ASANTE Bw. Huduma kwa sifa zote hizo. Kwa jina kweli nafanana na
Babu lakini siwezi uwanasiasa mie katika miaka hii. Kwanza, sio
mbinafsi; pili sitaki kuneemesha mke na watoto wangu kwa fedha
zinazowapora wananchi; ufisadi siujui nausikia tu; sijui kuficha
ukweli nikasema uongo ndio kweli; sijui kutoa ahadi za uongo; sijui
kukariri biblia wakati natakiwa kunukuu Msahafu; sivumilii
kuwapelekea Waancholi na Wanchoka kifaru cha pilipili badala ya
kuwaletea siasa za kuwaunganisha na kuwafanya wajione ndugu kwa
maendeleo ya Tarime na mkoa wa Mara kwa ujumla.
Wanasiasa wote wanafiki lakini unafiki huzidiana. Ila kwa hakika
chama tawala nijinafiki babu K!
Tuachilie hayo mbali. Umeniuliza tumuenzi vipi hayati Baba wa Taifa
katika siku au wiki kama moja hivi ijayo.
Yapo mengi Huduma ya kumuenzi baba wa Taifa. Na baadhi yake:
i) Kwanza ni CCM kukiri kwa ulimi na moyo kuwa wanaipeleka pabaya
nchi ambayo kama Mzee angelikuwa hai leo isingediriki kufuata njia
hiyo.
ii. Pili chama hicho kiengue watu waliopewa nyadhifa ambazo
hawaziwezi na ama wanamshauri mwenyekiti au chama vibaya.
iii. CCM isifisadi tu na kupeleka kwenye matumbo yao bali pia
wawekeze kwenye Nyerere Foundation sasa walijitia unafiki wa nini
kama hawawezi kuisadia. Eti na kila anayeula anataka naye akiondoka
madarakani aanzishiwe Foundation yake. Hivi kweli wote nyie, ila
Mwinyi, hamjui kuwa mnajifananisha na mlima na nyie ni vichuguu.
Kweli hamu inaweza kuwepo moyoni ya kumpiku lakini hamna mlilolifanya
hadi wa leo la kuonesha mmekaribia hata kuwa kichuguu kikubwa! Nyie
wote ni waigizaji na wasanii, mmekuja, mnakuja, mtaondoka na
mtatuacha vilevile kwa kuwa sio watu wa fikira, hekima na busara
jambo ambalo kama kuwa mkubwa pia ni neema na baraka za Muumba kwa
amtakaye. Na hili haliji bila kumgeukia kwanza huyo aliyekuumba.
iv. Utu- hakuna anayejali tena utu wa mwingine katika nchi hii
kuanzia juu hadi chini. Hivi kwanini enzi za Nyerere tulikuwa
wastaabu na leo washenzi?
v) Usawa-Babu alipigana sana kuhakikisha tofauti ya kipato kati yetu
haiwi kubwa kiasi cha kutisha hivi. Matokeo yake sasa baada ya soko
huru la uraruaji wa mali ya umma na mali asili kuna wanaopata
kupindukia kiasi cha kufia kwenye mabichi kila wiki wakijaribu
kufyeka mabinti wanne au watano kwa siku. Tuangalie hili la
kudanganywa na mishahara ya kikoloni tukidhani eti tutaendelea kwa
kuwalipa walimu, madaktari, manesi, wahandisi, askari na kadhalika
mishahara ambayo haikidhi mahitaji yao ya kila leo. Kama ndivyo mbona
kwa miaka 50 hatujaendelea. Au tunaingia 50 nyingine! Naam, mishahara
mizuri kweli itakuja tukiwa kaburini lakini ndio hivyo basi wajemeni?
vi) Kujitegemea- inatia aibu kuona kwamba vitu tunavyoweza kufanya
sisi wenyewe bado tunatembeza bakuli hadi Marekani na Uingereza
[waliotuingiza katika hali tuliyo nayo] na kusahau kuwa kuna nchi
zenye nia na dhati ya kweli kutusaidia sisi na sio hao
tunaowalimbukia. Lakini ndio hivyo tumezoea kupewa samaki na kila
siku tutaendelea kurudi Marekani.
viii) Kujilimbikizia-sasa hivi hakuna mwenye siasa au mwelekeo wa
kumsaidia mwananchi bali ni mbio za ufahari kutaka huyu kumshinda
huyu kwa nyumba kubwa zaidi, gari kubwa zaidi, akiba nono zaidi
benki, watoto kwenda nje na wasisome shule za walahoi na waliwakodi.
ix) Siasa safi-tunahitji hili ili tuendelee liko wapi? Hebu katika
Nyerere day tujiulize- Kasi Mpya, Nguvu Mpya na Ari Mpya vimeishia
wapi?
x) Uongozi bora nao pia- hivi Kila waziri ana Visheni na Misheni ya
Wizara yake? Anajua anakotaka kweli kuipeleka sekta yake. Nini
mipango yao, nini mikakati yao na nini malengo yao kila baada ya
miezi mitatu, nusu mwaka, mwaka mmoja. Au wapowapo tu kwenye
heyakondisheni wakipoozwa maka.....(Malizia Makengeza)...... maana
iwe ni kukarabati njia mpaka Nani aseme, ....shule mpaka Bwamkubwa
aseme, .......kufufua michezo na ushindani nchini, ........mpaka Nani
aseme......usafi na mabustani na magadeni na maviwanja ya watoto wetu
wanaogongwa kwa kucheza barabarani.... au kufia kwenye disko bubu
zisizoizinishwa.... mpaka Nani aseme.......Kilimo na kuwawezesha
wakulima vijana......yuko Wapi waziri jina wa Vijana?
Haya, jamani, hawa ndio mawaziri wenu na wanamaliza miaka mitano na
huku walikotoka hatujaona walichokifanya japo kuna mapipa ya taka
hapa yamejaa ahadi tupu.
Naomba radhi kwa jazba na kuandika kitu kirefu kuliko nilivyotarajia.
Ni matumaini yangu hata hivyo, Ndugu yangu, Mwenzangu, Mlalahoi
mwenzangu Bw. Huduma huko visiwani uko nami na umenielewa natamani
kungelikuwa na Mtanganyika kama wewe Mzanzibari mwenye mapenzi ya
kweli na Mwalimu kama ulivyo wewe. Lakini simuoni. Hata kina Mzee
Mwanakijiji naona wamekwishatekwa na Greencard na siasa zinazojua
kutumia tu bila ya kuingiza kwa halali. Zitatupeleka wapi. Wakati
umefika kujiuliza tushirikiane na Mashariki au tuendelee kuwa