Nyerere akashifiwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyerere akashifiwa!

Discussion in 'Jamii Photos' started by Shomari, Jul 7, 2012.

 1. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Jione mwenyewe, hii ni kwa mujibu wa gazeti la ANNUR. Source

  [​IMG]
   
 2. MCHONGANISHI

  MCHONGANISHI JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 363
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  Napiga tu!
   
 3. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Hawa wanatafuta tu Ugomvi, kwanini kila kitu ukitafutie makosa yake? yaani kuanzia vitabu wao ni kukosoa tu hapa pameandikwa sivyo, huyu siyo MASIHI lakini ndiye atakeyerudi siku za mwisho na KUOA mara atabadili DINI kabla ya kuwachukua watu wote.
  Lakini mwisho kinara wao alipoulizwa siku ya mwisho itakuwaje aliwajibu nendeni kwao mukawaulize mimi sijui na sitakuwepo.
  sasa mambo ya kumsemea MALASUSA ni hukohuko kwenye ANNUR hapa JF mtatuchonganisha, namuomba Mods aikimbize jukwaa la DINI ntachangia zaidi kuhusu siku nilipoacha kuingia humo ndani kwamba hata ukiwa wa mwisho katika mstari pembeni yako kuna mtu asiyeonekana (nilihofu na sitarejea bora niwe mpagani DINI ya mababu zangu kwani hizi zote zimeletwa na watu weupe ili watukandamize na NINASEMA ASILANI HAKUNA MTU ALIYEKWENDA HUKO AKARUDI KUTUHADITHIA ETI WAPAGANI HATUTAENDA KUNAKO RAHA)
   
 4. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ni Muhimu na ni lazima!!

  Vyombo vya Habari Viwe CONTROLLED against NATIONAL SECURITY!!

  Amani ya TAIFA itakapofikia BREAKING POINT Watanzania wote wataumia bila kujali dini, itikadi, kabila, ukanda , jinsia nk
  Jamii ya Tanzania Inaunganishwa na UTU kwani UTU hauna dini, hauna itikadi, hauna ukabila, hauna ukanda, hauna rangi, hauna jinsia UTU NI UTANZANIA na niwajibu wa kila Mtanzania kuulinda na kuutetea!!
   
 5. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Mbona hawakuwahi kumwambia Nyerere hivyo akiwa hai??
  Wabafiki utawajua tu!!

  Wanagombana na marehemu!
  Akili za reverse hizi
   
 6. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Mina nadhani hapo ni typing error,siyo bangi la Nyerere ila BUNGE LA NYERERE!
   
 7. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Watu wengine Bana! Eti amekashifiwa tena ? Kwani si tunaona kila siku watu wakitukanwa matusi ya nguoni humu?
  Achana nayo hayo hayatusaidii humu sisi! Si tunadai uhuru wa kusema ? Waache waseme watakavyo nawe andika lako kwa mwengine . Tuachie sisi na raha zetu.
   
 8. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Yaani kumkashifu mtu, ama kumtusi mtu ndio uhuru wa kusema?!! Uhuru wa kusema una mipaka. sasa wewe unapata raha gani baba wa taifa lako anapotukanwa?
   
 9. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Unaposema Baba wa Taifa langu una maana gani zaidi ya sifa tu au heshima? Hata hivyo huyo Baba hakuwa Saint kwamba hakuwa na mabaya. Sasa tunaposema mabaya yake unasema katukanwa? Naam wewe unahisi Bangi ni majani lakini kwa wengine Bangi inaweza kuwa jambo jengine na hilo jambo pengine ndilo alilolikosea na kulaumiwa, sijui ni kashfa hiyo?
   
 10. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #10
  Jul 8, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Kwa hakika hii ni typing error. Tusibishane kwa ajili ya typing error. Nyerere alitaifisha shule ili Waislamu waweze kusoma. Mimi nimesoma katika shule ya Kikristu na Waislamu wengi. Waislamu wanasema zamani shule za Kikristu ndizo zilikuwa nyingi,Wakristu tu ndio waliokuwa wanasoma,Wakristu tu ndio waliokuwa wanapata ajira. Na Nyerere ndiye aliyerithi huo mfuom kutoka kwa Wakoloni,eyey ndie alikuwa kiongozi,kwa hiyo,unaweza kusema, kwa hali fulani,yeye ndie mwenye makosa.
  Sheikh Kassim bin Juma alikuwa ansema,''Kila unapomuona mtu maskini Tanzania,more often than not,atakuwa ni Mwislamu,ndio maana tunasema hii nchi ina mfuom-Kristu,na hayo yote yameanza wakati wa Nyerere.......''
   
 11. MDAU JR

  MDAU JR JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 393
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huu ubaba alipewa na nani? Alikuwa binadamu kama wengine, alikosolewa/anakosolewa naye alikosoa, alitukana watu naye alitukanwa na anatukanwa ndivyo binadamu yeyote anavyokuwa.

  HAKUNA BINADAMU ALIYE MKAMILIFU.
   
 12. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #12
  Jul 9, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ngekewa, unaweza kutafsiri unavyoweza neno '' Bangi'' sababu kila mtu ana uwezo tofauti wa kufikiri. kwangu mimi bangi inabaki kuwa bangi tu, kama ilivyo nyekundu itabaki kuwa nyekundu. sipo hapa kukuaminisha kwamba nyerere katukanwa ama lah!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #13
  Jul 9, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Sijui ulipoposti na kusema kakashifiwa jee nalo neno kashifu lina maana nyingi tofauti? By the way tufunge mjadala baina yetu kwani Baba anauma na hasa unapokubali kuwa huyo ni Baba wako wa Taifa.
   
 14. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #14
  Mar 7, 2013
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Wewe utakuwa umelewa Chimpumu , kama sikosei
   
 15. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #15
  Mar 8, 2013
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nahisi kama wewe umekusudia hivyo?
   
 16. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #16
  Mar 8, 2013
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Sijakuelewa. fafanua zaidi
   
 17. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #17
  Mar 8, 2013
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kumkashifu!!!
   
 18. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #18
  Mar 8, 2013
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Labda nikuulize wewe, mtu akisema ''Bangi la Nyerere'' hapo wewe unaelewa nini? kawaida kwa hali ya sasa na tamaduni za kitanzania, jamii inamchukulia mvuta bangi kama ni mtu ambaye ni mhuni, asiye na mwelekeo. bila kusahau pia , kwamba wagonjwa wengi wa vichaa na matatizo ya akili wanahusishwa na matumizi ya bangi ama madawa mengine ya kulevya. sijui, una maoni gani?
   
 19. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2013
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwani pale tunapomlaumu spika bungeni na wengine wakimsifu wewe unahisi vipi? Unachokiona wewe kizuri usimlazimishe mwenzio akione kizuri na yuko wazi kukieleza atakavyo. Hivyo wewe unafikiri sote Bangi tunaiona ni mbaya?
  Kashifa kwa mimi ningeona kuwa ni matusi na sio mtazamo tofauti wa mtu juu ya fulani.
   
 20. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2013
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Nadhani, kwako wewe unaielewa , ama unaichukulia kashfa kama ni matusi yale ya kitandani. naomba nikujulishe kwamba: Bangi ni taboo (Mwiko ) pia matusi, bila kujali kama ni ya mdomoni ama ya kitandani, nayo ni taboo. sasa sielewi unachokiongea hapa. kwa mfano. spika kaingiaje kwenye mada hii?. kwa taarifa yako, kulingana na sheria za Tanzania, bangi ni zao haramu. halikubaliki.
   
Loading...