Nusu ya wako watoto ni wa kusingiziwa!

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,171
2,000
DNA: mkemia mkuu' kasema kuwa asilimia 44 ya waliopima vinasaba kwa ajili ya kujua uhalali wa watoto kwa baba, wamethibitishiwa kuwa watoto hao sio wao. My take: kwahiyo nusu ya watoto wa kitanzania sio wa wababa wanaoishi nao au wanao walea. Kwa ushauri wangu ninapendekeza watoto wote wakitanzania wapimwe ili wakabidhiwe kwa baba zao. Au mnasemaje wanaJF?
 
Oscardious

Member
Jun 28, 2012
24
20
..., hii inasikitisha sana kama upimaji huu wa DNA ni sahihi, basi inamaana 50% ya wapenzi au wanandoa wanamahusiano nje ya familia zao, na kwa maana hiyo itakuwa vigumu kwa njia na taratibu zote za kuthibiti VVU na Ukimwi kuweza kufanikiwa, kama watu bado wanajamiana hovyohovyo mpaka wanapatikana watoto nje ya ndoa. Mimi mwenyewe nimesikia habari hii kwenye kipindi cha magezeti yetu. Kweli inatiafedheha kwa wanafamilia, inabidi jamii yetu ibadilike.
 
Mlamoto

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
352
225
Kuna tatizo! Labda kifaa kibovu, au wataalamu wamekosea, sample iliyotumika siyo sahihi au kuna kingine ambacho hakijawekwa wazi.
 
Rubi

JF-Expert Member
Oct 5, 2009
1,620
1,500
Pengine na wewe uliyeleta mada umdhaniye babako kumbe siye ungeanza wewe kujipima. anayejua ukweli wa mtoto ni Mama chokochoko za nini?
 
hippocratessocrates

JF-Expert Member
Jul 1, 2012
3,601
2,000
Mkuu kbm, nadhani maelezo bado hayajatosha vizuri, ni asilimia 44 (44%) lakini ya watu wa ngapi waliopima?
Unajua inawezekana ni watu 100 tu, waliopima, Je, hiyo inatosha kusema asilimia "kubwa" ya jamii ya kitanzania(zaidi ya milioni 40) kuwa wana watoto/wazazi wasio wao?
 
Last edited by a moderator:

omujubi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
4,322
2,000
labda kama hizo mashine zao ni fake kama zile za wizara ya afya walizoingiza kupina HIV lakini kama ni kweli basi laana zitazidi kutuandama na huenda ikahitajika vizazi vingine kumi baada ya sasa kupata njia sahihi. Inasikitisha
 
kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,171
2,000
Mkuu kbm, nadhani maelezo bado hayajatosha vizuri, ni asilimia 44 (44%) lakini ya watu wa ngapi waliopima?
Unajua inawezekana ni watu 100 tu, waliopima, Je, hiyo inatosha kusema asilimia "kubwa" ya jamii ya kitanzania(zaidi ya milioni 40) kuwa wana watoto/wazazi wasio wao?

mkuu, kufuatana tafiti zinavyofanyika' mara nyingi inachukuliwa namba ndogo ya majaribio (samples) na kuwakilisha idadi ya kitu kizima, ndiyo maana mkemia mkuu katoa % inayowakilisha watu wote waliopimwa, kwahiyo % iliyopimwa inawakilisha % ya watanzania wote.
 
Last edited by a moderator:

sawabho

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
5,282
2,000
Mimi ambaye nina mtoto mmoja hiyo nusu hakuna !!! Hatahivyo, kama mtu anazaa nje ya ndoa ina maana hakutumia kinga, na kama hakutumia kinga kuna uwezekano wa kuambukizwa virus vya ukimwi.
 
Mr Ngoma

Senior Member
Jul 22, 2008
139
225
Guyz bora tupime nchi nzima ili kila aibuuu hata kwa viongozi wenye kumiliki watoto wasio wao tuwe wote ktk janga hili la mapungufu ktk uaminifu wa mahusiano!

Shida yake utaskia mfano: Mtoto wa waziri fulani (mfano: Joseph Robert) baba yake original ni Ali Said A K A Mpemba- aibuuu na mahakama itakulazimisha uchukue watoto wako, sasa balaa pale mtoto wa Upanga anarudishwa sombetini Arusha Hahaaaaaaa

Tupimwe nchi nzimaaaa!

Nawakilisha.

..., hii inasikitisha sana kama upimaji huu wa DNA ni sahihi, basi inamaana 50% ya wapenzi au wanandoa wanamahusiano nje ya familia zao, na kwa maana hiyo itakuwa vigumu kwa njia na taratibu zote za kuthibiti VVU na Ukimwi kuweza kufanikiwa, kama watu bado wanajamiana hovyohovyo mpaka wanapatikana watoto nje ya ndoa. Mimi mwenyewe nimesikia habari hii kwenye kipindi cha magezeti yetu. Kweli inatiafedheha kwa wanafamilia, inabidi jamii yetu ibadilike.
 
hippocratessocrates

JF-Expert Member
Jul 1, 2012
3,601
2,000
mkuu, kufuatana tafiti zinavyofanyika' mara nyingi inachukuliwa namba ndogo ya majaribio (samples) na kuwakilisha idadi ya kitu kizima, ndiyo maana mkemia mkuu katoa % inayowakilisha watu wote waliopimwa, kwahiyo % iliyopimwa inawakilisha % ya watanzania wote.

Natambua hilo, lakini hata kama ukijuliza mwenyewe what kind of sample is that?.. Nadhani itakuwa ni makosa kusema inawakilisha "watanzania wote" na ndio maana taarifa imesema asilimia ya waliopima hii haikuwa study ya watanzania, i think there's a difference mkuu.
 
Riwa

JF-Expert Member
Oct 11, 2007
2,597
2,000
DNA: mkemia mkuu' kasema kuwa asilimia 44 ya waliopima vinasaba kwa ajili ya kujua uhalali wa watoto kwa baba, wamethibitishiwa kuwa watoto hao sio wao. My take: kwahiyo nusu ya watoto wa kitanzania sio wa wababa wanaoishi nao au wanao walea. Kwa ushauri wangu ninapendekeza watoto wote wakitanzania wapimwe ili wakabidhiwe kwa baba zao. Au mnasemaje wanaJF?

Mleta mada ANAPOTOSHA tafsiri ya hiyo takwimu...nianze kwa kusema ni kweli imekuwa published kuwa 44% ya watoto ambao wanaenda kufanya kipimo cha vinasaba (DNA) kwenye ofisi ya mkemia mkuu imethibitika sio wao (baba). Lakini hii haina maana kuwa kati ya watoto wote wa kiTanzania karibu nusu sio wa baba wanaoishi nao...hii ni 'mis-interpretation' ya hiyo takwimu.

Hapa Tanzania, kipimo cha DNA kutambua mzazi halisi wa mtoto, hufanyika kwa maombi maalum toka 'Mahakamani' ambapo huwa na kesi ya kutambua mzazi halisi wa mtoto, kwa hiyo tayari umeshasegment sample yako kwa watu ambao kwa sababu moja au nyingine hawaamini kuwa ni baba halisi wa watoto hao...tayari hapo kuna mazingira ya kutoaminiana, na hivyo takwimu hii tayari iko biased na huwezi kuigeneralize kwa population nzima ya watoto wa kiTanzania....kosa ambalo mleta mada umelifanya.

Ili kuweza kugeneralize takwimu ili kurepresent general population, itabidi ufanye sampling kwa kutumia techniques sahihi za sampling kupata kweli sample size inayorepresent general population kuweza kugeneralize results zako. Kwa hiyo iwapo ofisi ya mkemia mkuu, wangechagua population sample ya watoto kwa ukubwa unaoshauriwa na kuwapima vinasaba, then hapo waweza sema asilimia 44% ya watoto wa kiTanzania...in short of that, NO!
 
Songoro

JF-Expert Member
May 27, 2009
4,124
0
Hesabu kweli gonjwa nyemelezi kwa vilaza wengi, Sylabus ipi ilokufundisha kuwa 44% ni nusu? Ungeendeleza u HKL wako bila kunajisi somo letu takatifu!
 
INGENJA

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
4,991
2,000
kuna DNA ya bibi zetu bwana acha za mzungu akiazaliwa mtoto,utaambiwa tu huyu wako au sio!!!
 
Rubi

JF-Expert Member
Oct 5, 2009
1,620
1,500
Mleta mada ANAPOTOSHA tafsiri ya hiyo takwimu...nianze kwa kusema ni kweli imekuwa published kuwa 44% ya watoto ambao wanaenda kufanya kipimo cha vinasaba (DNA) kwenye ofisi ya mkemia mkuu imethibitika sio wao (baba). Lakini hii haina maana kuwa kati ya watoto wote wa kiTanzania karibu nusu sio wa baba wanaoishi nao...hii ni 'mis-interpretation' ya hiyo takwimu.

Hapa Tanzania, kipimo cha DNA kutambua mzazi halisi wa mtoto, hufanyika kwa maombi maalum toka 'Mahakamani' ambapo huwa na kesi ya kutambua mzazi halisi wa mtoto, kwa hiyo tayari umeshasegment sample yako kwa watu ambao kwa sababu moja au nyingine hawaamini kuwa ni baba halisi wa watoto hao...tayari hapo kuna mazingira ya kutoaminiana, na hivyo takwimu hii tayari iko biased na huwezi kuigeneralize kwa population nzima ya watoto wa kiTanzania....kosa ambalo mleta mada umelifanya.

Ili kuweza kugeneralize takwimu ili kurepresent general population, itabidi ufanye sampling kwa kutumia techniques sahihi za sampling kupata kweli sample size inayorepresent general population kuweza kugeneralize results zako. Kwa hiyo iwapo ofisi ya mkemia mkuu, wangechagua population sample ya watoto kwa ukubwa unaoshauriwa na kuwapima vinasaba, then hapo waweza sema asilimia 44% ya watoto wa kiTanzania...in short of that, NO!
Unajua Riwa wengine wanakurupuka tu bora kasikia kichwa cha habari kwenye gazeti hata asijue habari ya kin inasemaje yeye huyo kwenye kibodi, Mimi ikitokea manaume ananiuliza eti huyo mtoto wanasema sio mwanangu nitamuuliza kwani wewe nani kakwambia yule ba mkwe ni baba yako mbona mimi najua sio baba yako tena siku nyingi tu. Kama unaona nakudandanya nenda kamuulize mama yako ndie anaujua ukweli na mimi niliupata kwake! then hatarudia kama sio ndoa kuleta sokomoko.
 
Last edited by a moderator:

LexAid

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
1,935
1,195
Positive Side: Watanzania wote ni nduu moja tunashare wazazi na watoto. Tumethubutu, Tutasonga Mbele.
 
HoneyBee

JF-Expert Member
Oct 23, 2012
912
1,000
Hii inajadiliwa pia hapa:

https://www.jamiiforums.com/mahusia...2-dna-nusu-ya-watoto-ni-wa-kusingiziwa-3.html

Jibu nililotoa ntaliweka hapa pia:

Aisee utawapa watu presha bure. Ujue hizi takwimu inabidi kuzielewa vizuri pia. Wanaoenda kupima DNA watakuwa na sababu za kutaka kuhakikisha kuwa mtoto ni wa kwao. Mfano labda kuna tetesi toka kwa majirani kuwa mke wa mzee fulani anatembea na jirani, mtoto katoka hafanani na baba, anafanana na muuza bucha, au labda kulikuwa na dalili za mke kumsaliti. Kwahiyo of course takwimu zinaonesha kwamba karibia nusu ya wanaopimwa DNA hazimatch. Ukisema upime nchi nzima DNA nina uhakika kwamba asilimia itakuwa chini zaidi.

Nilishatoa mfano kwenye thread nyingine. Unaweza kusema asilimia 97 ya wabakaji ni wanaume, lakini haimaanishi kwamba asilimia 97 ya wanaume ni wabakaji.

Kwahiyo unaweza kusema asilimia 44 ya waliopima DNA wamekuta watoto si wao, lakini haimaanishi kwamba asilimia 44 ya watoto nchi nzima ni wakubambikizwa. Pia hiyo sample ni chini ya watu 200 ambayo ni ndogo saana.

Anyways, kila siku kuna thread za kuzaa watoto nje na vimada. This is just the female equivalent, not as obvious!DNA: mkemia mkuu' kasema kuwa asilimia 44 ya waliopima vinasaba kwa ajili ya kujua uhalali wa watoto kwa baba, wamethibitishiwa kuwa watoto hao sio wao. My take: kwahiyo nusu ya watoto wa kitanzania sio wa wababa wanaoishi nao au wanao walea. Kwa ushauri wangu ninapendekeza watoto wote wakitanzania wapimwe ili wakabidhiwe kwa baba zao. Au mnasemaje wanaJF?
 
MVUMBUZI

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
5,184
2,000
Sijajua kwanini watu wame kuwa very defensive na hii topic. Tukiachana na sampling techniques na procedures zilizotumika kupata hiyo asilimia 44% hebu tuzame kwenye ukweli tuache malumbano. Wanawake wengi mno na wengine nawafahamu wamewachomekea waume zao watoto. Tushukuru Mungu wanaume wengi hawataki kujipa pressure kwenda kuhakiki kwa mantiki kwamba "kitanda hakizai haramu" Ila ndoa nyingi zingefanya DNA test za watoto wao tungekuwa shocked na results na huu ni ukweli wa mambo.
Wanawake wengi vijana na wa makamo wanajipatia huduma nje ya ndoa. Na kama vivyo hivyo wanaume. Mungu ameepusha wanaume wasibebe mimba kwani wangekuwa wanabeba basi kati ya watoto 3 ambao wangezaa basi mmoja tu ndiye angekuwa mtoto halali wa ndoa.
Hata hivyo wanawake wanajitahidi sana kupunguza hizi takwimu
 
Power G

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,892
1,225
DNA: mkemia mkuu' kasema kuwa asilimia 44 ya waliopima vinasaba kwa ajili ya kujua uhalali wa watoto kwa baba, wamethibitishiwa kuwa watoto hao sio wao. My take: kwahiyo nusu ya watoto wa kitanzania sio wa wababa wanaoishi nao au wanao walea. Kwa ushauri wangu ninapendekeza watoto wote wakitanzania wapimwe ili wakabidhiwe kwa baba zao. Au mnasemaje wanaJF?
Hata hivyo mimi siku zote naamini kwamba mtoto ni wa mama maana yeye hawezi kusingiziwa. Lakini ninyi akina baba tusaidieni tu kwa roho safi kulea kwa kuwa kitanda hakizai haramu.
 
Power G

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,892
1,225
Hata hivyo mimi siku zote naamini kwamba mtoto ni wa mama maana yeye hawezi kusingiziwa. Lakini ninyi akina baba tusaidieni tu kwa roho safi kulea kwa kuwa kitanda hakizai haramu.
Ndiyo maana mimi sijoa nasubiri nimpate mwanamke mwaminifu kama wewe ambaye atanifanya baba mzazi wa watoto wangu na siyo baba mlezi.
 
Power G

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,892
1,225
Ndiyo maana mimi sijoa nasubiri nimpate mwanamke mwaminifu kama wewe ambaye atanifanya baba mzazi wa watoto wangu na siyo baba mlezi.
Kuolewa napenda, lakini kama hiyo ndiyo picha yako kwenye avatar, mmmh siwezi. Labda dada Ciello anaweza kukubeba, mimi hapana kabisaaa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom