguka zunguka.

nakukumbusha kwenye hoja yako ya msingi unasema hivi:
Ubaba wa taifa sio Mapenzi ya mtu mmoja mmoja aidha kwa kutumwa au kwa juhudi binafsi bali ni heshima kwa mujibu wa sheria kama tulivyokwisha ona

LETE HIYO SHERIA MJOMBA, INAYOSEMA NYERERE NI BABA WA TAIFA.
 
Baba wa Taifa ni mmoja na ni Hayati Julius Nyerere....


Tena imetokea sana hii tabia hasa katika uongozi wa awamu nne na ninasikia BOSi mwenyewe hajawahi kumuita Baba wa taifa na hataki na wala haamini kuwa Nyerere ni baba wa taifa ILA ANAMUITA MZEE NYERERE SAWA NA WAZEE WENGINE. KUNA MTU ALINUAMBIA NA KWELI MKIMFUATILIA KATIKA HOTUBA ZAKE ZOTE HAJAWAHI KUMUITA BABA WA TAIFA.
 
safi sana kwa hoja. wanaomchafua baba wa taifa kuficha madhaifu yao wanajisumbua watanzania hawa si wale wa jana kifikra wanajua wapi mbivu wapi mbichi na wanaoingiza udini tusibishane nao coz ni kupitiwa kwa elimu ndio tatizo ila nawaombea tuelemishane zaidi kihoja kama member wangu ulivyofanya thank u
 
CHINA INA HISTORIA ZAIDI YA MIAKA 5000, KUNA EMPERORS, TANG, QIN, ZHOU, NA DYNASTIES KIBAO! NA WACHINA WANAJIVUNIA SANA HISTORIA YAO HIYO, CHINA ISHAKUWA SUPERPOWER MIAKA MAELFU KABLA YA HUYO SUN-YAT-SEN.

SASA UNAPOKUJA NA HOJA ETI, UBABA WA TAIFA NI WA MILELE NA MTU AKISHAUPATA HAUMPONYOKI, WACHINA WATAKUCHEKA.

WACHINA WAO WAMECHARACTIZE HISTORIA YAO KATIKA (1) ANCIENT CHINA (2) MODERN CHINA, AKINA SUN-YAT-SEN ARE FATHERS OF MODERN CHINA, NA EMPERROR KAMA Qin Shi Huang( FIRST Emperror) Ni father of Ancient China. SASA SWALI KWAKO NI JE KWA MUJIBU WA HOJA YAKO YA "UBABA WA TAIFA MTU AKIISHAUPATA HAUBADIRIKI" WEWE UNAONA FATHER WA CHINA NI NANI KATI YA HAO WAWILI?.

TUKIACHANA NA YOTE HAYO BWANA MCHAMBUZI, WEWE UMELIHUSISHA SUALA LA HESHIMA YA UBABA WA TAIFA KUWA LA KISHERIA, UKISHINDWA KUTHIBITISHA HILI, MUOMBE MOD AONDOE HII THREAD, KWA SABABU ITAKUWA IMEJENGWA KATIKA FLAWED PREMISES NA WRONG ARGUMENTATION PRINCIPLE!.

PIA NAOMBA UJENGE CASE VIZURI YA KWA NINI MWALIMU NYERERE APEWE HESHIMA YA UBABA WA TAIFA "PEKE YAKE", SO FAR ULICHOKIELEZEA KATIKA MADA YAKO NI SIFA NYINGI SANA ZA GEORGE WASHINGTON NA SI ZA MWALIMU, THEN UKACONCLUDE BY "ASSOCIATION" KWAMBA THEREFORE MWALIMU NDO AWE BABA WA TAIFA "PEKE YAKE".

WEKA POINT ZAKO MCHAMBUZI, KWA NINI NYERERE AWE BABA WA TAIFA LA TANZANIA NA SI KARUME SENIOR?(MAANA MIMI NA WEWE TUNAKUBALIANA KWAMBA KUWA RAISI WA KWANZA SI KIGEZO CHA KUWA BABA WA TAIFA, TUKATOLEA MFANO WA MAHTMA GANDHI WA INDIA)
NATAKA a,b,c,d THEN TUTAZICHAMBUA HIZO POINTI, NA PIA USISAHAU KUTULETEA SHERIA INAYOSEMA KWAMBA NYERERE NI BABA WA TAIFA KAMA ULIVYOSEMA KWAMBA IPO.
 
Magonjwa ya asili haya. Vipi kule uchina ambapo imani ya kikiristo na ukatoliki ni uhaini? Je hawaiti Baba wa taifa?
 
Hayo yote unaotetea yanakwenda kinyume na mafundisho ya Uislaam. Hakuna baba zaidi ya baba yako aliyekuzaa. Huo mwingine wote ni Ukatoliki.
Nikikuita Mama FaizaFoxy hautaitika. Huku kungine kuna Mama Maria Nyerre, Mama Salma Kikwete,...DINI yako inaruhusu kuwaita hivi hawa?
 
Aliyakuta zaidi ya hayo, usitujaze ujinga kuwa kayaleta yeye, neno "Sheikh" kiarabu ni kama Kiswahili "Mzee" kwa hiyo ukisikia mtu anaitwa Sheikh Nyerere wala usishangae. Ni simply imemaanishwa Mzee Nyerere, lakini si "baba". NO.
Unataka kutuambia na kale katoto kalikokuwa kanafanya "miujiza" kakaitwa Sheikh Sharifu mlikuwa mnamaanisha Mzee Sharifu?
 
Hatutaki heshima za Kikatoliki, hukohuko kanisani, huo ndio udini wenyewe, kwanini mlazimishe kitu ambacho kinawaudhi wengine?
Mbona wale wazee Ustaadh wapigania uhuru maarufu waliona na ku-surrender na kumpa uongozi na urais kafiri yule Julius Kambarage Nyerere? unaakili fupi kweli wewe. zimejaa ma-biases!!!!
 

Mwandishi ameelezea utofauti kati ya Baba na Rais bora wa Taifa,kila mtu ameelewa,labda kama mtu hakubali. Halafu ameonyesha kuwa asili ya ubaba wa taifa ama jina hilo haikutokea kanisa katoliki wala si Roma wanaotoa jina hilo kwa viongozi wa nchi hapa duniani,iwe za kiislamu au kikristo. Hata hatukuwahi kusikia aliyetoa jina hilo alikuwa kardinali Rugambwa au Pengo! Mi nadhani imechukuliwa kifamilia zaidi kwamba...kiongozi wa familia huwa ni mwanamume. Na kwa bahati ni kwamba wanaharakati wengi katika ukombozi na mapinduzi ya nchi zao,walikuwa wanaume... Kifamilia kuna mambo ambayo hayakamiliki hadi baba aje.. Heshima ya ubaba,ni kuonesha uongozi,msimamo,ujasiri,vision,na maamuzi ambayo hata kama yatapingwa na watoto au wake zake,ya baba yanakuwa ya mwisho.. Someone can correct me ila huo ndiyo ufahamu wangu.
 
Kwanza kabisa napenda kumpongeza mwandishi kwa kuwa jasiri wa kutoa hisia zake bila woga. Hisia zilizojikita zaidi katika itikadi yake ya chama. Lakini amekuwa mwalimu zaidi badala ya kuwa mwenye kujadili. Amejitahidi sana kuonyesha heshima zinapatikanaje. Tumemuelewa.Lakini wakati unaanzisha mada kama hii lazima ufahamu kuwa wapo watu wanaomfahamu zaidi Julius Kambarage Nyerere kuliko wewe. Nina maana waliotawaliwa na Nyerere wakiwa watu wazima, wakfanya kazi naye na wakaonja matamu na machungu ya utawala wake. watu hao wakipewa uhuru wakueleza hisia zao naona wanaweza kukamatwa Haitoshi kutafuta uhuru ikawa tiketi ya kupewa heshima milele. Naomba nimjuze mwandishi kuwa mada yako inaweza ikahamasisha watu wakatoa michango ambayo badala ya kujenga heshima ya Nyerere ikamshusha zaidi sijui kama hili nalo uliliangali kabla hujaamua kuandika. kwa sababu mwandishi amekuwa wazi ni vema akatujuza hicho cheo cha baba wa taifa alipewa na nani wapi na kwa utaratibu upi. Siku nyingine usijaribu kuwashawishi watu waamini kile unachoamini wewe na kudai wanaotoa maoni wasiachiwe kutoa maoni. kama kuna mpotoshaji ambaye ameandika kabla ya kuijua historia ya Tanzania basi ni wewe.
 
Mchambuzi, I have just read this article from the Economist (Bonyeza hapa) na nipofika kwenye hizi para nikakumbuka maandishi yako. Kudos mkuu!!!!!






Anywayz anachokielezea mwandishi hapo juu ni kwamba pamoja na madhila na mapungufu ya hao aliowataja bado wanabaki kuwa the founding fathers.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…