Nyasi za Juncao: Suluhusho la malisho ya ng'ombe, mbuzi na kondoo

Nimekuza sana, hope mwakani nitaweza kupanda hata eka tatu.

Nilichukua mbegu kidogo naona zimekubali sana sema natuma picha zinagoma.
Umepanda eneo la kawaida au kwenye ardhi ya majimaji?

Ulipanda kipindi cha mvua au ulipanda kwa kumwagilia maji??
 
Bosii hii mimea Ina madhara gani kwa ardhi, pia kama Eka Moja inaweza kulisha mbuzi 60 kwa mwaka ni kwa namna gani? Maana nilivyoelewa ni kwamba inavunwa kwa mara moja au Kuna namna ya kuhifadhi majani yaliyovunwa kwa matumizi ya baadae?
 
Haina madhara,mimi navuna kila baada ya siku 30,namwagilia na kuweka mbolea ya samadi,yanahifadhika kwa njia ya silage.

Hizi chini ni picha za mwezi Septemba 2023 wakati huu wa ukame.

Mawasiliano:0756625286

.
IMG_20230829_162944_173.jpg
IMG_20230929_112843_160.jpg
 
Bado tuko nyuma sana kuliko wenzetu kwa Kweli
Viongozi wetu na sisi wenyewe hatujishughulishi na kuungana na dunia
Huu mmea hapo jirani Kwa Zulu natal mwaka 2010 walikuwa wamepanda sana

Hata Rwanda pia wamepanda sana ila sisi tunaisaidia dunia bila kujijua huku wakibeba mbegu na hata wadudu na wanyama ila sisi haturudi na kitu kipya pindi tunapokuwa nje ya mipaka
Mkuu mbona hayo yamejaa Rungwe tele.
Shuleni huyapanda kama mpaka. Hata shule niliopo yapo.
 
Yapo mengi tu bongo yanastawi vizuri eneo lenye maji.
Ula kwa bongo yakijazana hivyo yatakuwa makao makuu ya nyoka
 
Nyasi za Juncao ni nyasi zilizofanyiwa utafiti nchini China, utafiti ulifanywa na Profesa Zin Zhanxi wa chuo kikuu cha Fujian Agriculture and Forestry.Ni hybrid ya aina tofauti za napier na yanafanana na majani tembo(elephant grass).Yanafahanika pia kwa majina ya Giant Juncao na majani ya maajabu.China wanayatumia zaidi kwa ajili ya kutengenezea uyoga.

Maajabu yake:
Ni nyasi kubwa, ndefu na pana, urefu wake unafika futi 8,Yana mizizi imara na mirefu inayofanya yavumilie ukame,hutoa machipukizi mengi,yanakua kwa haraka.

Nyasi za Juncao pia zina virutubisho vya wanga, vitamin na kiwango cha protini ni 12%.Eka moja ya Juncao huweza kutoa tani 180-200za majani mabichi kwa mwaka mmoja kiasi kinachotosha kulisha ng'ombe 15 kwa mwaka mmoja.

Mwaka 2017 nchi ya Papua New Guinea iliweka rekodi ya kuvuna tani 341 kwenye eka moja na hicho ndicho kiwango kikubwa cha mavuno ya Juncao kilichorekodiwa hadi sasa.

Juncao pia huweza kulisha kuku na ndege wengine wanaokula nyasi kama chakula cha ziada.

Tupande nyasi ili tuepukana na ukosefu wa malisho hasa wakati wa ukame.
Ukihitaji mbegu za Juncao piga simu-:0756625286.

.View attachment 2279361View attachment 2278996View attachment 2279358View attachment 2279363View attachment 2279363
Mbegu unauza bei gani mkuu?
 
Bado tuko nyuma sana kuliko wenzetu kwa Kweli
Viongozi wetu na sisi wenyewe hatujishughulishi na kuungana na dunia
Huu mmea hapo jirani Kwa Zulu natal mwaka 2010 walikuwa wamepanda sana

Hata Rwanda pia wamepanda sana ila sisi tunaisaidia dunia bila kujijua huku wakibeba mbegu na hata wadudu na wanyama ila sisi haturudi na kitu kipya pindi tunapokuwa nje ya mipaka
Hii tayari fanyia Kazi mkuu usilielie
 
Back
Top Bottom