Sangarara
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 13,100
- 5,649
Mwaka 1995 kama isingekuwa Nyerere ndio Mwaka ambao CCM ingeondoka Madarakani kote Tanzania Bara na Visiwani lakini Nyerere aliingilia kati na kuaribu movement yote, tena akasimika rasmi imani potofu kwa wananchi dhidi ya upinzani kwa kauli zake nzito mpaka za kuwafananisha wapinzani na mbwa.
Kule Zanzibar, Inasemekana Nyerere ndio aliyeasisi Hulka ya kutangaza mshindi mgombea aliyeshindwa. Hulka hii sasa imekomaa na kuwa mwiba kwenye mfumo mzima wa kidemocrasia
Sababu walizokuwa nazo watanzania Mwaka 1995 ndio walizonazo leo. Augustine Lyatonga Mrema alitudhihirishia kutokana na utendaji wake kwamba hakuwa tayari kusimamia serikali ambayo viongozi wake wanahujumu uchumi wa nchi na kupora rasilimali za taifa. Ni mambo haya ambayo leo tunayaita ufisadi.
Wote ni mashahidi kwamba, ufisadi wote mkubwa uliofanyika nchini mwetu tukiufuatilia nyuma haturudi zaidi ya mwaka 1995. maana yake ni kwamba mpaka kufikia mwaka 1995 ufusadi wa kccm katika nchi yetu ulikuwa bado ni mchanga sana na kama Watanzania tusingemsikiliza nyerere leo hii tusingekua tumefikia kwenye hali tete tuliyonayo ambapo mafisadi wanaheshimika na kuogopwa kuliko wazalendo.
Nyerere alikuwa ni kinara wa kupambana na uovu wote wa kiuongozi, kuanzia uzembe, rushwa, ubaguzi, nk na Mrema alikuwa na uwezo wa kutupeleka kwenye hatua ya juu zaidi ya upambanaji wa wazi na kweli dhidi ya uchafu huu.
Nahisi, kosa alilolifanya nyerere sasa linaitafuna hata Historia yake.
CCM aliyoipigania Mwaka 1995 wakati watanzania walipoamua kuitosa kwa sababu ya kukumbatia ufisadi na kutoshughulikia mambo ya watanzania leo haimuheshimu wala kumkumbuka badala yake inawaenzi Mafisadi na Majizi na kukandamiza wananchi na mfumo wa kidemocrasia.
Leo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hataki kusikia habari za Nyerere, Wakati wa Kampeni za Mwaka jana bila kutafuna maneno Kikwete, katika kuelezea msimamo wake na chama chake kwamba wamedhamiria kuachana na falsafa, itikadi na maelekezo yote ya Mwalimu ambayo kimsingi leo watanzania wanamuhenzi kwayo alisema kwamba kila zama zina kitabu chake.
Namuheshimu sana Mwalimu, Na ninatambua kwamba alikuwa ni binadamu kama sisi na hakuwa na uwezo wa Kimungu kuweza kuona namna ambavyo CCM ingemgeuka katika zama hizi, lakini kwa namna ambavyo busara yake ina thamani kubwa kama lulu katika kizazi chetu cha sasa itoshe tu kusema kwamba Mwalimu alirudi kinyume nyume.
Na katika kumkumbuka, ninashauri watanzania tusije kurudia kosa la kumsikiliza mtu mmoja hasa katika wakati ambao kama taifa tumekwishaamua kufanya maamuzi ambayo yanakinzana na Matakwa yake.
Leo tukiri kwamba hatutamsikiliza mtu yeyote katika maamuzi tuliyofikia ya kuiondoa CCM madarakani. Na hapa ndio tutakuwa tunamuenzi vyema kwa kudumisha maelekezo yake ya kutokubali kuwasikiliza wapumbavu sababu watatudharau.