Nyerere aliwagomea TANU kususia uchaguzi ila Mbowe kawashawishi CHADEMA kususia!! Hili laweza kuwa kaburi la CHADEMA

kuna tofauti kubwa kwani wakati wa ukoloni walau sheria za uchaguzi ziliheshimika na kura zilihesabiwa kwa uwazi mkubwa aliyeshinda kashinda aliyeshindwa kashidwa, ila kwa sasa ni uharibifu mtupu, mauaji, utekaji wa wagombea na wizi wa kura wa wazi wazi - sasa kuepusha haya yote ni kheri kama kiongozi ukawaeleza watu wako kupigania katiba mpya na Tume iliyo huru ya uchaguzi.
Na huwezi kupigania katiba mpya chini ya mazingira yaliyopo kwani utaulizwa na wananchi mbona ulishapata wabunge zaidi ya 40% chini ya tume na katiba hii!? Kwa hiyo itaonekana kama mfa maji
 
Na huwezi kupigania katiba mpya chini ya mazingira yaliyopo kwani utaulizwa na wananchi mbona ulishapata wabunge zaidi ya 40% chini ya tume na katiba hii!? Kwa hiyo itaonekana kama mfa maji
Kupata wabunge hata 50% hakumaanishi kwamba kuna ustawi kwa demokrasia huru. Kushiba home kisiwe kigezo kwamba nyumba hiyo ina amani.
 
Kutoshiriki uchaguzi kwa chama cha siasa ni pigo kubwa sana. Namkumbuka maalim seif alipojifanya kususia kule zanzibar jambo lile halikukisaidia chochote chama chake zaidi ya kukididimiza na sidhani kama angekuwepo eti umshauri asusie uchaguzi kama angekuelewa!! Sababu za wapiga kura kuchagua mtu A na sio B sio lazima iwe mapenzi kwa chama zipo sababu nyingi tofautitofauti lakini pia hujuma za uchaguzi hazipo kila jimbo, kwa hiyo kuwaondoa wagombea wa chama kunawaongezea hasira na kuwakatisha tamaa waliokusudia kupiga kura za hasira dhidi ya mgombea aliyesimamishwa na chama hata kama hakubaliki na wengi

..Chadema walishiriki 2020 na dhuluma waliyotendewa na afadhali wasingeshiriki.

..Kinachohitajika Tz ni uwanja ulio huru kwa kila chama kufanya siasa na kushiriki uchaguzi.

..Hoja yako kuhusu kura za hasira au chuki nazikataa. Nadhani fikra za namna hiyo ndio zinazoharibu siasa za Tz.

..Badala ya kuchemsha bongo na kuja na sera zitakazoboresha maisha ya Watz vyama viko busy kupika propaganda za kupotosha na kujenga chuki.

..Turudi kwenye KANUNI YA DHAHABU / Golden rule kwamba kila mwananchi amtendee mwenzake vile angependa na yeye atendewe.
 
Utadai kupitia jukwaa lipi!? Chama cha siasa ni jukwaa rahisi la kuwaunganisha watu
Kwa mfano sasa hivi CDM wanafanya digital membership registration je wanawafikia wananchi kwa kutumia jukwaa lipi ? information flow sasa hivi kwa kutumia new technologies imerahisishwa sana ndugu - ni mambo ya kujipanga tu.
 
Back
Top Bottom