Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,913
- 30,255
KUTOKA NYARAKA ZA LAWI NANGWANDA SIJAONA: MWALIMU ANAMWAGIZA MSAIDIZI WAKE JOAN WICKENS AMPELEKEE SIJAONA KITABU ''FALSE START IN AFRICA''
Adam Sijaona mtoto wa marehemu Nangwanda Lawi Sijaona amenifungulia nyaraka za baba yake nisome kama Ally Sykes alivyonifungulia nyaraka zake.
Hili ni jambo kubwa sana kwa mtafiti yeyote kuonyeshwa nyaraka za ndani chumbani wala si za uani za historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiandikiana na wale ambao alikuwanao kwanza katika kupigania uhuru wa Tanganyika miaka ya 1950 kisha katika kuendesha serikali miaka ya 1960 na kuendelea.
Adam Sijali Sijaona kaniandikia ananieleza kuwa katika nyaraka za baba yake kuna barua kutoka kwa Mama Wickens kwenda kwa baba yake kuhusu vitabu ambavyo Mwalimu akiazimana na Lawi Sijaona.
Adam akanifahamisha kuwa barua hizi anaziweka pembeni.
Mimi ile kusoma kuwa Nyerere akiazimana vitabu na Sijaona moyo umeanza kwenda mbio.
Kimoyomoyo naanza kumlaumu Adam kwa kule kusema kuwa barua hizo za Joan Wickens kwa baba yake anaziweka pembeni maana yake kuwa mimi hatanionyesha.
Adam kwake yeye kaona labda si muhimu kwangu.
Kanichokoza naweka hapa chini maneno niliyomwandikia rafiki yangu:
''Duu...
Baba akiazimana vitabu na Kambarage!
Hii kubwa kushinda Mlima Kilimanjaro.
Nipatie hizo barua kaka.
Sijali wewe unataka kufanya maskhara bwana.
Hii sijaona popote.
In Shaa Allah nitaandika jambo kuhusu Nyerere na vitabu tena kutoka kwa watu wake wa karibu sana.
Nyerere alikuwa na wazimu wa vitabu.''
Juma Mwapachu anaijua maktaba ya Mwalimu na kapata kunisifia kuhusu hazina iliyoko nyumbani kwa Mwalimu Butiama.
Adam akaniletea barua hizo na kwa uungwana wake akaniambia,''...kumbe hizi nyaraka sipaswi kutolea hukumu mimi nilibahatisha kukufahamisha sikujua utakuwa na shauku nazo kiasi hicho.''
Mtafiti gani ambae hatakuwa na shauku ya kusoma nyaraka za Joan Wickens au za Julius Nyerere mwenyewe?
Mimi nilitaka kujua Mwalimu akisoma vitabu gani?
Kwani kuna vitabu na vitabu.
Si kila kitabu ni kitabu.
Mzigo wa barua za Julius Nyerere kwa Joan Wickens, barua za Wickens kwa Lawi Sijaona na kadha wa kadha zikaingia.
Furaha yangu haielezeki.
Soma mwenyewe hapo chini barua ya Mwalimu kwa Lawi Sijaona.
Tusiandikie mate wakati kidau cha wino tunacho.
Sijali akawa kanipa ufunguo kwa kufungua kwanza ubongo wa baba yake Mzee Sijaona pili ufunguo wa kufungua ubongo wa Mwalimu Nyerere.
Kuna barua nyingine Mwalimu Nyerere anamuagiza Joan Wickens, Personal Assistant to the President kumpeleka Lawi Sijaona kitabu hiki, ''False Start in Africa,'' kilichaondikwa na Mfaransa Rene Dumont.
Kitabu hiki kilikuwa maarufu sana miaka ya 1960 na Mwalimu kakisifia anamwambia Sijaona kuwa kinafaa kwa maendeleo ya Tanzania.
Maneno haya Mwalimu kaandika mwaka wa 1966.
Nilipoona kitabu hiki cha Rene Dumont katika barua ya Mwalimu akili yangu ikarudi nyuma hadi mwaka wa 1972 niko nyumbani kwa Dome Okochi Budohi, Ruiru, Nairobi nimekwenda kumtembelea.
Dome Okochi Budohi kadi yake ya TANU ni. No. 6.
Naamini wengi mtashangaa mbona hamjapata kumsikia popote akitajwa katika ya TANU na uhuru waTanganyika?
Historia ya Dome Okochi Budohi katika siasa za TAA hadi TANU ni ndefu na nimemweleza katika kitabu cha Abdul Sykes.
(Dome Budohi alikamatwa Dar es Salaam 1955 na kufungwa kisiwani Lamu, Kenya akishukiwa kuwa ni Mau Mau).
Kitabu hiki ''False Start in Africa,'' nilikikuta nyumbani kwa Dome Budohi Nairobi na nilianza kukisoma lakini sikuweza kukimaliza na Mzee Budohi akanipa kitabu hiki nikimalize kusoma Dar es Salaam.
Kwa miaka mingi kitabu hiki nilikuwanacho Maktaba lakini kimepotea.
Kitabu hiki kimesomwa na Julius Nyerere, Lawi Sijaona na Dome Budohi wote hawa wanachama wa TAA na waasisi wa TANU.
Hii inaonyesha vipi fikra za wazalendo hawa zilivyokuwa zinashabihiana katika kutafuta maendeleo ya nchi yao.
Nimeiona maktaba ya Hamza Mwapachu katika miaka ya 1970 iko vilevile kama alivyoiacha mwenyewe miaka mingi baada ya kufariki.
Wazalendo hawa walikuwa watu wa kusoma vitabu.
Picha: Barua ya Mwalimu Nyerere kwa Nangwanda Lawi Sijaona, Mwandishi na Dome Okochi Budohi na Adam Sijali Sijaona na baba yake Nangwanda Lawi Sijaona.