NYERERE DAY: Mwalimu Jr. uko wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NYERERE DAY: Mwalimu Jr. uko wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Huduma, Oct 7, 2008.

 1. H

  Huduma Member

  #1
  Oct 7, 2008
  Joined: Jan 26, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NINAMFUATILIA kwa karibu sana Mwalimu Jr. na kwa hakika naona kama vile mawazo yake ni ya Al-Marhum baba wa Taifa, Mwalimu J. K. Nyerere wajina wake.

  Tueleze basi mwalimu jr. ni njia ipi ya kusherehekea Nyerere Day kwa namna ambayo si ya unafiki na kula hela za walipa kodi kwa kuweka matangazo yanayolipiwa mara mbili au tatu ya bei ya kweli ya kazi kama hizo?

  Tunakusubiri kwa hamu Mwalimu Jr.

  huduma,
  zanzibar
   
 2. Z

  Zanaki JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2008
  Joined: Sep 1, 2006
  Messages: 544
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Al Marhum ndio nani?
   
 3. Iteitei Lya Kitee

  Iteitei Lya Kitee JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2008
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 589
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  ZANAKI, AL MARHUM maana yake ni marehem kwa kiarabu kama sijakosea,hayati.
   
 4. Iteitei Lya Kitee

  Iteitei Lya Kitee JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2008
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 589
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  AL MARHUM ni marehemu kwa kiarabu ZANAKI
   
 5. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Sorry and who is malimu jr?
   
 6. m

  mwalimu Jr. Member

  #6
  Oct 7, 2008
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  ASANTE Bw. Huduma kwa sifa zote hizo. Kwa jina kweli nafanana na
  Babu lakini siwezi uwanasiasa mie katika miaka hii. Kwanza, sio
  mbinafsi; pili sitaki kuneemesha mke na watoto wangu kwa fedha
  zinazowapora wananchi; ufisadi siujui nausikia tu; sijui kuficha
  ukweli nikasema uongo ndio kweli; sijui kutoa ahadi za uongo; sijui
  kukariri biblia wakati natakiwa kunukuu Msahafu; sivumilii
  kuwapelekea Waancholi na Wanchoka kifaru cha pilipili badala ya
  kuwaletea siasa za kuwaunganisha na kuwafanya wajione ndugu kwa
  maendeleo ya Tarime na mkoa wa Mara kwa ujumla.


  Wanasiasa wote wanafiki lakini unafiki huzidiana. Ila kwa hakika
  chama tawala nijinafiki babu K!

  Tuachilie hayo mbali. Umeniuliza tumuenzi vipi hayati Baba wa Taifa
  katika siku au wiki kama moja hivi ijayo.

  Yapo mengi Huduma ya kumuenzi baba wa Taifa. Na baadhi yake:

  i) Kwanza ni CCM kukiri kwa ulimi na moyo kuwa wanaipeleka pabaya
  nchi ambayo kama Mzee angelikuwa hai leo isingediriki kufuata njia
  hiyo.
  ii. Pili chama hicho kiengue watu waliopewa nyadhifa ambazo
  hawaziwezi na ama wanamshauri mwenyekiti au chama vibaya.
  iii. CCM isifisadi tu na kupeleka kwenye matumbo yao bali pia
  wawekeze kwenye Nyerere Foundation sasa walijitia unafiki wa nini
  kama hawawezi kuisadia. Eti na kila anayeula anataka naye akiondoka
  madarakani aanzishiwe Foundation yake. Hivi kweli wote nyie, ila
  Mwinyi, hamjui kuwa mnajifananisha na mlima na nyie ni vichuguu.
  Kweli hamu inaweza kuwepo moyoni ya kumpiku lakini hamna mlilolifanya
  hadi wa leo la kuonesha mmekaribia hata kuwa kichuguu kikubwa! Nyie
  wote ni waigizaji na wasanii, mmekuja, mnakuja, mtaondoka na
  mtatuacha vilevile kwa kuwa sio watu wa fikira, hekima na busara
  jambo ambalo kama kuwa mkubwa pia ni neema na baraka za Muumba kwa
  amtakaye. Na hili haliji bila kumgeukia kwanza huyo aliyekuumba.
  iv. Utu- hakuna anayejali tena utu wa mwingine katika nchi hii
  kuanzia juu hadi chini. Hivi kwanini enzi za Nyerere tulikuwa
  wastaabu na leo washenzi?
  v) Usawa-Babu alipigana sana kuhakikisha tofauti ya kipato kati yetu
  haiwi kubwa kiasi cha kutisha hivi. Matokeo yake sasa baada ya soko
  huru la uraruaji wa mali ya umma na mali asili kuna wanaopata
  kupindukia kiasi cha kufia kwenye mabichi kila wiki wakijaribu
  kufyeka mabinti wanne au watano kwa siku. Tuangalie hili la
  kudanganywa na mishahara ya kikoloni tukidhani eti tutaendelea kwa
  kuwalipa walimu, madaktari, manesi, wahandisi, askari na kadhalika
  mishahara ambayo haikidhi mahitaji yao ya kila leo. Kama ndivyo mbona
  kwa miaka 50 hatujaendelea. Au tunaingia 50 nyingine! Naam, mishahara
  mizuri kweli itakuja tukiwa kaburini lakini ndio hivyo basi wajemeni?
  vi) Kujitegemea- inatia aibu kuona kwamba vitu tunavyoweza kufanya
  sisi wenyewe bado tunatembeza bakuli hadi Marekani na Uingereza
  [waliotuingiza katika hali tuliyo nayo] na kusahau kuwa kuna nchi
  zenye nia na dhati ya kweli kutusaidia sisi na sio hao
  tunaowalimbukia. Lakini ndio hivyo tumezoea kupewa samaki na kila
  siku tutaendelea kurudi Marekani.
  viii) Kujilimbikizia-sasa hivi hakuna mwenye siasa au mwelekeo wa
  kumsaidia mwananchi bali ni mbio za ufahari kutaka huyu kumshinda
  huyu kwa nyumba kubwa zaidi, gari kubwa zaidi, akiba nono zaidi
  benki, watoto kwenda nje na wasisome shule za walahoi na waliwakodi.
  ix) Siasa safi-tunahitji hili ili tuendelee liko wapi? Hebu katika
  Nyerere day tujiulize- Kasi Mpya, Nguvu Mpya na Ari Mpya vimeishia
  wapi?
  x) Uongozi bora nao pia- hivi Kila waziri ana Visheni na Misheni ya
  Wizara yake? Anajua anakotaka kweli kuipeleka sekta yake. Nini
  mipango yao, nini mikakati yao na nini malengo yao kila baada ya
  miezi mitatu, nusu mwaka, mwaka mmoja. Au wapowapo tu kwenye
  heyakondisheni wakipoozwa maka.....(Malizia Makengeza)...... maana
  iwe ni kukarabati njia mpaka Nani aseme, ....shule mpaka Bwamkubwa
  aseme, .......kufufua michezo na ushindani nchini, ........mpaka Nani
  aseme......usafi na mabustani na magadeni na maviwanja ya watoto wetu
  wanaogongwa kwa kucheza barabarani.... au kufia kwenye disko bubu
  zisizoizinishwa.... mpaka Nani aseme.......Kilimo na kuwawezesha
  wakulima vijana......yuko Wapi waziri jina wa Vijana?
  Haya, jamani, hawa ndio mawaziri wenu na wanamaliza miaka mitano na
  huku walikotoka hatujaona walichokifanya japo kuna mapipa ya taka
  hapa yamejaa ahadi tupu.

  Naomba radhi kwa jazba na kuandika kitu kirefu kuliko nilivyotarajia.
  Ni matumaini yangu hata hivyo, Ndugu yangu, Mwenzangu, Mlalahoi
  mwenzangu Bw. Huduma huko visiwani uko nami na umenielewa natamani
  kungelikuwa na Mtanganyika kama wewe Mzanzibari mwenye mapenzi ya
  kweli na Mwalimu kama ulivyo wewe. Lakini simuoni. Hata kina Mzee
  Mwanakijiji naona wamekwishatekwa na Greencard na siasa zinazojua
  kutumia tu bila ya kuingiza kwa halali. Zitatupeleka wapi. Wakati
  umefika kujiuliza tushirikiane na Mashariki au tuendelee kuwa
   
 7. gabyo

  gabyo Member

  #7
  Oct 7, 2008
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We Still Love U Mwalimu!!!!!!!!
   
 8. Z

  Zanaki JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2008
  Joined: Sep 1, 2006
  Messages: 544
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ahsante sana
   
 9. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  salute Mwalimu jr.,
  maneno yako mazito sana mwenye macho na aone na ayatafakari kwa makini hivi ni kweli chombo chetu hakiendi mrama? Tufanyeje ndugu..
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,769
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Kesho ni miaka tisa tangu Mwalimu afariki dunia.
  Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba tumuombee
  ili roho yake ilazwe mahali pema peponi~AMEN
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,769
  Trophy Points: 280
  Mhariri
  Daily News; Monday,October 13, 2008 @20:00

  Leo Watanzania tunatimiza miaka tisa tangu kuondokewa na kiongozi wetu mpendwa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

  Tunasema kiongozi mpendwa kwa sababu tangu alipotangaza kung'atuka katika uongozi wa nchi na baadaye katika Chama Cha Mapinduzi alichokiasisi, bado aliendelea kuwa baba aliyekemea pale alipoona mambo hayaendi vizuri.

  Ni kiongozi mwenye sifa nyingi, lakini kubwa ni ile sifa ya kutopenda makuu. Licha ya madaraka makubwa aliyokuwa nayo, lakini maisha yake yalionekana ya kawaida hivyo kumfanya afanane na wananchi aliowaongoza.

  Ndio sifa inayofanya hadi leo Watanzania tuendelee bado kumkumbuka hasa katika kipindi hiki ambacho macho yetu yanashuhudia maadili katika jamii, wakiwamo viongozi wetu, yakiwa yamemong'onyoka.

  Viongozi wetu wamepotoka na hata zile tambo za kuahidi kumuenzi mwasisi huyo wa taifa ambazo tulizitoa mbele ya jeneza lake na hata kando ya kaburi lake hazionekani na zimetoweka katika matendo yao.

  Leo hii jamii imeshuhudia baadhi ya viongozi wetu na watumishi waandamizi wa umma wakijilimbikizia mali kwa tamaa zao na wengine wamediriki kuiingiza nchi katika mikataba mibovu kwa tamaa na uroho wao wa kutajirika haraka bila kujali athari ambazo taifa litapata.

  Vitendo hivi vya kutia aibu enzi za utawala wa Mwalimu Nyerere hatukuviona na hiyo inatokana na yeye kuipenda nchi yake kwa moyo wake wote na kufanya kila jambo alilofanya atangulize mbele zaidi maslahi ya taifa yake badala ya maslahi binafsi.

  Tunapoadhimisha miaka tisa ya kuondokewa na kiongozi huyu ambaye ameendelea kuwa taa yetu katika kipindi hiki cha giza, tunawasihi viongozi wetu waiangalie taa hii iwaangaze na pale wanapoona hawaendani na mafundisho yake waweze kujirudi.

  Tunaomba wajirudi ili taifa hili changa aliloliasisi miaka 47 iliyopita liweze kupiga hatua kubwa ya maendeleo.Tunataka kuona kwa vitendo wanafunzi hawa wa mwalimu wanavyoipigania nchi yao kama ilivyokuwa kwa mwasisi huyu wa taifa letu, ili ile ndoto yake aliyokuwa nayo ya kuifanya Tanzania iwe moja ya nchi zinazokimbia katika kujiletea maendeleo yake yenyewe iweze kufikiwa.

  Tutafikia hatua hii iwapo viongozi wetu, na sisi wengine wote, tutaacha tamaa na uroho wa kujilimbikizia mali na jamii kuichukia rushwa kama alivyoichukua Mwalimu Nyerere.

  Viongozi waonyeshe njia na tuonekane kweli kuwa sisi ni wanafunzi wake watiifu tuliofundwa kuichukia rushwa na vitendo vingine vyote ambavyo vinachangia kurudisha nyuma maendeleo yetu.
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Malecela: Ufisadi ni ishara ya kumsahau Nyerere

  WAZIRI Mkuu mstaafu John Malecela amesema vitendo vya ufisafi vya baadhi ya viongozi wa umma ni ishara ya kusahau misingi ya uongozi iliyowekwa na Mwalimu Julius Nyerere.

  Katika mahojiano maalumu na HabariLeo kuhusu mustakabali wa Taifa miaka tisa tangu kifo cha Mwalimu Nyerere, Malecela alisema wapo viongozi walioanza kumsahau Mwalimu kwa kukiuka maadili na miiko ya uongozi, lakini akasema hawatafanikiwa katika mipango yao.

  “Nyerere ametuachia nidhamu ya uongozi, aliweka misingi ya viongozi kuwaheshimu wananchi, kuwa waadilifu na waaminifu kwa Taifa lao lakini pia kuwa wazalendo,” alisema Malecela.

  Alisema viongozi wanaodhani kwamba kutokuwapo kwa Mwalimu Nyerere ni mwanya kwao kuwaongoza wananchi bila kuzingatia miiko na misingi ya uongozi, watakumbana na matatizo makubwa. “Hili nalisema wazi, iwe ni ndani ya chama (CCM) au katika serikali, ni lazima matunda ya Uhuru yawanufaishe wananchi wote.

  “Balaa kubwa litatokea kama Watanzania wachache watakuwa matajiri huku wengine wengi wakiwa masikini,” alisema.

  Akizungumzia maadhimisho ya leo ya kifo cha Mwalimu Nyerere, Malecela alisema ingawa Watanzania wanamkumbuka Mwalimu kwa kuhesabu miaka tangu alipofariki, lakini wanapaswa kufahamu kuwa kumbukumbu hiyo ni ya milele.

  “Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ni ya milele, Watanzania tutamkumbuka Mwalimu Nyerere kwa uhai wetu wote hata baada ya kupita miaka mia moja, mia mbili au hata elfu moja.”

  Alisema hiyo inatokana na ukweli kwamba Mwalimu Nyerere ndiye aliyepigania Uhuru wa Taifa la Tanzania na kuweka misingi imara ya uongozi ambayo ndiyo inayowafanya Watanzania kuendelea kujivunia amani na utulivu hadi sasa.

  Habari Leo
   
 13. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2008
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Ndugu:

  Hivi safari ya peponi inachukua muda gani? Maana ata wajukuu zetu wataambiwa kuchukua nafasi hii kuomba ili roho yake ilazwe peponi.

  Na kama kila mtu anabeba mizigo yake, basi maombi yetu hayana mpango.
   
 14. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45

  Kwa maombi yetu tuu hayawezi kufanya roho yake ilazwe mahali pema peponi kama yeye mwenyewe HAKUJIANDAA kuomba roho yake iwe mahali pema peponi na kufanya mambo mema ya kusababisha roho yake iwe huko
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,577
  Likes Received: 18,555
  Trophy Points: 280
  Na kama kila mtu anabeba mizigo yake, basi maombi yetu hayana mpango.

  Maombi yana mpango ndio maana kabla ya dini za kisasa, mababu zetu walitambika. Kupalilia makaburi na misa ya shukrani does something good.
  By the way the issue hapa ni Nyerere. He was a noble man. Pamoja na ubinaadam wake alikuwa mtakatifu na aliishi maisha matakatifu.

  By now I'm not sure kama rohp yake imeishapokelewa rasmi peponi ama nae bado anasubiri ufufuko wa miili ile siku ya hukumu ya mwisho.
  Kuendelea kumuombea ni muhimu.

  Roho yake ipumzike kwa amani-Amen
   
 16. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #16
  Oct 14, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  Malecela: Ufisadi ni ishara ya kumsahau Nyerere
  Oscar Mbuza
  Daily News; Tuesday,October 14, 2008 @00:02

  WAZIRI Mkuu mstaafu John Malecela amesema vitendo vya ufisafi vya baadhi ya viongozi wa umma ni ishara ya kusahau misingi ya uongozi iliyowekwa na Mwalimu Julius Nyerere.

  Katika mahojiano maalumu na HabariLeo kuhusu mustakabali wa Taifa miaka tisa tangu kifo cha Mwalimu Nyerere, Malecela alisema wapo viongozi walioanza kumsahau Mwalimu kwa kukiuka maadili na miiko ya uongozi, lakini akasema hawatafanikiwa katika mipango yao.

  “Nyerere ametuachia nidhamu ya uongozi, aliweka misingi ya viongozi kuwaheshimu wananchi, kuwa waadilifu na waaminifu kwa Taifa lao lakini pia kuwa wazalendo,” alisema Malecela.

  Alisema viongozi wanaodhani kwamba kutokuwapo kwa Mwalimu Nyerere ni mwanya kwao kuwaongoza wananchi bila kuzingatia miiko na misingi ya uongozi, watakumbana na matatizo makubwa. “Hili nalisema wazi, iwe ni ndani ya chama (CCM) au katika serikali, ni lazima matunda ya Uhuru yawanufaishe wananchi wote.

  “Balaa kubwa litatokea kama Watanzania wachache watakuwa matajiri huku wengine wengi wakiwa masikini,” alisema.

  Akizungumzia maadhimisho ya leo ya kifo cha Mwalimu Nyerere, Malecela alisema ingawa Watanzania wanamkumbuka Mwalimu kwa kuhesabu miaka tangu alipofariki, lakini wanapaswa kufahamu kuwa kumbukumbu hiyo ni ya milele.

  “Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ni ya milele, Watanzania tutamkumbuka Mwalimu Nyerere kwa uhai wetu wote hata baada ya kupita miaka mia moja, mia mbili au hata elfu moja.”

  Alisema hiyo inatokana na ukweli kwamba Mwalimu Nyerere ndiye aliyepigania Uhuru wa Taifa la Tanzania na kuweka misingi imara ya uongozi ambayo ndiyo inayowafanya Watanzania kuendelea kujivunia amani na utulivu hadi sasa.
   
 17. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #17
  Oct 14, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  maneno ya malecela yatakuwa na maana iwapo ataanza kupambana na ufisadi kwa vitendo. kwa kuwa amekubali kuwa kuna ufisadi, hiyo ni hatua ya kwanza kuelekea kuushinda. sasa aingie kwenye vita vya matebndo dhidi ya ufisadi, ambao umeshamiri sana ndani ya chama chake. Afanye vita hivyo akitambua kuwa yeye alikuwa kiongozi wa ngazi za juu wa chama hicho kwa muda mrefu sana, hivyo ameshiriki katika kuulea ufisadi, kwani kama angeuua tangu wakati akiwa kiongozi, usingefikia hali hii ya leo
   
 18. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #18
  Oct 14, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  nahisi ulianzia kipindi chake
   
 19. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #19
  Oct 14, 2008
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Rais jk amekuwa mstari wa mbele kupigana na ufisadi na ndio leo hii linazungumzwa wazi wazi na amepiga hatuwa kubwa kurekebisha hilo na limekuwa likionekana hata kwa mataifa wahisani na wao kukubali kazi yake Rais kuwa ni yakupigiwa mfano katika ulimwengu ingesaidia kama John Malecela angeweza kulieleza hilo kwa wananchi wakati alipokuwa akitowa maoni yake haya Hongera Rais JK kwa msimamo wako imara zidi ya Mafisadi
   
 20. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #20
  Oct 14, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  Rais jk amekuwa mstari wa mbele kupigana na ufisadi na ndio leo hii linazungumzwa wazi wazi na amepiga hatuwa kubwa kurekebisha hilo na limekuwa likionekana hata kwa mataifa wahisani na wao kukubali kazi yake Rais kuwa ni yakupigiwa mfano katika ulimwengu ingesaidia kama John Malecela angeweza kulieleza hilo kwa wananchi wakati alipokuwa akitowa maoni yake haya Hongera Rais JK kwa msimamo wako imara zidi ya Mafisadi


  mkuu spea

  kuzungumza waziwazi bila kufanyia kazi hakuna maana hata kidogo na ndio maana wasiojua wanabwatuka na hongera kwa jk!!!!!leo hii kama wanaongelewa na bado wanaendelea kuiba sioni umuhimu wake!!!!natumaini utamshauri aache blaablaaah
   
Loading...