Nusu ya wakazi Dar kutopiga kura Desemba 14

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
557
500ASILIMIA 42 ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam ndiyo waliojitokeza kujiandikisha kwa ajili ya upigaji kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, utakaofanyika Desemba 14, mwaka huu.

Imeelezwa kuwa kati ya wapigakura 1,679,726 wenye sifa ya kujiandikisha, ni 704,002 tu ndiyo wamejiandikisha, sawa na asilima 42.

Sababu kubwa imetajwa ni pilika za maisha miongoni mwa wakazi wa jiji hilo, ambao mara nyingi hutoka alfajiri na kurejea nyumbani usiku, muda ambao vituo vya kuandikisha vinakuwa vimefungwa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki alitoa taarifa hiyo jana kwa waandishi wa habari. Alisema katika Halmashauri ya Wilaya ya Ilala lengo lilikuwa kuandikisha watu 329,726, lakini waliojiandikisha ni 184,850, sawa na asilimia 56.1.

Kinondoni walengwa walikuwa 850,000, lakini waliojiandikisha ni 272,869 sawa na asilimia 32, wakati kwa Temeke lengo lilikuwa kuandikisha watu 500,000, lakini walijitokeza ni 246,283 sawa na asilimia 49.2.

Uandikishaji wa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulifanyika kwa wiki moja kuanzia Novemba 23 mwaka huu. Kwa mujibu wa ratiba ya mchakato wa uchaguzi, vyama na wagombea sasa wapo katika kipindi cha kampeni hadi Desemba 13, siku moja kabla ya uchaguzi.

Akizungumzia changamoto walizokumbana nazo katika uandikishaji, alisema mbali na watu wengi kutojitokeza, pia kulikuwa na migogoro ya mipaka katika baadhi ya mitaa mipya ya Turiani na Kigezi kata ya Buyuni na Kiboga na Kichangani Kata ya Kinyerezi kwa upande wa Ilala.

Alisema nafasi zinazowaniwa ni wenyeviti wa mitaa 559 na wajumbe wa kamati za mitaa 2,795, ambapo sasa uhakiki wa majina unaendelea katika ofisi husika.
Pia, alisema mawakala wa vyama vya siasa walikuwa chanzo cha vurugu katika kujiandikisha katika baadhi ya vituo vya kujiandikisha. Alitoa mwito kwa vyama kufanya kampeni za kistaarabu.

Aidha, alikumbusha kuwa siku ya uchaguzi, vyama vya siasa haviruhusiwi kufanya kampeni; na kwa siku za kampeni, muda unapaswa kwisha ifikapo saa 11 jioni, kinyume cha hapo wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Maabara za JK Akizungumza utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya Kikwete la kuhakikisha kila shule ya sekondari ya Kata, inakuwa na maabara tatu za masomo ya sayansi kabla ya mwishoni mwa mwezi uliopita, alisema Dar es Salaam imekamilisha ujenzi huo kwa asilimia 97.

Alisema maabara 274 kati ya 281 zimejengwa na kufikia hatua mbalimbali za ukamilishaji, zikiwemo uwekaji masinki, mifumo ya maji safi na majitaka, umeme, meza na vifaa vya maabara.

CHANZO: Habari Leo
 
Pokola

JF-Expert Member
Jul 16, 2010
718
225
Ifike wakati nchi iwekeze kwenye teknolojia. Ni wakati muafaka sasa tume ianzishe utaratibu wa online registration. Mimi ukiniambia niache kwenda kutafuta mkate wa kila siku haiwezekani kabisa.

Lakini ningejiandikisha kirahisi tu online.
 
Adharusi

JF-Expert Member
Jan 22, 2012
13,894
2,000
Mmoja wapo ni mimi,sijajiandikisha,tena wapo karibu tu,hapa makuburi mtaa wa mwongozo,ukisoma katba serikali za mitaa wamepewa mamlaka wasiyoweza kuyatumia,nasubiri daftari la kudumu la kupigia kura nikajiandikishe kijijini kwetu
 
Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,044
2,000
walitoa muda mfupi sana wa kujiandikisha,hata katika family yangu tupo watu wazima sita hakuna aliyepata muda wa kujiandikisha...
_nilitamani niwape ukawa kura yangu ila sasa maisha magumu natoka nyumbani saa moja kamili kurejea ni saa tatu usiku,jumapili tu ndio napata nafasi tena mchana!
~~~alafu serekali hawakutaka hili jambo litangazwe sana sikujua lengo ni nini hasa,hata walipoombwa kuongeza muda bungeni pinda aligoma kabisa!!
 
bona

JF-Expert Member
Nov 6, 2009
3,801
1,250
Ifike wakati nchi iwekeze kwenye teknolojia. Ni wakati muafaka sasa tume ianzishe utaratibu wa online registration. Mimi ukiniambia niache kwenda kutafuta mkate wa kila siku haiwezekani kabisa.

Lakini ningejiandikisha kirahisi tu online.
acha ujinga uchaguz ni muhim sana ktk maisha tujenge utaratibu wa kushiriki siasa kikamilifu, ina maana hadi jumamosi na jumapili ulikosa hata dk 5 ya kwenda kujiandikisha maana vituo vilikua mitaan kwetu kabisa!!! na uzuri hakukua na folen kabisa tuache kulalamiak kwenye mitandao ya kijamii tu na kutukana bila kuchukua hatua!!!
 
Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,247
2,000
Hii dalili mbaya kwa uchaguzi wa mwakani huenda ikatokea hivi.
 
Pokola

JF-Expert Member
Jul 16, 2010
718
225
acha ujinga uchaguz ni muhim sana ktk maisha tujenge utaratibu wa kushiriki siasa kikamilifu, ina maana hadi jumamosi na jumapili ulikosa hata dk 5 ya kwenda kujiandikisha maana vituo vilikua mitaan kwetu kabisa!!! na uzuri hakukua na folen kabisa tuache kulalamiak kwenye mitandao ya kijamii tu na kutukana bila kuchukua hatua!!!
Learn to understand before you argue. Usifikiri sote tunafanya kazi za kupumzika weekends. But anyway, don't you see a point in what I propose? Kama la, unastahili kuombewa.
 
Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,389
2,000
Wiki moja nini maana yake unapolenga jambo kubwa hivi na ukijua hari halisi ya miji kama dar? hizi ndo hira za ccm
 
grafani11

JF-Expert Member
May 24, 2011
15,457
1,500
Katika hao 52% nami nimo. Parandesi ya 3 ya mleta uzi inahusika zaidi....
 
grafani11

JF-Expert Member
May 24, 2011
15,457
1,500
Wiki moja nini maana yake unapolenga jambo kubwa hivi na ukijua hari halisi ya miji kama dar? hizi ndo hira za ccm
Hii nchi inafurahisha sana yaani kampeni za sambaza upendo zilitangazwa zaidi kuliko Suala nyeti kama hili la Uchaguzi. Limefanywa kimyakimya kama biashara ya Bangi
 
grafani11

JF-Expert Member
May 24, 2011
15,457
1,500
acha ujinga uchaguz ni muhim sana ktk maisha tujenge utaratibu wa kushiriki siasa kikamilifu, ina maana hadi jumamosi na jumapili ulikosa hata dk 5 ya kwenda kujiandikisha maana vituo vilikua mitaan kwetu kabisa!!! na uzuri hakukua na folen kabisa tuache kulalamiak kwenye mitandao ya kijamii tu na kutukana bila kuchukua hatua!!!
Mtaani kwangu zozi liliendeshwa kimya kimya kiasi kwamba watu walijua sehemu kituo cha kujiandikisha kilipokuwa siku ya mwisho. Hiyo foleni siku ya mwisho ndiyo iliyofanya watu wengi washindwe kujiandikisha...
 
Tee Bag

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
7,186
2,000
Hiyo takwimu ni kwa mikoa takribani yote, tume pamoja na halmashauri wameshindwa kuhamasisha, huu uandikishaji umefanyika kwa siri kidogo ila wao wametonyana
 
Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
40,340
2,000
acha ujinga uchaguz ni muhim sana ktk maisha tujenge utaratibu wa kushiriki siasa kikamilifu, ina maana hadi jumamosi na jumapili ulikosa hata dk 5 ya kwenda kujiandikisha maana vituo vilikua mitaan kwetu kabisa!!! na uzuri hakukua na folen kabisa tuache kulalamiak kwenye mitandao ya kijamii tu na kutukana bila kuchukua hatua!!!
Hebu funga domo lako kenge wewe, kama uko busy muda wa kuja kujambajamba hapa JF unaupata wapi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom