Nyama choma

Nyama choma

michepuko

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2014
Posts
1,192
Reaction score
346
Kwa members wenzangu mnaoishi dar,si vibaya tukishare information ya sehemu ninayoweza kupata nyama choma nzuri iwe bar au hotel ndani ya jiji letu hasa ikizingatiwa na leo ni week end..

JF where information meet the Destination...
 
Kwa members wenzangu mnaoishi dar,si vibaya tukishare information ya sehemu ninayoweza kupata nyama choma nzuri iwe bar au hotel ndani ya jiji letu hasa ikizingatiwa na leo ni week end..

JF where information meet the Destination...

... NYAMA CHOMA
Miongoni mwa vyakula vinavyopendwa na
kuliwa na watu wengi ni pamoja na nyama za
kubanika maarufu kama ‘nyama choma’
zitokanazo na wanyama (Red Meat). Kiuasili
wake, nyama ni chakula muhimu kwa mwili
wa binadamu kutokana na kuwa ndiyo chanzo
kikuu cha protini. Na kwa kawaida, nyama
choma huwa bora zaidi kuliko nyama za
kukaanga au kuunga kwa mafuta.
Hata hivyo, ukiukwaji wa kanuni za mpangilio
wa ulaji vyakula umeifanya nyama kuwa
hatari kwa afya za watu wengi. Katika kundi
la vyakula, nyama hasa nyekundu, imewekwa
katika kundi la vyakula vinavyotakiwa kuliwa
kwa kiasi kidogo kwa lengo la kuupatia mwili
protini.
Lakini katika hali halisi, hali haiko hivyo. Watu
wanapenda sana kula nyama kupita kiasi na
kwa kiwango ambacho kiingiapo mwilini
hugeuka kuwa sumu inayokimbilia kwenye
‘joints’ za miguu na kuwafanya walaji
kupatwa na matatizo ya kuumwa miguu. Pia
ulaji wa nyama kupita kiasi, huchangia
ukosefu wa choo kwa muda mrefu kwa mlaji.
Ieleweke kwamba ulaji wa nyama siyo jambo
la kuonyeshea ufahari au kujivunia, mtu
anayekula mboga za majani au dagaa ni bora
zaidi kuliko yule anayekula nyama kila siku.
Hivyo kwa kujali afya zetu, tunashauriwa kula
nyama kwa nadra na kwa kiasi kidogo.Badala
yake tupende zaidi kula mboga za majani, au
samaki, kuku na dagaa.
Aidha, hata ulapo nyama choma au ya
kukaanga au kupika, ikiwa ni jamii ya nyama
nyekundi, ni lazima ujue jinsi ya ‘kubalansi’
mwilini. Itafaa zaidi ulapo nyama ukala
pamoja na mboga za kutosha, zikiwemo
nyanya, vitunguu na kisha kunywa maji mengi.
Hii itakusaidia kuondoa sumu iliyopo kwenye
nyama kwa urahisi zaidi pindi iingiapo
mwilini.
Lakini kwa bahati mbaya sana, watu wengi
hupenda kula nyama choma au mishikaki ya
nyama nyekundu kisha kushushia na bia. Kwa
mtindo huu wa maisha, watu hawa hutia
mwilini vitu hatari ambavyo huleta madhara
ya kiafya makubwa baadaye na hata tatizo
lolote la kiafya likitokea, si rahisi kujua
limetokana na staili hii ya maisha.
Tunatakiwa kujiepusha na mtindo huu wa
maisha.
 
Kbm kama huna hela sema. Nyama ina sumu gani ? si wamasai wote wangekua marehemu kwa sasa. wakurya je ambao kkila siku mtu lzm ale nyama choma kutwa mara tatu. Ondoa angalizo lako. tunakula nyama kwa raha zetu plus castle briiiidi at yhe right temperature.
 
Java - banana
kwa members wenzangu
mnaoishi dar,si vibaya tukishare information ya sehemu ninayoweza kupata
nyama choma nzuri iwe bar au hotel ndani ya jiji letu hasa ikizingatiwa
na leo ni week end..

Jf where information meet the destination...
 
Back
Top Bottom