Nyerere alijisaliti na kuwasaliti watanzania

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,649
Mwaka 1995 kama isingekuwa Nyerere ndio Mwaka ambao CCM ingeondoka Madarakani kote Tanzania Bara na Visiwani lakini Nyerere aliingilia kati na kuaribu movement yote, tena akasimika rasmi imani potofu kwa wananchi dhidi ya upinzani kwa kauli zake nzito mpaka za kuwafananisha wapinzani na mbwa.

Kule Zanzibar, Inasemekana Nyerere ndio aliyeasisi Hulka ya kutangaza mshindi mgombea aliyeshindwa. Hulka hii sasa imekomaa na kuwa mwiba kwenye mfumo mzima wa kidemocrasia

Sababu walizokuwa nazo watanzania Mwaka 1995 ndio walizonazo leo. Augustine Lyatonga Mrema alitudhihirishia kutokana na utendaji wake kwamba hakuwa tayari kusimamia serikali ambayo viongozi wake wanahujumu uchumi wa nchi na kupora rasilimali za taifa. Ni mambo haya ambayo leo tunayaita ufisadi.

Wote ni mashahidi kwamba, ufisadi wote mkubwa uliofanyika nchini mwetu tukiufuatilia nyuma haturudi zaidi ya mwaka 1995. maana yake ni kwamba mpaka kufikia mwaka 1995 ufusadi wa kccm katika nchi yetu ulikuwa bado ni mchanga sana na kama Watanzania tusingemsikiliza nyerere leo hii tusingekua tumefikia kwenye hali tete tuliyonayo ambapo mafisadi wanaheshimika na kuogopwa kuliko wazalendo.

Nyerere alikuwa ni kinara wa kupambana na uovu wote wa kiuongozi, kuanzia uzembe, rushwa, ubaguzi, nk na Mrema alikuwa na uwezo wa kutupeleka kwenye hatua ya juu zaidi ya upambanaji wa wazi na kweli dhidi ya uchafu huu.

Nahisi, kosa alilolifanya nyerere sasa linaitafuna hata Historia yake.

CCM aliyoipigania Mwaka 1995 wakati watanzania walipoamua kuitosa kwa sababu ya kukumbatia ufisadi na kutoshughulikia mambo ya watanzania leo haimuheshimu wala kumkumbuka badala yake inawaenzi Mafisadi na Majizi na kukandamiza wananchi na mfumo wa kidemocrasia.

Leo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hataki kusikia habari za Nyerere, Wakati wa Kampeni za Mwaka jana bila kutafuna maneno Kikwete, katika kuelezea msimamo wake na chama chake kwamba wamedhamiria kuachana na falsafa, itikadi na maelekezo yote ya Mwalimu ambayo kimsingi leo watanzania wanamuhenzi kwayo alisema kwamba kila zama zina kitabu chake.

Namuheshimu sana Mwalimu, Na ninatambua kwamba alikuwa ni binadamu kama sisi na hakuwa na uwezo wa Kimungu kuweza kuona namna ambavyo CCM ingemgeuka katika zama hizi, lakini kwa namna ambavyo busara yake ina thamani kubwa kama lulu katika kizazi chetu cha sasa itoshe tu kusema kwamba Mwalimu alirudi kinyume nyume.

Na katika kumkumbuka, ninashauri watanzania tusije kurudia kosa la kumsikiliza mtu mmoja hasa katika wakati ambao kama taifa tumekwishaamua kufanya maamuzi ambayo yanakinzana na Matakwa yake.

Leo tukiri kwamba hatutamsikiliza mtu yeyote katika maamuzi tuliyofikia ya kuiondoa CCM madarakani. Na hapa ndio tutakuwa tunamuenzi vyema kwa kudumisha maelekezo yake ya kutokubali kuwasikiliza wapumbavu sababu watatudharau.
 
Nilipokuwa naanza kuisoma hii thread yako nilianza kuchukia cause nilikuwa naona kama una mtuhumu sana Mwalimu, but kila nilivyokuwa naendelea nikakuta kwamba jambo unalolizungumza NI LA MSINGI SANA.

Kwa hili ulilozungumza ni kweli mwalimu hakututendea haki cause aliaminisha watu kwamba hakukuwa na mbadala wa CCM,alilazimisha mambo ili kuhakikisha mgombea wa CCM ashinde hulka mabayo hadi leo hii wanaendelea kuitumia. CCM bila ya mwalimu ilikuwa niaondoka madarakani mapema sana by 1995.

Akihojiwa juu ya kwanini asiwe neutral mwalimu alisema hawezi kufanya hivyo kwani pamoja na mapungufu mengi ambayo CCM ilikuwa nayo, bado alikuwa haoni mbadala wa chama hicho.

Pamoja na hayo tunatakiwa kumuenzi kwa kukiondoa chama chake, chama ambacho kimeondoka katika misingi ambayo aliiweka yeye kwa maendeleo ya watanzania wote na badala yake kimeamua kuwakumbatia MAFISADI.
 
Mengi uliyoandika siwezi kusema ni nkweli au si kweli, lakini kitu kimoja kimenionyesha kwamba wewe si makini na si mtafiti, mbaya zaidi lugha ya Malkia wa Uingereza huiwezi. Neno alilotumia Mwalimu Nyerere, "I can not allow my country to go to the dogs" au kitu kama hicho maana yake si hiyo unayoandika wewe katika forum hii.

To go to the dogs, refers to greyhounding racing where one goes to rack, dissipate and probably ruin. Maana rahisi ni kucheza kamali au gambling, ambapo matokeo yake ni mwenye kupata apate mwenye kukosa akose.

Hivyo basi, Mwalimu alisema kwamba kwa wakati ule kuwapa wapinzani ingekuwa sawa na kubahatisha. Nina hakika kama angekuwepo leo angesema tofauti.
 
Kwa siku kama ya leo kuandika mada kama hiyo lazima utakuwa na lako jambo,kwa ujumla wake alifanya mema kuliko mabaya
Huu ndio ukweli utakaosimama kwa karne nyingi
 
Napenda sana mageuzi lakini laiti nchi ingeangykia mikononi mwa Augustino Mlema nadhani tungekuwa na migogoro mikubwa zaidi labda kuzidi iliyoko sahivi.Mlema kwa hulka yake nadhani kwanza angegan'gania madaraka

Pili inavyoonekana alisoma alama za nyakati akaona kwamba watanzania walikuwa wamechoka sana na ccm, kwa kuwa kipindi hicho mfumo wa vyama vingi ulikuwa umeanza aliona kwamba akiwa mtendaji mzuri angekuwa maarufu na lengo lake la kugombea urais lingetimia na yeye kwa ndoto zake alidhani angeiangusha ccm.

Kwa hiyo JK NYERERE aliona kwamba nchi ingeangukia mikononi mwa watu kama MLEMA Ingekuwa matatizo makubwa,maana huyu mzee anaonekana hana msimamo thabiti zidi ya wanyonge.mnaona siku hizi anavyomfagilia JK pamoja na madudu yote anayoyafanya.
 
Nyerere amechangia kutufikisha hapa tulipo kutokana na udikteta wake.
 
Hivi Nyerere angekuwa hai enzi hizi za mtandao-whereas people freely air their views what would have happened-me is just thinking aloud
 
Nyerere alifanya mazuri mengi, na bila shaka nakubaliana na waliombatiza baba wa Taifa.
Lakini ni vyema pia tukubali kama kuna mambo alifanya ambayo hayakuwa sahii.
Mosi ni hili KATIBA TULILONALO LEO, ambalo mimi naliita JANGA LA TAIFA, liliasisiwa au kupata baraka zake. Katiba ambalo Rais anakuwa next to GOD. Ikumbukwe pia baada ya watanzania KUKATAA VYAMA VINGI, Nyerere alishiniza kuwe na vyama vingi LAKINI KWA WAKATI HUOHUO, akatengeza mazingira ya KIKATIBA ambayo yanaiweka CCM madarakani milele, labda tu Mungu ashuke na TUME YA UCHAGUZI WAJIFANYE HURU, ndipo watakuwa fair katika maandalizi ya uchaguzi na baadae kutangaza MSHINDI HALALI.
Katika hili la katiba ya CHAMA KIMOJA, kutumika katika mazingira ya VYAMA VINGI, mimi huwa siku zote namlaumu Nyerere. Kwa sababu vyama vingi vililetwa kama geresha kwa wahisani ambao walikuwa wanashiniza uwepo wa vyama vingi. Lakini kwa ndani na kwa dhati kabisa CCM (pamoja na NYERERE) hawakutaka vyama vingi kabisa, hata kuvisikia walikuwa hawataki. Ndo maana leo watu wanaambia mkichagua vyama vingi mtaleta vita.
Naomba kuwakilisha!
 
Nyerere si wenu Watanganyika au......? maanake mnasifu hata kama alikuwa Dictator, na kinachofuatia ni kumuabudu (Mungu Nyerere)!

Nafikiri ulikuwa na namna bora ya kuliwakilisha/kuwakilisha hoja yako bila matusi na kejeli! Unaweza kuwa na hoja katika kile ulichotaka kumaanisha lakini matusi yameharibu uzito wa hoja yako.

Naamini MODS watakutendea haki katika hili!
 
Sijapoteza muda mwingi kusoma hiyo mishairi yako mireefuuu.. kifupi ni kwamba.. " alikua sahihi kufanya aliyoyafanya kwa muda ule"...
 
nimesoma ubeti wa pili. sikujua kama umemtaja huyu mnafi wa kichaga Mrema... kifupi hii post ni .. "CRAP"
 
Ubeti wa 3.... ulitulia kidogo.. ni kweli ufisadi mkuu alifanya MKAPA.. na JK amerithi madhambi mazito yasiyobebeka
 
ubeti wa nne 4.. umechemka.. kumchanganya Nyerere na mrema..... CRAP
 
Dereva Nyerere alipenda kuendesha gari peke yake bila ata kumfundisha konda na kuwasikiliza abiria.Aliacha gari likiwa aliendi gereji na mafuta yakiwa kidogo kwenye tanki(gauge) dereva alipokea gari ajaenda ata gereji au kuongeza mafuta kwahiyo gari lina mis mis na spea hamna.TAFAKURI.
 
Nyerere ni Baba wa Taifa alifanya makosa yake kama binadamu,mwingine yoyote hapa duniani lakini aliasisi kitu ambacho mimi kijana ambae wakati mimii nina miaka chini ya kumi yeye ndio anatoka madarakani lakini leo hii nina imani sana kwenye baadhi ya mambo yake ya misingi ya haki na utu wa mwanadamu yoyote.Uwa naumia sana anaposema haki utainunua kwa bei gani?hakika ni maneno ya uchungu sana hasa ukikumbana na Mtanzania ambae haki yake imeuzwa kwa mwenye fedha hakika machozi ya tumboni yanakutoka.

Lakini mfumo [system] ambayo mwalimu aliiasisi ndiyo imemtupa kwa mbali sana lakini wakiendekeza kuwa Mwalimu ajakosea wakitamka wasiyotenda wakitenda wasiyotamka.Nimefurahi kuwa Pro Shivji anasema yale ambayo Mwalimu alikosea ndiyo yanapaswa kusema ili watu wajifunze madhara yake.lakini leo hii kuna baadhi ya viongozi wamekuwa wanafiki wasiotaka kukili makosa ya Mwalimu wayaseme wazi kuambia Watanzania kwa kuwa wanajua makosa ya Mwalimu wao leo ndio neema zao kufaidika kujilimbikizia mali kwa migongo ya makosa ya Mwalimu.

Kuna viongozi ukiwaona sura zao mbele ya umma utafikilia Maraika,na ukiwachukua raia wazee wa miaka 50- na kuendelea ndio uwaambii kabisa kuhusu hawa waalibifu wa Taifa wanaamini ni wafuasi bora wa Mwalimu.Asilimia kubwa ya watu wazima wa miaka 50 na kuendelea ni waoga wa mfumo kinoma sana kiasi kuwa woga wao huo umefikisha Taifa kuachia viongozi walafi kuliibia Taifa kwa visingizio wale wana hoji wizi huo KUONEKANA WAKOLOFI NA KUWA NI WAVUNJAJI WA AMANI.Watamkopi Mwalimu kutete uovu wao huo.

Mwalimu ametuachia baadhi ya wanafiki kibao ambao wana furahi kuishi Manhattan USA kitabia na matendo lakini wanaongea na kuzungumza kimanzese Tanzania.
 
Back
Top Bottom