The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,503
- 2,046
- Thread starter
- #41
Na huwezi kupigania katiba mpya chini ya mazingira yaliyopo kwani utaulizwa na wananchi mbona ulishapata wabunge zaidi ya 40% chini ya tume na katiba hii!? Kwa hiyo itaonekana kama mfa majikuna tofauti kubwa kwani wakati wa ukoloni walau sheria za uchaguzi ziliheshimika na kura zilihesabiwa kwa uwazi mkubwa aliyeshinda kashinda aliyeshindwa kashidwa, ila kwa sasa ni uharibifu mtupu, mauaji, utekaji wa wagombea na wizi wa kura wa wazi wazi - sasa kuepusha haya yote ni kheri kama kiongozi ukawaeleza watu wako kupigania katiba mpya na Tume iliyo huru ya uchaguzi.