Zamiluni Zamiluni
JF-Expert Member
- Feb 11, 2014
- 13,997
- 15,104
Shukran jazila..... umenifaa sana kilugha.Black mamba kwa jina lingine
Shukran jazila..... umenifaa sana kilugha.Black mamba kwa jina lingine
Na akikudeshi kulalalia au kukimbilia kulia we pitia huko aliko aliko lalia kwan hubadili aamuzi ghafra na kupitia aliko acha wazi ili we ukijaa tu unakurana nqae huo ndo utaratibu wake.
Huo utaalamu wa wadudu aina ya maji moto pale SUA wanao. Wanawapandikiza ktk miti ya machungwa, miembe n.k. nyoka hakatizi, wanasepa huku wakitii sheria bila shuruti.
Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
Shukran jazila..... umenifaa sana kilugha.
KOBOKO !! sijapata kuona hata picha yake haipatikani GOOGLE !!
Lakini mbona wanadai siyo mkorofi? Wanadai ni hadi umkorofishe, la sivyo akishaona kuna mzozo yeye Koboko anakimbia. Au ni stories tu za Wazungu wanatuzingua?
eboo wanalenga utosini tena, inamaana wanatabia ya kukaa juu sio chini?
kuhusu kuishi kwenye mashamba ya bangi na kuwa thamini watunzaji wa hilo shamba kuna ukweli wowote hapa kuhusu huyu kiumbe koboko???
mkuu koboko hapendi kabisa kelele na mara nyingi anakaa msituni sn, koboko akikuona huwa anajihami kwani anajua utamletea zengwe! Sasa hapo kwenye kujihami ndo anaweza akakimbia au akasimama wima kukutisha na ukitikisika tu lazima akupe mambo!
Ndo maana nilikwambia kusimama kunahitaji ujasiri na pia uhai wako unategeme huruma yake sisi akisimama tulikuwa tunasema anakupima urefu. Koboko kukukimbia ni mara chache sn na akikimbia huwa haendi mbali so usilogwe kumfuatilia kwani huyu ni km askari wa msituni anaweza akakujeruhi muda wowote!!
Mkuu huyu kiumbe ni bora umsikie, kuna stori nyingi juu ya huyu kiumbe na wazee wanatwambia ukimkuta kwenye shamba la bangi huwa anakuwa mkorofi zaidi na wao wakamhusisha kuwa anavuta bangi japo inasemekana huwa anakula mbegu za bangi.
Nadhani nimekujibu mkuu!
Duuh! Hawa nyoka si maliasili yetu, kwa nini wauwawe, si wawakamate na kuwaweka Snake Park.
Hata hivyo, Nakumbuka kule Singida, Wilayani Iramba katika Gereza la Kazi la Ushora, Koboko aliwauwa wafungwa 15 in 3 minutes askari magereza akafanikiwa kumpiga risasi. Sumu yake ni Neurotoxic yaani inashambulia cell za fahamu na mishipa ya fahamu kwa ujumla and causes instant DEATH. Face KOBOKO Face DEATH.
Koboko anaitwaje kwa kienglish?
Kaka Morphine hao wanaenda kula posho na matunda pori tu hasa yanayoitwa nhondwa maana ndo msimu wake huu. Huyo nyoka ni mtalaamu wa kusoma mazigira hakuna mfano. Usiku hutoa kichwa shimoni na kuanza kupiga kelele kama msuguano wa msumeno wa kukatia mbao usiotumia umeme. Nyoka hao huhama wenyewe kila pori linapokuwa linafyekwa (uharibifu wa mzigira unapofanywa hasa ukataji miti). Hakuna watakachofanikiwa labda wapige mabomu kama yale ya Syria au kuteketeza miti yote hasa aina ya "migobeko" ambayo ndio beach zake koboko. Mie nilicheka sana baada ya kumuona Nyalandu akiwahadaa wana Urambo. Njia nyingine ya kienyeji ni pamoja kumuuita Koboko kwa style ya mluzi ukiwa umetengeneza banda la miti ya kijani japo na imani za dawa za kienyeji hutumika. Wakati tukiwinda ndege kwa style ya mluzi koboko alikuwa anatuibukia mara kwa mara lakini ujasiri wa kupambana nae ulikuwa unatoweka na kila mtu kutelekeza ndege na koboko anajilia na kusepa zake. Ni kama hadithi lkn amini usiamini. Kwanza dawa kama hizo waliokuwa nazo washaaga dunia na mara nyingi zilikuwa zinapatikana kwa Wagoyangi (malenga wa ngoma za kucheza na nyoka)
mkuu hizo stori zipo lkn ukweli ni kwamba huwa anakula mbegu za bangi km chakula so wanahusisha kuwa zinamvuruga akili na kumpa kujiamini km alivyobinadamu mvuta bangi.
Ni kweli ukimkuta kwenye shamba la bangi sio rahisi kumtoa ni aheri umuache atoke mwenyewe!