Nusu ya wakazi Dar kutopiga kura Desemba 14

...natoka nyumbani saa moja kamili kurejea ni saa tatu usiku, jumapili tu ndio napata nafasi tena mchana!
Sasa kama ulipata nafasi jumapili, nini kilikushinda kwenda kujiandikisha? Tunapenda haki, lakini hatuwajibiki! Basi tusilalamike kuwa kuna uongozi mbovu, kwa kuwa ni sisi ndio tumewaachia watu wengine watuchagulie viongozi hao!
 
Dar ndio watakaokwamisha ukombozi wa nchi hii.
Sehemu nyingi duniani ukombozi huanzia mjini na zaidi kwenye miji mikubwa iliyo na wakaazi wengi kutokea maeneo tofauti ya nchi. Ni tofauti sana na Dar iliyojaa mazuzu wasiojitambua na kuzidiwa na mikoa ya mbali. Wao huwa na majidai ya kujiweka bizi muda wote kiasi cha kuacha mambo ya msingi. Siku waitoka usingzni TZ itakuwa mbali sana.
 
acha ujinga uchaguz ni muhim sana ktk maisha tujenge utaratibu wa kushiriki siasa kikamilifu, ina maana hadi jumamosi na jumapili ulikosa hata dk 5 ya kwenda kujiandikisha maana vituo vilikua mitaan kwetu kabisa!!! na uzuri hakukua na folen kabisa tuache kulalamiak kwenye mitandao ya kijamii tu na kutukana bila kuchukua hatua!!!

Siyo ujinga, kwani kuna ubaya gani kutumia teknolojia kujiandikisha? kama wangetumia teknolojia huoni kwamba wengi wangejindikisha huko? Mimi nimejiandikisha siku ya mwisho lakini kuna watu wengi wameshindwa kwa sababu wanaondoka asubuhi na kurudi jioni wakati vituo vimeshafungwa.

Kuna njama za makusudi zinafanywa na Serikali ili watu wasijiandikishe, kama Mkuu wa mkoa wa Dar Said Meck Sadiki angekuwa na nia njema angewahimiza watu au hata kushauri mamlaka husika kuongeza muda wa kujiandikisha kutoka saa 10 jioni hadi saa 2 usiku. Serikali pia ingeweka online registration ili mtu ajiandikishe popote alipo.
 
Hii nchi inafurahisha sana yaani kampeni za sambaza upendo zilitangazwa zaidi kuliko Suala nyeti kama hili la Uchaguzi. Limefanywa kimyakimya kama biashara ya Bangi


Hata vyama vya siasa havikuona umuhimu wa kuhamasisha suala hili?
 
Signature?

Haswaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Hilo andiko naona kila leo linatimia kwa kasi ya ajabu.
Nahisi population sasa hivi ina stand kwa kila mwanaume mmoja kuna wanawake 6 au 7.
Ha ha ha ha ha ha
WHich means players have a wide range of toys to play with
Ha ha ha ha ha ha
 
Sababu kubwa imetajwa ni pilika za maisha miongoni mwa wakazi wa jiji hilo, ambao mara nyingi hutoka alfajiri na kurejea nyumbani usiku, muda ambao vituo vya kuandikisha vinakuwa vimefungwa.


Wiki moja ya uandikishaji ilikuwa haitoshi ila kwa vile ilikuwa njama ya CCM wamelazimisha iwe hivyo maana itawanufaisha wao na hii ni pamoja na kutokufanyiwa maboresho Daftari ya Mpiga Kura ilikuwezesha vijana wengi kujiandikisha.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki alitoa taarifa hiyo jana kwa waandishi wa habari. Alisema katika Halmashauri ya Wilaya ya Ilala lengo lilikuwa kuandikisha watu 329,726, lakini waliojiandikisha ni 184,850, sawa na asilimia 56.1.

Angalia tofauti. 144,876

Kinondoni walengwa walikuwa 850,000, lakini waliojiandikisha ni 272,869 sawa na asilimia 32, wakati kwa Temeke lengo lilikuwa kuandikisha watu 500,000, lakini walijitokeza ni 246,283 sawa na asilimia 49.2.


Angalia tofauti. Kinondoni 577.131 na Temeke 253717.

CCm wanaweza kuchekelea hali hii lakini kwa wataalamu hali hii siyo njema kabisa kwa ustawi wa jamii na hasa amani.
Panapojitokeza mgogoro wa kijamii wahawa ambao hawajajitokeza eti-pilika za maisha miongoni mwa wakazi wa jiji- watakuwa wa kwanza kurusha mawe kwenye mzimu wa matatizo yao. Na hili ni suala la muda/Bomu.


 
Wakazi wa Dar wanasifika kwa kula utumbo na miguu ya kuku. Unategemea watakuwa na akili ya kuniandikisha kupiga kura kweli?
 
Haswaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Hilo andiko naona kila leo linatimia kwa kasi ya ajabu.
Nahisi population sasa hivi ina stand kwa kila mwanaume mmoja kuna wanawake 6 au 7.
Ha ha ha ha ha ha
WHich means players have a wide range of toys to play with
Ha ha ha ha ha ha
Toys...Hahahahaaaaaa......let them not pass this way
 
Hata vyama vya siasa havikuona umuhimu wa kuhamasisha suala hili?
Nadhani ni jukumu la serikali kwanza halafu vyama vinafuatia. Mbona sauala la vitambulisho vya Taifa na Uandikishaji wa Daftaari la wapiga kura linatangazwa vya kutosha....
 
Nadhani ni jukumu la serikali kwanza halafu vyama vinafuatia. Mbona sauala la vitambulisho vya Taifa na Uandikishaji wa Daftaari la wapiga kura linatangazwa vya kutosha....


Vyama kama vyama vina nafasi kubwa katika hili, kwa mwendo huu ni vigumu kupambana na chama tawala kama hata uhamasishaji wa uandikishaji hakuna. Matokeo yake kwenye majukwaa wanaonekana watu wengi lakini siku ya kupiga kura hawaonekani. Kenya kwenye uandikishwaji UhuRuto walihakikisha ngome zao zote watu wanajiandikisha na kwenye upigaji wa kura wakahamasisha vya kutosha, hapa utamhamasishaji mtu akapige kura wakati hajajiandikisha?
 
Learn to understand before you argue. Usifikiri sote tunafanya kazi za kupumzika weekends. But anyway, don't you see a point in what I propose? Kama la, unastahili kuombewa.
acha kutafuta justification mkuu. Hii ni kitu ya mara moja katika miaka 5... kweli umeshindwa kupata siku 1 katika miaka hii 5 ujiandikishe? Unadhani mapinduzi yatafanyika hapa kwenye mitandao.... nyie mnatia aibu kweli kweli, ukiumwa unaenda kazini? Kwa nini usideshi hiyo siku moja angalau ukajifanya / jiona unaumwa ili utimize haki ---- ya kikatiba. Nimeshangaa kuona wana JF wengi hawajajiandikisha sijui wanategemea mapinduzi yatafanyika hapa jamvini!!!!! Plz plz uchaguzi mkuu wandugu mkajiandikishe ni aibu kama hata nyie wasomi hamfanyi hivo.... kuna rafiki yangu mmarekani wakati wa uchaguzi anapanda ndege kwenda marekani ili avote lakini wewe huwezi pitia kwenye kituo kujiandikisha na baadae kuja na sababu zisizo na mashiko. Na hapo ndo CCM wanapo pigia bao na ndo maana wanatoa muda mfupi tu wa kujiandikisha...
 
acha ujinga uchaguz ni muhim sana ktk maisha tujenge utaratibu wa kushiriki siasa kikamilifu, ina maana hadi jumamosi na jumapili ulikosa hata dk 5 ya kwenda kujiandikisha maana vituo vilikua mitaan kwetu kabisa!!! na uzuri hakukua na folen kabisa tuache kulalamiak kwenye mitandao ya kijamii tu na kutukana bila kuchukua hatua!!!
Kama sijasahau, uandikishaji ulianza Jumatatu 24 hadi Ijumaa 28/11/2014. Sasa hizo Jumamosi na Jumapili zingeingiaje hapo!
 
Kwa DSM pilikapilika za siku nzima pamoja na foleni imechangia kwa watu kujitokeza kujiandikisha, naona ni vyema ikatumika mbinu nyingine ya kuweza kuwapata ama kuwaandikisha wapiga kura si kwa daftari la uchaguzi wa serikali za mitaa bili pia kwa daftari kwa la uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na raisi. Napendekeza kuwe na mobile registration centre, ambapo mpiga kura anafuatwa aliko iwe kariakoo ama posta na kwingineko kwenye mkusanyiko ya watu.
 
Zinaweza kutajwa sababu lukuki zaidi ya watu kutumia muda mwingi kujitafutia riziki. Nakubaliana na baadhi ya wadau kuwa zoezi la kujiandikisha lilifanyika kificho kwanio hakukuwa na jitihada za makusudi kutoa elimu kwa umma hasa kupitia vyombo vya habari.

Nikisema vyombo vya habari simaanishi vilivyozoeleleka, radio, TV na magazeti, dunia imekwenda mbele kidogo, nasi hatuna budi kubadilika. Lakini hata ukitumia vyombo vilivyozoeleka ndugu zetu, wanaopfikiri kwa niaba "yetu", watapeleka kwneye TV, radio za mijini magazeti ambayo muda unavyokwenda yanendelea kupoteza wasomaji kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuimba "ukasuku" wa makongamano, warsha, semina n.k.

sababu nyingine ya watu kukataa kushiriki chaguzi ni kutokana na kukata tamaa na siasa na wanasiasa, hivyo kwao ni bora kujiepusha na mambo hayo ingawa ni gharama zaidi kuliko kujitenga nao.

Yote kwa yote, viongozi wabovu huingia madarakani kutokana na watu makini kuacha kutekeleza wajibu wao wa kiraia wa kupiga na kupigiwa kura
 
hapo hawajajiandikisha hafu matokeo ya uchaguz yakitoa utasikia yamechakachuliwa

CCM Wamechakachua kura za wajumbe wa bunge maalum la katiba mchana kweupe.Uchaguzi serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ndio yale yale. Suluhu pekee ni popular revolt.
 
Wala msipoteze mda wenu kubishana na walioshindwa kujiandikisha kwani tulioona umuhimu tulienda na tayari majina yetu yametoka ..kuandikisha kulianza tarh23 jumapili na mie nilijiandikisha siku hiyohiyo,lakini kuna watu wanajitetea hapa kana kwamba wao ndo wanafanya kazi pekee wengine hatuna kazi,nawaambieni kwa hapa dar watu wanapenda sana starehe kuliko wajibu,katika mambo mengi sana starehe zinawapotezea mda na hata huko makazini muda wao mwingi wanawaza starehe na umimi umewajaa sana
 
Back
Top Bottom