Mkuu Mwanafalsafa,
Kuna giza totoro la ufahamu wa kiroho katika kanisa katoliki. Biblia hawaifuati wao wameamua kufanya kama waonavyo kuwa ni vyema machoni pao. Ndo maana YESU anasema;
Marko 7: 6-8
6Akawaambia (YESU), watu hawa huniheshimu kwa midomo, ila mioyo yao iko mbali nami 7Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu, 8 Ninyi mwaiacha amri ya MUNGU, na kuyashika mapokeo ya wanadamu.
Kuhusu kuombewa na waliokufa Bibilia inasemaje?
Mhubiri 9:5-6
5Kwa sababu waliohai wanajua ya kwamba watakufa, lakini wafu hawajui neno lolote, wala hawana ijara tena, maana kumbukumbu lao limesahauliwa. 6Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao imepotea yote pamoja, wala hawana sehemu tena katika jambo lolote linalofanyika chini ya jua
Nani mwombezi wetu?
Waebrania 7:25
25Naye (YESU) kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai siku zote ili awaombee
Je zaidi ya YESU kutuombea tunahitaji intermediate person called saint? The answer is no.
Waebrania 10:19-22
19Basi ndugu kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, 20 njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani mwili wake, 21na kuwa na kuhani mkuu juu ya nyumba ya MUNGU 22na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya; tumeoshwa miili kwa maji safi.
MUNGU awasaidie macho yao ya rohoni yatiwe nuru wapate kuona.
__________________
Mzalendo halisi hufanya biashara zake kwa uwazi na kulipa kodi kwa usahihi