cDNA
JF-Expert Member
- Nov 10, 2016
- 353
- 348
Habari zenu wadau....
Napenda kushea nanyi kilichonikumba majuu.
Ni kawaida yangu kula menyu yoyote ile iwapo mbele yangu hasa nyama almuradi isiwe ya wanyama tunaokatazwa waislamu, haijalishi imechinjwa na muislamu au mkristo, mwanamke au mwanamme. Bongo wanyama waliwao na jamii kubwa ya TZ, pia waislamu hula isipokuwa wanyama wachache maarufu kama mbwa na Kitimoto. Pamoja na kuwepo kwa general formula (ktk uislamu) ya wanyama wasioliwa lakini mara nyingi hatutarajii waTZ kula wanyama kama paka na mfano wake.
Wakati fulani nilipokuwa moja ya nchi za Ulaya ktk shughui zangu nilienda kuwatembelea rafiki zangu wazungu. Waliniuliza vyakula gani ninakula...nikawajibu vyote kasoro nguruwe. Mbwa sikumtaja kwa kuwa Ulaya mbwa athaminiwa na kujaliwa mno na hawawezi kumchinja kama kitoweo. Safari mbili tofauti nilizokaribishwa kuwatembelea nilikula nyama za kawaida (ng'ombe, kuku). Safari ya tatu nikakuta wameandaa menyu kama kawaida na nilipoangalia kitoweo nikaona kama samaki mkubwa (mfano wa seewa) amekatwa vipande vingi (transversely).
Nilipokuwa naendelea kukamua...ni kawaida ya wazungu kuelezea aina ya chakula kilichomezani. Hapo wakataja nyama ile ni ya "Raccoon"...mbali ya classification yangu yote ya O' level na A' level hako kalikuwa kamsamiati kapya na kakanitoa jasho ila nikajipa moyo ni mnyama wa kawaida ambao kwetu ni halali kula...
Mi nikawajibu kuwa nilidhani ni samaki nyama imefanana mno na ya samaki. Wakasema ati nyama ile ni kutoka kwenye mkia.
Nilipomaliza makamuzi kikaletewa kitabu kikubwa kama BS wakijaribu kumdadavua huyo mnyama na kunionesha picha yake na kumpa sifa kede kede za akili n.k.
AYAA KUMBE MNYAMA MWENYEWE NDO HUYU! C KAMA PAKA TU...NILIJISIKIA VIBAYA KAMA KICHEFUCHEFU ILA KUTAPIKA CTAPIKI NIKAWA MNYONGE SANA BUT CKUWAONESHA HILO WENYEJI WANGU. Nikagundua kuwa nilipaswa niwape general formula ili wajue kuwa waislamu hatuli wanyama wenye sifa zipi kuliko kumtaja nguruwe pekee.