Nyerere, Mwinyi, Mkapa and Kikwete: Leadership Styles and A Lesson to Learn!

Msitafute mchawi wa Tanganyika.

waarabu tuna usemi "" In order to build something strong, it helps to start with best and possible materials.""

Sasa siku zote misingi mibovu huzaa nyumba mbovu. Na kwa Tz ni Nyerere aliweka misingi mibovu sana ya uchumi na kuimarisha siasa.

Sasa ndio kinawasibu. Ni wazuri kisiasa lakin wabovu sana kiuchumi.

msitafute mchawi. Mchawi wenu ni Nyerere.
 
Kuacha mambo yote..at least Mkapa alikuwa makini siyo kama mambo yalivyo sasa..inafikia hata raisi kuwekewa mafuta yaliyochakachuliwa, umakini umepungua sana kwa JK ukilinganisha na Ben.
 
1. MWINYI ALIPEWA NCHI BAADA YA MWALIMU NYERERE KUMSHINDA. Huyu mzee wa watu alijitahidi. Rejea hotuba yake aliongea Stalight Hotel Kuwajibu KKT, WALIPOSEMA NCHI INANUKA, IMEJAA RUSHWA.

2. MKAPA AMEINGIZA NCHI KATIKA MIKATABA YA KIJINGA. Tumeuza Madini Yetu kwa bei ya kutupwa. Usisahau EPA.

3. KIKWETE IS TOO DEMOCRATIC.

NOW JUDGE FOR YOURSELF.
 
Nadhani hata mtoto aliyezaliwa leo anajua Jk hana hata sifa yakuwa kiongozi ma hawezi
 
Nyerere ni muasisi wa Ufisadi Tz.

yeye aliasisi ulanguzi na ubadhilifu wa mali za umma kitu ambacho kilikuwa hakimo kabisa miongoni mwa waTz kabla ya uhuru wenu.

Kukomaa kwa ulanguzi na ubadhilifu wa mali za umma ndiko kumezaa siku hizi Ufisadi.
 
Baada ya Nyerere tumeongozwa na watu ambao uwezo wao walistahili kuwa wabunge ktk majimbo madogo madogo kama ya uchaguzi ya Zanzibar na Pemba! Matokeo ya uongozi wao mbovu tunavuna sasa,umasikini,udini,ukabila,ukanda,nk
 
Baada ya Nyerere tumeongozwa na watu ambao uwezo wao walistahili kuwa wabunge ktk majimbo madogo madogo kama ya uchaguzi ya Zanzibar na Pemba! Matokeo ya uongozi wao mbovu tunavuna sasa,umasikini,udini,ukabila,ukanda,nk

Na mkichagua Padre na chama chake basi hazo ndio sera zao.
 
Mkapa kwa kweli...natamani katiba ingeruhusu agombee tena
 
Kila rais wa nchi hii ana mazuri aliyoifanyia nchi yake ktk session yake,hii ni kutokana na lengo hasa la mtu kugombea u rais kwa lengo la kusaidia nchi yako iweze ku achieve aspects fulani socially,economically etc.

Ila kila mmoja ana weakness zake kinachowatofautisha ni kutokana na aina gani na extent ya udhaifu,let say awamu ya sasa wasaidizi walioko kwenye position za chini ya rais wanakuwa very free kujifanyia mambo yao especially mis use of public resources na hakuna wa kuwakemea, nchi inafanywa kama shamba la bibi, ila tofauti na enzi za mwalimu, mzee kifimbo alikua final, no one could dare to temper with the authority of president.

Awamu ya BWM ilikuwa na mazuri mengi bt iliwekwa doa na most of investment deals.

Yote kwa yote awamu hii inaonekana iko kwenye position ngumu kuliko zote with lots of challenges misuse of funds, maamuzi ya kukurupuka, baadhi ya viongozi kuwa ''miungu wadogo'' etc.

Labda ukitaka kujua trend ya awamu hii angalia namna ambavyo watawala wanavyo solve emerging issues ndo utajua where are we going.
 
viwanda alivyobakisha vinafanana sana na shule za kata! Kwani unahitaji orodha ya shule za kata kujua ujinga unazidi kupiga kambi? Mwalimu aliacha National milling je unga wa ugali ilikuaje utoke US,viwanda vya nguo ilikuaje watu wavae kamanyora nchi nzima kama uniform,hujui sukari haikupatikana hata kwa wenye fedha?unajua kuwa vifaa muhimu kama fridge,tv, ilikuwa uhujum uchum? Unajua kuwa miji haikui kwa kusomba watu na kujaza sehem moja?jifunze factors for growth of towns then untajie miji ipi ilikuzwa kwa kukusanya watu kibabe?mwalimu alikuwa mzalendo bt ubishi wake ndo umetufikisha hapa!angemsikiliza christopher kasanga tumbo,kaselabantu na Oscar kambona tusingekuwa hapa. 1967 kambona alisema ujamaa wa nyerere utakufa,kamuulize mama maria anakumbuka ushauri wa kambona!
 
Nyerere ndo kilaza namba moja kwa kutuletea vilaza wenzie Mwinyi na mkapa.
 
tuangalie pale tulipojikwaa siyo pale ambapo tumeangukia,ukizungumzia kikwete tutakuwa tumemwonea,mfano suala la umeme ni mipango mibovu ya waliomtangulia,twende kwa madaktari bd tatizo la kuwarekebishia mafao yao ungeenda kwa awamu sasa wangekuwa mbali kwa ufupi miye nasema na mwenyezi mungu amrehemu tatizo tunaanzia na kwa baba nyerere
 
Mwl. Nyerere aliongoza nchi hii akijua utajiri ilionao (ardhi, madini, mito, maziwa na bahari). Mwl. aliongoza kizaz kilichokuwa DUNI kielimu lakini hakuthubutu kuzitumia hizo kwa ubadhirifu. Angeweza kuzitumia mali hizo kwa kujinufaisha yeye mwenyewe na familia yake tena bila kuulizwa na yeyote, lakini kwa kuwa alikuwa na upeo na hakupenda kujilimbikizia mali, aliweka msimamo mkali juu ya matumizi ya utajiri huo. Aliwahoji wate alioingiwa na wasiwasi nao juu ya utajiri wao. Mwl aliipenda nchi na watu wake. alikuwa tayari kula muhogo kwa dagaa akiwa ikuru lakini raslimal za watanzania zibaki zikiwa salama kwa kizazi cha baadae. Alikuwa na mke pia watoto lakini hakuna aliyetumia kivul cha ikuru kujinufaisha. Familia ya Mwl mpaka leo wanaishi maisha ya kawaida na wameridhika na kile walichokipata.

Tofauti na Mwl; mkapa na kikwete hawana upeo kwa kizaz cha kesho. Keki ya TAIFA wamejimilikisha wenyewe pamoja na maswahiba wao, Majumba makubwa kwao na swahiba wao ni kawaida, migodi na mashirika ya umeme wanajigawia kwa migongo ya watu wa nje, viwanja hasa mijini wamejimilikisha wenyewe na familia zenu (arusha, mosh, chalinz, dar) bei za mafuta ya taa na petrol zinapanda kila kukicha huku pembeni utawakuta wao wenyewe wakimilik shelly kubwa za mafuta.
Familia zao zinamiliki mahotel makubwa na nyumba za mikutano. Wanaingia ubia na serikal kupitia migongo ya watu wengine kumbe ni wao wenyewe wanao lifirisi taifa, wezi wa keki ya watanzaia wote. Familia zao wameziweka mbele kumfikilia masikini aliyeko KAISHO-KARAGWE akiteseka na bei mbovu za kahawa, wizi wa mifugo na ukame unaolikumba taifa. Familia zinatumia mgongo wa ikuru kufanikisha mambo yao km. kupata viwanja, kujenga mahotel nk.

Taifa letu linapelekwa pelekwa tu kama meli isiyo na nahodha. Kila wanalo ongea nafsi zao zinawasuta na kuwa aibu kwao. Hii ni dhahiri kuwa yote mliyofanya/mnayofanya hayaendani na mapenzi ya MUNGU na ndio maana mnaaibika na kuaibishwa ingali bado mnaingoza nchi. Mungu anawafanyia kile alichomfanyia Sauli kwa Kumwonesha mfalme mpya angali bado anapenda kuendelea kutawala. Niwapi wanaweza kwenda wakaongea kauli yao ya "NGUVU MPYA, HARI MPYA NA KASI MPYAS?" au "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA"

Nawashauri hiyo kauli ya mwisho, waibadilishe na kila wanapoongea na mihadhara waseme
"NGUVU NA KASI YA KULIIBIA TAIFA" pia "MAISHA BORA KWA KILA FISADI NA MBADHIRIFU WA MALI YA UMMA"

Naomba kuwasilisha
 
Mwalimu Nyerere alikuwa mzalendo mwenye uchungu na nchi yake ndio maana haakutumia nafasi aliyopewa kunufaisha familia yake
Aliwapenda waafrika na kuwakemea wazungu ambao siku zote walijiona bora kuliko watu weusi
Alichukia rushwa na unafiki siku zote alikuwa mkweli
Ukiacha kambona aliyetoa shutuma ambazo hakuthibitisha mpaka leo hakuna mtu aliyekuja na kumtuhumu wizi wa mali ya umma
Hakuwa na urafiki na viongozi wezi na wabadhilifu wa mali za umma
Alipenda kushindana kwa hoja
kwa hayo machache jaribu kuwalinganisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom