Nyaraka mpya za Kagoda zawalipua Rostam, Manji

Anaitwa Kainerugama Msemakweli. Aliwahi kuja na single ya Mafisadii wa Elimu hapa nchini wakiwemo Makongoro, Diallo, N.k
Thanx kwa info mkuu..ngoja nijaribu kutafuta profile lake kwa undani zaidi
 
Kwakuwa DPP amenitafuta jana ili nimwongezee ushahidi, nitaonana naye kesho kwakuwa kaonyesha uungwana lakini baadhi ya ushahidi sina sababu ya kuwapa kwakuwa najua wanao.

Tunachotaka ni hawa wezi kupelekwa mahakamani kwakuwa wanajulikana. Namaanisha Yusufu Manji na Rostam Aziz
 
Huyu mhaya John Kato anayetumiwa hana kazi yoyote ya maana kwenye kampuni ya Caspian isipokuwa anatumiwa tu kwenye michezo hii michafu.
 
Msemakweli ni nani huyoo jamani?
Huyu ndio yule mwanaharakati alieandika kitabu cha matapeli wa elimu Tanzania, kawaorodhesha matapeli wote wenye Phd na degree za uongo wakiwemo Makongoro Mahanga, Deodatus Kamala, Emanuel Nchimbi hao ni kwa uchache orodha ni ndefu.
 
Kwakuwa DPP amenitafuta jana ili nimwongezee ushahidi, nitaonana naye kesho kwakuwa kaonyesha uungwana lakini baadhi ya ushahidi sina sababu ya kuwapa kwakuwa najua wanao.

Tunachotaka ni hawa wezi kupelekwa mahakamani kwakuwa wanajulikana. Namaanisha Yusufu Manji na Rostam Aziz
Kwanini wapelekwe mahakamani wakati tayari wanajulikana na wameshaanza kuzirejesha hizo hela?
 
Kwa kifupi nilitaka kuwaeleza haya, kuwa wezi wa Kagoda wanafahamika na serikali isidanganywe wala isidanganye juu ya wezi hawa hivyo nimewataja bila kuumauma maneno
 
msemakweli ni kijana mmoja mwanasheria aliyetoa kitabu cha mafisadi wa elimu
 
Mkuu invisible, siku zote tumekuwa tukiambiwa na kuamini kwamba pesa zilizoibwa na Kagoda zilikuwa ni kwa ajili ya kuisaidia CCM katika uchaguzi wa 2005. Lakini mbona Kato anasema si kweli ila hizo pesa waligawana tu Rostam, Manji na Tabu Omari? Ukweli ni upi sasa?
 
Niseme ukweli mimi si mwana CCM na sintokufa nikiwa CCM, mimi ni CHADEMA tangu mwaka 1999 na nitaendelea kuwa CHADEMA - Msemakweli
 
ninachokiona hii movie inaelekea pazuri!!
mungu wetu tenda miujiza watanzania tupate haki yetu waliotupora na wanayoendelea kupora
 
msema kweli anayo yaongea naanza kuyaamin.hata alipotaja viongozi wenye vyeti feki kila mmoja alisema anaenda mahakamani lakini hadi sasa hakuna aliyethubutu kumshitaki.mimi hadi sasa nampa salute msema kweli.msema kweli mia.
 
Umemaliza?
Hapa sijaona kitu kipya..ni yale yale tu tuliyoyazoea!
Huyu Msemakweli anajitafutia tu umaarufu.
 
Mkuu invisible, siku zote tumekuwa tukiambiwa na kuamini kwamba pesa zilizoibwa na Kagoda zilikuwa ni kwa ajili ya kuisaidia CCM katika uchaguzi wa 2005. Lakini mbona Kato anasema si kweli ila hizo pesa waligawana tu Rostam, Manji na Tabu Omari? Ukweli ni upi sasa?
Pesa za Kagoda zilienda kwenye kampuni ya Manji kwa mafungu na nyingine zilienda baada ya uchaguzi 2005; sidhani kama hizi zilienda kwenye kampeni za JK kama watu wanavyoweza kudai. Ushahidi upo na hata Msemakweli kaliongelea hili.

Hakuna transaction inayoonyesha kwenda kwa Manji. Kama hela zilitoka Dubai zikaja CCM basi hapo ndo hatukuweza kupabaini!
 
kuna watu wakiskia jina hilo nywele zinawaisha kichwani... kwa wanaokumbuka ile ishu ya digri fek
 
Kwanini wapelekwe mahakamani wakati tayari wanajulikana na wameshaanza kuzirejesha hizo hela?
Rejao hivi umehanithiwa akili? Tangu lini sheria ya jinai ikatoa nafasi ya mwizi kurejesha alichoiba na akaruhusiwa kudunda mtaani?au ndivyo Ccm mnatumaliza ?na je kwanini Serikali inadai kutowajua hao wezi na wakati huo inasema wamerudisha pesa walizokwapua?contradicting!!!!!
 
Kampuni ya Afritainer ilirejesha kiasi cha kama Bil 3 hivi (na ushahidi upo). Wakurugenzi wa kampuni hii ni wajomba zake Rostam, wamefanya uhuni mwingine wa kuwaondoa hawa wajomba zake kama wakurugenzi na kuwaweka wakurugenzi feki.
fungu funguka funguka mwana....na mwaka huu magamba yatajibeba.mia
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Ukweli ni kuwa kina Rostam na Manji wanataka watanzania waamini kuwa pesa zilienda CCM kwenye uchaguzi lakini hii ni janja ya kutaka wasifikishwe kwenye mikono ya sheria.

Rostam na Manji nawamudu, siogopi usalama wangu. Siwaogopi na liwalo na liwe! Sitishiki juu ya usalama wangu.

Msemakweli
 
Back
Top Bottom