Aah..kula nguruwe ni matusi, ww vp? Nguruwe ni kama samaki anasaidia kuongeza uwezo wa kufikiri na kupambanua mambo bila upendeleo, unafiki au chuki binafsi ambalo hilo ndo tatizo lako. Sasa ukianza kula nguruwe atakusaidia kutibu huo ugonjwa wako!
Huoni hata haya kusema sabuni zilipatikana? labda Arita. Umasikini wakati wa nyeyere inaonesha hukuuona wewe, wote makata mbuga. vijijini makaniki mtindo mmoja, mjini ma krimplini. Kula unakimbiza gari litashusha duka gani tena hujui ni nini kitashushwa. Magari mafuta foleni, jumapili hakuna ruksa magari kutembea. Dhiki mtindo mmoja, kutoa chakula mkoa mmoja kupeleka mwingine marufuku, mageti eti ya kipindupindu. Dahhh, wadanganye wasio yaona. Niliyaona.
Unatuuliza sisi tena??
Mimi sijawahi kumuita, sintamuita wala watoto hawatawezi kumuita nikiwa hai!
Kwa ufupi hawezi kuwa baba labda huko kwenu..
Ustaadh salam aleykum?
Hukulazimishwa ndugu hata Hayati Julius Nyerere yote sawa tu; vipi jibu langu la Somalia unalo?
Chama
Gongo la Mboto DSM
Akili zenyewe ndio hizo mnakatazwa kuzaa halafu mnaitwa baba. Huko huko kanisani.
Mama Faiza Foxy hivi huna hata jirani mmoja wa kikatoliki hapo mtaani kwako? Sumu ya UDINI imekupanda lakini tahadhari Barubaru si mwenzetu likitokea anapo pa kukimbilia hata kauli zake zinajionyesha wazi mfano wakati tunapomzungumza Raisi mh. Kikwete na nchi yetu yeye hutumia kauli hizi, "Raisi wenu", "nchi yenu" huyu bwana muangalie kwa mapana na marefu.
Chama
Gongo la Mboto DSM
Shida ipi ulionayo? Tukusaidie japo ki mawazo maana hiyo ndio shida kubwa ya Watanzania. Mafursa yaliyojaa haya halafu mtu analia shida. Unachekesha!
Wewe una udini kwa faizy tu, huoni akifanya wengine siwapendi wanafiki
Gerezani ni USA? au sio?
Hata wewe si nilishakuambia mdini
Chama
Gongo la Mboto DSM.
Gerezani ni USA? au sio?
Na wewe unashida tukusaidie?
Mwanakijiji mkuu wangu hapa unakosea kabisa kwa sababu Ismail ni mtoto wa kuzaliwa na Ibrahim, hivyo kumwita baba inaswihi na hata hayo uloyasoma yanazungumzia baba zao kweli wa uzazi na sio mtu yeyote..Kuna watu wamejenga hoja ya kidini kuwa "katika Uislamu hakuna baba". Hii si kweli hata kidogo. Qurani Tukufu yenyewe inaweka wazi jambo hili kwamba wapo wanaoitwa "baba" kati ya wanadamu na tena ni waamini. Katika Surat Affat (37:102 na kuendelea) tunaona kuwa Ishmaeli anamuita Ibrahim "Baba". Waislamu wanaamini kuwa Mitume wote hata kabla ya Mohammed (SAW) walikuwa ni Waislamu. Kuwa hata Ibrahim alikuwa ni Muislamu. Kwa hiyo kama ni kweli hivi (Italiki na Msisitizo mweuzi wangu)
Basi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanao subiri (37:102)
Na katika sura hiyo hiyo Qurani inawasifia manabii wengine waliotangulia na inapofika kwa Nabii Ilyas (Elia) inasemwa hivi:
NaA hakika Ilyas bila ya shaka alikuwa miongoni mwa Mitume
lipo waambia watu wake: Hamwogopi?
Mnamwomba Baa'li na mnamwacha Mbora wa waumbaji
Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa zamani? 37:123-126
Kitu pekee ambacho kiko wazi katika Qurani na katika mafundisho ya Uislamu ni kuwa Mungu si Baba. Ukisoma mistari inayofuatia hapo chini hili liko wazi kabisa. Na kwa wanaosoma historia ya dini ni kuwa Uislamu umekataa kabisa toka mwanzo Kumuita Mungu "Baba" kwa sababu Wakristu walikuwa wanamuita Mungu "Baba" na iliaminika kana kwamba wanamaanisha Mungu alichukua mke akazaa naye. Hili Qurani Tukufu inalikataa hata kwenye sura hii:
Ati ni kwa uzushi wao ndio wanasema
Mwenyezi Mungu amezaa! Ama hakika bila ya shaka hao ni waongo!
Ati amekhiari watoto wa kike kuliko wanaume? 37:151-153
Pia tunaona katika Sura 33:6 kuwa wake wa Mtume ni "mama wa waamini" na ndio maana hata leo Waislamu wanamuona Bi. Khadijah kama "mama yao". Je, kama mke wa nabii (kama mstari unavyosema) ni "mama" wa waumini je nabii mwenyewe anaweza kuchukuliwaje? Hasa ukizingatia kuwa Qurani inawatambulisha wale manabii wa zamani (hiyo sura ya 37) kuwa ni "baba" wa zamani? Je manabii nao ni kama baba zetu?
Kumbe ni rahisi kuona kuwa:
a. Uislamu unatambua nafasi ya "ubaba" na kuwa haikatazi kumuita mtu "baba". Katika Biblia labda ni kali zaidi kwa sababu Yesu ndiye alisema wazi kuwa "Usimwite mtu yeyote baba hapa duniani kwani baba yenu ni mmoja tu aliye mbinguni!" Mathayo 23:9.
b. Uislamu unakataza kumuita Mungu "Baba" kwa sababu Mungu "hakuzaa wala hakuzaliwa". Na ni kinyume na mafundisho yaliyokuwepo ya Wakristu waliomuita Mungu "Baba yetu".
c. Kama ndivyo ilivyo kwamba Qurani inawatambulisha mitume waliotangulia kama "baba" ni wazi kuwa haikatazwi kumuita mtu "baba" moja kwa moja; inakataza kumuita Mungu "baba". Na tunafahamu inaposema wake wa nabii ni "mama" wa waamini sidhani kama kuna mtu anaamini kwamba inasema huyo "mama" alizaa waamini wote kimwili. Ni wazi ni cheo na nafasi ya heshima ambayo mama hao wanazo. Hili ni kweli pia kwa wale manabii. Wanapoitwa "baba" zetu si kwa sababu waliwaingilia mama zetu!
Hivyo, hoja ya kuwa Nyerere hafai kuitwa 'baba' haina msingi na kuwa mtu aliyezaa asiitwe 'baba' nayo haina msingi vile vile!
Nasimama kusahihishwa.
Mwanakijiji mkuu wangu hapa unakosea kabisa kwa sababu Ismail ni mtoto wa kuzaliwa na Ibrahim, hivyo kumwita baba inaswihi na hata hayo uloyasoma yanazungumzia baba zao kweli wa uzazi na sio mtu yeyote..
Waloyasema FaizaFoxy na Topical kuhusu Uislaam ni kweli na huwezi kumwita mtu yeyote baba kwa sababu hatuna titles za utaifa zaidi ya Utukufu kwa mwenyezi Mungu. Hivyo neno Baba lina maana yake na haliwezi kutumika hovyo..
Na katika utaratibu wa Kikristu ndio unakuta neno baba linatumika popote kwa sababu ukiristu na tawala vinafunagamana ktk mambo mengi sana. Na ndio maama mimi huwa sina tatizo mnaposema Yesu ni mtoto wa Mungu ikiwa ni ktk tafsiri zetu maana Padre huitwa Baba na mwanamke huitwa Sister. Mungu akiitwa Lord na Yesu pia hivyo ni hadi mtu ajue vizuri matumizi ya maneno haya ktk Ukristu ndio anaweza kuzungumza..
Kifupi kuvunja ubishani huu, kuwa mwarabu ama kutumia kiarabu haina maana ndio Uislaam, wapo waarabu wengi sana ambao sii waislaaam kama kiswahili ukisema - Mungu mkubwa haikufanyi wewe uwe mkristu. Waarabu kwa asili wanaita baba wa Taifa lakini haina maana ndio Uislaam kwa sababu huyo huyo mwarabu muislaam baba yake wa kambo hatamwita baba..Huu ni mchanganyiko wa culture na dini lakini hakuna kitu baba kwa mtu ambaye sii mzazi wako wa kiume.
Jihabari reefu, kuandika kooote huko unataka tumuite Nyerere "baba"? Unanchekesha, huo ni ukatoliki. Hata Kikwete sijamsikia akimuita hivyo Nyerere. Upelekeni ubaba kanisani, huku wananchi tuwacheni tumuite Mwalim Nyerere.
Hakuna Muislaam anaefata Uislaam wake atathubutu kumuita Nyerere baba, labda wale mnakutana kwenye mabaa.
This is really sad! Eti hata kikwete hujamsikia akimuita hivyo Nyerere! Kweli we should never underestimate the predictability of stupidity!
Hayo wala sina tatizo nayo, hayo ni "by the way" mimi nipo kwenye u "baba" tu.
Baba Mtakatifu, Baba Askofu, Baba Mchungaji wakondoo, na sasa mnataka kutubambikia "baba" wa Taifa. Kama si udini ni nini? Pelekeni u baba wenu kanisani huku mitaani Muacheni nyerere abaki kuwa Rais wa Kwanza wa JMT.
Nani alokwambia kikwete ni uislam ndugu??
Uislamu ni zaidi ya kikwete